Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Acheni siasa zenu za kishabiki na kipuuzi, jimbo lipo kwa Ndugulile miaka 10 sasa na halijapotea, sasa mnaanza kuleta ukanda na usukuma wenu humu! Kafieni mbali
 
Umenena vyema kwa upande wako, sio kosa kwake kumuambia Mhe. Rais matamanio yake pia. Kazi ya Ukuu wa Mkoa kafanya vizuri, bila shaka hata kazi ya ubunge atamsaidia zaidi na zaidi.

Wewe ni mpiga zumari wa Makonda na unaruhusiwa kuwa hivo. Lakini unaposema kazi za ukuu wa mkoa kazifanya vizuri, unafungua milango ya kuulizwa ni kazi zipi hizo.

a) watoto walioachwa na baba zao?
b) wanawake wanaopigwa na waume zao?
c) miradi ya wizara na halmashauri kusemwa na yeye?
d) kuzuia shisha na matamasha?
e) kuleta furniture za majumbani kwa jina la samani za mashule?

Ambacho hukujua muda wote huo ni kuwa Makonda ni populist na mpenda kuonekana. Na alifanya mambo yanayoweza kumfanya akaandikwa kwenye magazeti au vyombo vya habari TU!! Alitafuta kuwa maarufu!! Alionesha kuwa Rais TU ndio lolote na wengine si lolote!! Alitoa matamko yanayohusu Dar es Salaam utadhani yeye ni Rais wa nchi. Tuna bahati wakuu wa mikoa mingi hawakuiga tabia zake kama walivoshauriwa. Tungesikia mambo ya ajabu sana kama wangeamua kuiga!!

Maamuzi ya wapiga kura wa CCM yaheshimiwe. Kwa CCM jambo hili ni kipimo. Wasipoheshimu haki ya mshindi Ndugulile, hawawezi kamwe kuwa na serikali inayoheshimu haki za mwananchi yeyote. Heshima na haki huanzia nyumbani!!!!
 
Mtulia kumbuka wewe ndie ulisababisha mauaji ya Binti mrembo Acwilina, wewe ndie ulisababisha wenzako kufungwa na kulipa mamilioni ya shs! mshahara wa dhambi ni mauti na laana ile itakuandama ktk maisha yako yote.
 
Ujumbe umefika kwa Magufuli ni kuwa aliowatumbua wengi wanapendwa na wananchi, Ndungulile na Makamba ni mfano.

Gambo na Bashite wote si wasafi lakini wameamua kumbakiza Gambo.
Na nape alimtumbua, but kashinda kwa kishindo
 
Toa kabisa kwenye orodha Tundu Lisu na makanjanja wenzie!

Kitu kingine ambacho nafikiri akili yako imeshindwa kukitambua ni kwamba Tz Ina watu 60 mil... Humo tumo wengi Sana tunaofaa Mara Mia kwa hao uliowataja!

Magu ni mzee wa kuangalia nje ya box, hiyo ndio inamtofautisha Sana yeye na Marais wengine. Na hii hupelekea wengine kufikiria Kuwa hashauriki! Mungu azidi kumuongoza, kumlinda na kumbariki rais wetu mpendwa Dr. John Magufuli na nchi yetu yote!
 
Kukatwa sio tatizo sababu unapoingia uwanjani tegemea kushindwa au kushinda.Aje huku Sengerema tuvue samaki si walishasema tujiajiri.
 
Bwana mdogo mpiga debe wa Makonda, tulikuambia lakini ukashupaza shingo.
Mtoto akililia wembe mpe.
 
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI

Na, Robert Heriel

Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia moja mfano wa Makonda ambao watakuwa nchi nzima kwa ajili ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii.

Ni muhimu Makonda akipitishwa na CCM katika nafasi ya ubunge kisha baadaye apewe nafasi ya uwaziri katika wizara zinazowahusu vijana, burudani na michezo.

Kwa nini Makonda ni kete muhimu kwa siasa za sasa hapa nchini?
Hoja zifuatazi zitahusika;

1. UJASIRI
Makonda ni kijana jasiri asiye mwoga. Ni moja ya vijana wachache hapa nchini ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika uongozi, Makonda matukio aliyojiingiza yanambeba licha ya kuwa hajafanikiwa sana lakini angalau tuliona nia yake. Kuna mambo kuyafuatilia lazima uwe na roho ya kikulungwa, roho ya simba. Kufuatilia Wauza Madawa ya kulevya ni moja ya mambo ambayo ni magumu sio hapa nchini hata duniani kwa ujumla.

Makonda ni jasiri kwani haogopi kusimamia kile anachokiamini. Watu waoga huwa hawana Msimamo. Kilichomwangusha Makonda ni mipaka ya mamlaka katika kazi yake.

