Kumkaribisha Haji Manara Jangwani Ni Kosa Kubwa Sana!

Kumkaribisha Haji Manara Jangwani Ni Kosa Kubwa Sana!

Mtu mwenye akili timamu anawaza hivyo. Ndio maana huwa nasema tatizo la Yanga ni uongozi wao kutotumia akili
I hope kuna tahadhari wamezichukua kuhakikisha anafanya kazi katika uweledi unao takiwa zaidi.
 
Sina shaka na uwezo wake katika eneo lake. Lakini kitendo cha kuvuka mipaka ni jambo ambalo linatupatia hofu baadhi ya mashabiki wa Yanga SC.


Vilabu vyetu vya Mpira ni Taasisi kama zilivyo Taasisi zingine Duniani. Taasisi zote Duniani zimekua zikipambana kuhakikisha zinapata wafanyakazi Bora ambao wataifikisha Taasisi husika kwenye kilele cha Mafanikio. Bahati mbaya mpira wa Tanzania Kwasababu Kwa miaka mingi umekua ukiendeshwa kitamaduni. Soka letu Kwa miaka mingi limekua likiongozwa na mashabiki Wa vilabu badala ya watu Wenye Weledi, Taaluma na uzoefu wa kuhudumu Kwenye Idara mbalimbali za vilabu vyetu.

Mapinduzi makubwa ya kibiashara Kwenye soka la Tanzania yaliyochipua Kwa miaka ya Karibuni yanapelekea Mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kimfumo Kwenye Taasisi hizi. Kidogo Kidogo utaratibu wa mashabiki kuviongoza vilabu Bila kujali ubora,uzoefu na Taaluma zao unaenda kutoweka. Alianza Senzo kutoka SA mpaka Simba Akiwa sio mwanachama, Baadae akaibukia Jangwani. Tumeona aliekua Katibu Mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboraha akitambulishwa Azam FC, na hatimaye Leo Haji Manara amerejea "Umamani". Yanga Ni klabu yenye historia kubwa zaidi Nchini kuliko yeyote, inafanya mazuri lakini walikosa mtu wa kuyakweza na kuyasemea wanamwachaje mtoto wao anazagaa wakati ana mdomo wa Dhahabu???

Mwisho watu wanatakiwa kutambua Kwamba Yanga ni Zaidi ya klabu, Yanga ni utamaduni na utamaduni Una tabia ya kurithiwa. Haji Manara ni Nani asiwe sehemu ya mirathi ya Baba yake, wazazi wake na familia yake?. Karibu Jangwani HAJI, Hadithi za klabu kubwa Afrika Mashariki sasa inaenda kusimuliwa Kwa Sanaa na Ubunifu Wa kisasa. Haya Ni unblock Basi Tuungane kuipeleka mbele Yanga yetu tuliyoirithi.
 
Sina shaka na uwezo wake katika eneo lake. Lakini kitendo cha kuvuka mipaka ni jambo ambalo linatupatia hofu baadhi ya mashabiki wa Yanga SC.
Mimi sijapenda pia ila acha tutumie nguvu ya manara kujiweka sawa,jamaa ana kipaji cha uhamasishaji,usishangae siku na wanigeria kwa mkapa kukajaa pale,kingine tuwakere tu hawa 🐒 dadadeki
 
Tutumai iwe hivyo!
Ujinga Wakati Wa Kwenda Kurudi Njia Unaijua

Akirudia Yote Aliyoyafanya Simba Tutajua Ni Sikio La Kufa




Simba Na Yanga Upinzani Utani Ni Kwenye Mpira Tu
Mambo Mengine Yanakuwa Kawaida Sana
 
Unajua binadam sisi kila mmoja kazaliwa na kitu chake na nguvu fulani iliyo ndani mwake.

Tunatofautiana kuitumia.


Haji Manara, haraharaka ukimchek sio kitu ILA JAMAA ANA NGUVU KUBWA SANA , NGUVU YA KIUONGOZI NDANI YAKE, JAMAA ANA MAMLAKA.


nandicho kinamuweka mjini, Sisi tunapiga kelele, hafai hafai, ila ndio ivo imeshakua !!!.


Usishangae siku akatoka Yanga, akaenda Azam na BADO AKAKUBALIKA.
Aliwahi kuwa katibu mwenezi CCM pale wilaya gani sijui Dar, so ni mwanasiasa usishangae na sijashangaa

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nimemsikia Haji maneno yake wakati anakaribishwa,kwanza ameonyesha yeye hana mapenzi na Yanga kafata pesa,pili kaonyesha kuwa yeye ni mkubwa pale Yanga kwa masaa machache tu aliyotambulishwa.huyu atawavuruga tu pale,na kasema wazi hana tatizo na Simba,muda utaongea.
 
Mambo yanaenda kasi sana🤣
20210824_210654.jpg

20210824_210650.jpg
 
Nimemsikia Haji maneno yake wakati anakaribishwa,kwanza ameonyesha yeye hana mapenzi na Yanga kafata pesa,pili kaonyesha kuwa yeye ni mkubwa pale Yanga kwa masaa machache tu aliyotambulishwa.huyu atawavuruga tu pale,na kasema wazi hana tatizo na Simba,muda utaongea.
Huyu hana tatizo na Simba bali Mo na Babra. Ila hata kuja Yanga siyo kuwa ni ishu za michezo tu, bali ni muendelezo wa ushindani wa kibiashara kati ya GSM na Mo.
 
Back
Top Bottom