Aliewaitaga nyani hakukosea kabisa,mpira sio maneno wala sio uhamasishaji,bado mna akili za kijamaa na kishoshalist kuamini propaganda inaweza kufanya kazi!!
Mpira ni uwekezaji,na management nzuri,duniani kote uko mpira ulipopiga hatua kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kuanzia kwenye wataalamu wa benchi la ufundi,wachezaji wazuri,vifaa vya mazoezi,vifaa tiba,lishe,na program tofauti za kiufundi.
Suala la makelele halina tofauti na waliopigana vita ya majimaji,kuamini kwenye propaganda kuwa wanaweza kuwashinda watu wanaotumia zana zenye teknolojia ya kisasa mwisho wa siku watu wakafa kwa kuamini ujinga,au walioamini propaganda za babu wa loliondo mwisho wa siku wakatumia kikombe kisicho na utaalamu na uthibitisho wa kisayansi wakafa!!
Watu wa Yanga kwa sababu ya ulofa wao, GSM amepoka madaraka kinyemela na sasa wanaongoza timu kwa manufaa ya kibiashara ya jina lao,bila kujali utamaduni wa timu hio,kama kweli yanga wanaitaji mafanikio waache kuwekeza kwenye propaganda wawekeze kwenye utaalamu zaidi.