2. MWANAJAMII
Makonda ni moja ya viongozi wasiojifungia ndani. Huchangamana na jamii. Sio wale viongozi ambao wakipewa nafasi hujifungia ndani muda wote maofisini, kumuona tuu utahangaika mpaka ukate tamaa. Hii ni tofauti na Makonda, yeye anapatikana muda wowote, ukifika ofisini kwake hakuna milolongo ya ajabu ajabu. Makonda ni kawaida kumuona kwenye matukio ya kijamii mathalani matamasha ya vijana ya burudani na michezo, matukio ya misiba, n.k. Hii ni tofauti na viongozi wengine. Kiongozi lazima achangamane na jamii.

3. USTAHIMILIVU
Kama kuna vijana wavumilivu kwenye hili taifa ni pamoja na Makonda. Moja ya vijana walioonja joto la jiwe awamu hii mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni pamoja na Makonda. Licha ya kashfa kibao kama vile Kufoji vyeti, ambapo mahasimu wake walidai alicharaza mswaki kidato cha nne kwa majina yake halisi Daudi Albert Bashite. Hilo akalivumilia, kashfa za kuwa anatabia za kishoga, nalo akavumilia, kashfa za kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto, yote alistahimili.

Pengine aliniudhi siku moja aliyolia kanisani, ile siku alijishushia credit. Mwanaume kulia lia mbele za watu sio jambo jema hasa wanaume shupavu. Hata hivyo halimuondolei sifa zingine lakini namuasa, siku nyingine asilie lie mbele za watu. Mwanaume kulia lia ni dalili ya udhaifu.

4. DHAMIRI YA DHATI YA KUISAIDIA JAMII
Makonda ni moja ya viongozi waliojipambanua katika kuisaidia jamii yake hasa kwenye Mkoa aliopewa auongoze. Makonda amesaidia vikundi vingi vya kina mama na vijana. Makonda ameonyesha nia za kuwasaidia watoto na kinamama waliotelekezwa na waume zao. Makonda ameonyesha nia ya kuwasaidia wale walioonewa kisheria kwa kuwawekea wanasheria, Makonda kajitahidi kupunguza uchafu wa jiji la Dar es Salaam, Makonda kajitahidi kurejesha usalama jijini Dsm kwa kupunguza vikundi vya Panya Road, sijui watoto wa Mbwa n.k.

Makonda anaweza asionekane ni kijana bora labda kutokana na tabia yake ya kujitukuza, na kutoa maneno ya shombo ambayo kwa sehemu kubwa nafahamu analenga kujifariji na kuwaumiza adui zake. Kwa kawaida kisaikolojia watu wanaotoa maneno ya shombo huyatamka kama njia ya kujifariji na kuondoa sonona, na kuwaumiza adui zao.

Wapo wakuu wa Mikoa wengi lakini waliofanya kama makonda hawafiki kumi. Hii ni dalili kuwa Makonda anafaa kupewa nafasi zaidi ya ukuu wa Mkoa.

5. MSAADA MKUBWA KWA MAGUFULI
Kama kuna watu waliomsaidia Mhe. Magufuli katika uongozi wake basi ni pamoja na Makonda. Imekuwa ngumu kumtenganisha Magufuli na Makonda katika siasa za awamu ya tano. Makonda amekuwa moja ya wabadilisha upepo katika masuala yanayotokea hapa nchini. Kwa namna hii amekuwa msaada mkubwa katika siasa za awamu hii. Makonda haoni shida kusemwa yeye kwa kupoteza mada fulani iliyokuwa inavuma ikiisakama Serikali.

Pengine Makonda asiwe na ushauri wa maana kwa Magufuli lakini kiukweli anamchango mkubwa katika kubadili upepo wa mambo yanayovuma hapa nchini. Hili pekee linatosha kwa Magufuli kumkubali Makonda. Kumzima Makonda kwa wakati huu sio uamuzi wa akili. Nyota yake inang'aa lazima itumiwe kwa maslahi ya nchi.

6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO
Makonda ni moja ya viongozi wachache waliofanikiwa kuleta utisho kwa watu wengi hapa nchini. Watu wa kawaida na viongozi wengi wanamuogopa Makonda. Kujenga hofu ni moja ya mambo ya muhimu katika utawala. Hofu hufanya utekelezaji uende kwa haraka. Makonda kwa cheo alichokuwa nacho cha ukuu wa Mkoa hakilingani na hofu aliyoijenga ndani ya jamii yake. Wengi humheshimu kupita cheo alichonacho.

7. BINGWA WA UHAMASISHAJI NA UCHANGISHAJI
Kiongozi sharti awe amebobea katika kuhamasisha watu. Makonda anajua kuhamasisha watu. Makonda anauwezo wa kuwachangisha matajiri, Akawaweka pamoja wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu. Makonda anauwezo wa kuhamasisha vyombo vya habari vizungumzie jambo fulani. Tumeona mara kadhaa Makonda akikodisha kumbi za gharama kwa ajili ya tukio fulani mpaka wengine wanasema huyu Makonda anatoa pesa wapi. Makonda ni mhamasishaji na mchangishaji kwa wale atakaowaona wadau wa maendeleo.

