Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Na namba umeweka..That's nice,atakukumbuka kwenye ufalme wake


Sijaandika anikumbuke, mbona nimewataja wengine hapo.

Makonda nimeshamuandika kwa miaka mitano sasa, asinikumbuke kipindi hicho anikumbuke leo?

Kazi yangu ni kuandika, akikosea anasemwa, akinuna shauri yake, hata Mhe. Rais naye akikosea anasemwa, akinuna atajua mwenyewe.
 
Ni kawaida nikiandika nawekaga Mkuu. Hata nikikosoa naweka pia
Safi sana mkuu,ngoja nikutoe hofu CCM yote kuanzia Mwenyekiti,Bashiru,Polepole hakuna mwenye uwezo wa kumkata Makonda yaani hata wakae Vikao vya mwezi mzima uwezo huo hawana.
 
Yaani wakipatikana vijana kama makonda kama 20hivi Tanzania itapaa juu sana kiuchumi
 
Ni kweli kabisa, lakini kwenye nchi hii, vijana wachache wenye uwezo wa Makonda
Hatujabisha ndg. Lakini kitendo chake cha kutosikiliza maonyo ya wakubwa zake (raisi wake na mwenyekiti wake wa chama), kwamba asiache utumishi wa umma kwa tamaa ya ubunge inaonesha Makonda ni mtovu wa nidhamu.

Raisi kamvumilia kwa mengi sana. Ndio sababu alipochukua fomu, mheshimiwa akateua mtu jioni yake kuchukua kiti chake.
 
Katika Siasa za vijana, Makonda kamsaidia sana Magufuli kwa sehemu kubwa. Makonda ameshiriki matusi, katukanwa na watu wa ndani na nje ya nchi. Sijaona mpaka sasa aliyeonja uchungu na utamu kwa awamu hii kama Makonda. Mhe. Rais mwenyewe analijua hilo
Nilijua unasema anaongoza kwa kupendelewa na jiwe
 
Kwanza ni viongozi wavmchache sana waliongoza dar kwa kipindi cha miaka mitano wengi waliishia 2, 3, 1
 


Sio kosa kuonyesha matamanio yako kwa boss wako. Sio kosa.
 
6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO

Yaani hili nalo ni la kujivunia?
Badala ya mtu alete matumaini wewe unashangilia mtu kuleta hofu (Terror)?
Ajabu sana hii!
 

Sasa namba ya simu ya nini? Hebu tueleze unategemea nini kuweka namba ya simu.
 
Umeongea kimahaba Sana, Mtu akishatoa taarifa halafu akatia chumvi ikazidi inapoteza kabisa ladha hata ya habari yenyewe. Makonda Ni mtu anayefanya kazi kweli lakini matatizo yake Ni makubwa kuliko kazi anazozifanya.Kama humjui makonda Ni mbinafsi kuliko unavyoweza kufikiri, mtu ambaye anaweza kua tayari kupitisha bidhaa kinyemela kupitia cheo chake kidogo tu Cha RC akipewa wizara atafanya mangapi? Atuambie Mali alizozipata akiwa Rc tu tukimpa wizara itakuaje? Ni mtu hatari Sana Sana wakuogopwa hafai hata kwa kukopea sema ndio hivyo tu kipenzi Cha baba.
 
We ni mpuuz nilijua unasema anaongoza kwa kupendelewa na jiwe


Kama mtu anajipendekeza kwako kwa nini usimpendelee?
Mtu anatukanwa kwa kazi uliyompa kwa nini usimlinde?
Mtu ananidhamu ya kazi uliyompa bado usimbebe?
 
Umesahau moja ya sifa yake ya ujasiri. Kumpiga Mzee Warioba!
 
Wewe fani yako ni fasihi, huna jipya. BASHITE ni nani hadi asikatwe? Haya nenda kachukue mkwanja wako, kazi uliyotumwa umeimaliza.
 
Kwa hili hapana aisee
 


Wakifuata ushauri wako CCM watalipoteza jimbo la Kigamboni asubuhi kweupe.Makonda ni kijana mzuri lakini alikuwa bado anahitaji kujifunza kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…