Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli kimeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhihirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.
Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.
Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za magharibi..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?
Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.
Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza mgawanyiko mkubwa huko mbeleni.
Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania, nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibi kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.
Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme tu ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.
Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.
Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?
Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.
Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
Mkuu
Kwanza nishukuru umekiri Magufuli hajuwa malaika ambacho ni kweli tupu.
Pili Magufuli alikua mtumishi wa umma kupitia utumishi wake unapimwa au matumizi yote aliyoyafanya au kuidhinisha huwa yanakagulia.
Tatu Kama kiongozi wa umma alipewa miongozo mbalimbali Kama instruments za kumsaidia kufanya maamuzi yote aliyopaswa kufanya.
Sasa tukiangalia ubinadamu wake na Kama kiongozi aliyopaswa kuyafanya hapa ndipo tunapopima utendaji wake na kumpongeza kwa mazuri na kulaani mabaya yake.
Report ya CAG imeonesha pasipo kificho kwamba kumekuwa na madudu mengi Sana kwenye serikali ya mwendazake. Kibaya mwendazake alisema hadharani hakuna anayewaza kula fedha za umma. Report inatuonesha mabillion yameliwa na hayajawatokea kila palipo wazi Kama alivyosema mwenda zake.
Tukumbuke hii report ni ya 2019/2020 ambapo mwendazake aliisimamia mwanzo mwisho. Lakini pia report ilikua inafuatilia mapendekezo ya nyuma yaani 2016-2019 utekelezaji wake hatukusikia wakifungwa.
Hivyo Kama wezi alikaa nao alikula nao eg. Waziri wake Kigwangalla na hakuna hatua alichukua. Nani alaumiwe?
Kwa hiyo serikali ya Magufuli ilikua ya kifisadi Kama zilivyokuwa hizo zingine. Lakini hii imekula zaidi ya hizo zingine.
Hoja eti kando ya ziwa ndio Muhimili wa CCM huo ni uongo. Ukitaka nikuthibitishie nitafanya hivyo.
Pili eti umati mwingi uliojittokeza kuaga ulikua unamsupport Magufuli sio kweli. Kwa sababu wengi wa watanzania hawakuwahi kuona au kusikia Rais aliyeko madarakani kafa. Hivyo wapo kweli waliokua mashabiki wake lakini wapo wengi Sana walioenda tu kuona imekuaje. Lakini wapo waliokuwa na chuki nae walioenda kuhakikisha ni kweli amekufa?
Hivyo ummati wa msiba hauwezi kukupa picha nzuri hata kidogo.
Hebu Rudi nyuma miezi 6 wakati wa kampeni bila malori kulikua na Hali gani? Kwa Nini wanafunzi na walimu walilazimishwa kwenda kwenye kampeni?
Ni hayo kwa leo