Matajiri watachanga iwe kwa kumuogopa au kwa upendo. Hiyo haitamhusu Makonda ilimradi lengo limefikiwa.

Viongozi wengine katika hili walishindwa kabisa.

Magufuli anahitaji vijana kama hawa, watu kama Makonda, Tundu Lisu, Jokate, Anthony Mtaka, Prof jay, Ally Hapi, GJ Malisa, Ole Mushi, Ole Sebaya, Sugu, Profesa Mkandara, Ummy Mwalimu, Joyce Ndalichako, Suleiman Jafo, Bashe, Kassim Majaliwa, Bashiru, Ester Bulaya, miongoni mwa viongozi wengine wenye sifa.

Nafahamu kila mmoja ana mapungufu lakini kwenye mizani; ubora uzidi mapungufu.

Makonda apewe nafasi kwani ni mtu anayejirekebisha kila uchwao, sio mtu wa kutoa boko tena kama zamani alipokuwa mgeni wa kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300.

Kwenye siasa lolote laweza kutokea
Kwenye maisha😂😂
 
Sentensi yako ya mwisho inadhilisha wewe ni member wa kundi la rabid hater wa Makonda, kwa maneno mengine mnakuwa driven na chuki binafsi na wivu juu, bahati mbaya vinara wenye chuki binafsi wako kwenye rika ya vijana!! Badala kufanya mambo ya kujiendeleza na kujipatia kipato cha ziada, wanashinda kwenye social media wakimsema vibaya MAKONDA.
Mimi ni muumini wa humanity,so kila mtu anayo haki ya kuishi,kuona Jamii ikiteswa,umizwa,fanyiwa uovu ni against humanity.
 
Sentensi yako ya mwisho inadhilisha wewe ni member wa kundi la rabid hater wa Makonda, kwa maneno mengine mnakuwa driven na chuki binafsi na wivu juu, bahati mbaya vinara wenye chuki binafsi wako kwenye rika ya vijana!! Badala kufanya mambo ya kujiendeleza na kujipatia kipato cha ziada, wanashinda kwenye social media wakimsema vibaya MAKONDA.
Tetea msukuma mwenzako, pinga maumivu ya wengine
 
Yaani wakipatikana vijana kama makonda kama 20hivi Tanzania itapaa juu sana kiuchumi
Hahaha,Makonda alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Daresalam aliamrisha watu waanze kunywa pombe saa 10 jioni,yaani Baa zianze kufunguliwa kuanzia saa 10 jioni kwa siku za kazi..

Daresalam Salam Ndi mji mkubwa wa Biashara Tanzania

Mji wenye Bandari inayotegemewa na Nchi jirani, watu kutoka nchi za jirani Kama vile Rwanda,Congo,Zambia nk,humiminika Dar kibiashara..

Kufungwa kwa Baa kumeifanya Dar kukosa sehemu za kukutania watu,kumeifanya Serikali kukosa Kodi,raia kukosa ajira,nk

Miji yote mikubwa ya Biashara kuanzia Dubai,New York, Copenhagen, London, Paris,Ni miji ambayo watu hawalali,iko busy 24hr..

Binafsi amri Ile ya kufungua Baa saan10 jioni nimeona kuwa Makonda hana uwelewa wa anachokifanya,alikurupuka
 
Labda mleta uzi huu asichoelewa ni kuwa kilichomtokea Makonda ni msaada mkubwa sana kwa Mhe. Rais. Watanzania wanajua kuwa sakata la majina na vyeti vya Makonda halikwisha na kwa kweli sasa ndio ulikuwa wakati mzuri wa kulifikisha mwisho kwani kugombea kwake na hata kama angeshinda suala hilo lingepelekwa tume na tume ikileta figisu lingefika mahakamani kupinga ushindi wake. Mhe Rais amepata fursa ya kutupa nyama chini ili kuachana na nzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo unaempigia debe sidhani kama anania ya kusaidia raia ...mkuu wa mkoa ana nafasi kubwa sana ya kutumikia raia wake kuliko mbunge ...huwezi acha ukuu wa mkoa ukachukue fom ya ubunge kama kweli unania ya kutumikia raia,,

Nkujuze tu

Mkuu wa mkoa ana mshahara mkubwa kuliko mbunge

Huo ni mshahara

Mbunge ana posho kubwa kuliko mkuu wa mkoa

Kikao unajua kabisa ni 240k per day kwa muda bunge litakavokuepo

Plus posho ya milion 8 pesa ya kujikimu je

Haya ukistaafu yan ile miaka 5 ikiisha una kama 240mil kama asante😁😁 hivi huoni kama anafata hilo swala??

Maana kutumikia raia kama unataka basi ukuu wa mkoa ndo unaweza kwa asilimia 100
 
Back
Top Bottom