Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Kifupi kabisa bila kumung'unya maneno ni kuwa JPM ndiye aliligawa Taifa kwa itikadi za kivyama. Aliwaona wapinzani ni adui,wasaliti na wasiostahili mema ya nchi hii. Kinachoonekana sasa baada ya kifo chake ni mavuno ya chuki aliyoipandikiza mwenyewe.
 
Hayo ni maoni yako tu.

Na hao unaowaita Watanzania wajinga na wasio na uelewa nao wanaweza kukuona wewe u mjinga na uliye na uelewa wa chini.

Kujiona una akili haimaanishi kwamba una akili kweli.

Haupo vile ujidhaniavyo.
Utawala wa magu ulikuwa upo vizuri mno kwenye propaganda, hao unaosema walimpenda walikuwa ni victim wa propaganda zake

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Walikua wanapagawa sana na vihela vya uwizi...
 
Ona huyu nae,Message was sent clearly wakati wa msiba wake! Huu ndiyo ukweli na hauwezi kuuficha. Kanda ya Ziwa especially Mwanza-Geita to Chato walituma message kwa Taifa hili. JPM atabaki kuwa shujaa wetu.
We mnyamwezi gani! Huna akili?

Siku zote kibaya chajitembeza kizuri chajiuza

Magufuli angekuwa kiongozi mzuri wala usingeskia kelele zote hizi unazoziskia.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Sizani kama Watz wana tabia ya kuwasema marehemu tena hadharani hasa kwa mambo mabaya.Hakuna aliye mkamilifu Ila kwa unafiki watz mnatisha sana.
 
Sema ninalia.
Tunalia ndio nini?
Basi na mimi ngoja nikuunganishe kwenye langu.
Hatulii na tunatamani angechimbiwa Kaburi kilometa moja.
Na ma vyeti yako feki akakutumbua lazima umchikie.
Kwani wewe hutokufa? Majambazi lazima mmchukie magufuli.bora yeye kazikwa je vip wewe unajua utafia wapi? Na utazikwa wapi?
 
Kila mtu ashinde mechi zake. Usinipangie wala usinifundishe kuhuzunika. Nyie mnaohuzunika endeleeni, na sisi tunaishangilia msiba tuacheni tufurahi.

Magufuli alikuwa kila wakati anasema "NIOMBEENI", baada ya hapo anaua watu, ana dhulumu, anasema uwongo na anaiba fedha za Watanzania. Watu kweli WAKAMUOMBEA afe na apotee. Ogopa sala za watu wengi waliodhulumiwa wakiomba kwa pamoja
 
mtu anayemsifia mwendazake atakua hajui kilichokua kinaendelea nchini. huyu kwa chuki zake bnafsi kapoteza wafanybiashara wakubwa, wasomi na wanasiasa wanaojitambua. aliharibu kila seem hata sehem ambazo hupaswi kuzichezea kwa sababu zinazobeba maisha ya watu moja kwa moja km kule mifuko ya jamii kaivuruga kwa kukwapua ela za wastaafu alafu anaua soo kwa kujifanya anaiunganisha mifuko yote na kuleta kikotoo kipya. ona sasa wazee wetu wanavohangaishwa. huyu alikuwa wa kumwongezea kina cha kabur lake tu.
 
Sasa ungeanzia wap kumpenda na vyeti vyako feki?
Sina vyeti feki na sijawahi kufanya kazi serikalini

Ila ukweli ndio huo hta km huutaki! Magufuli alikuwa rais wa hovyo sana

Kilifanya watu km nyie kumuona mtu wa maana ni propaganda zake baada kupiga pini vyombo vya habari vyote

Kwa akili zenu finyu mkamuona malaika wakati alikuwa anaidumbukiza nchi shimoni

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mbona watu mmejaa chuki na ukabila sana au rais kuwa msukuma au ulitaka atokee kabila lako? Daima chuki sio jambo jema.HESHIMA YA MAGUFULI ITABAKI DAIMA.
 
Mkuu

Kwanza nishukuru umekiri Magufuli hajuwa malaika ambacho ni kweli tupu.

Pili Magufuli alikua mtumishi wa umma kupitia utumishi wake unapimwa au matumizi yote aliyoyafanya au kuidhinisha huwa yanakagulia.

Tatu Kama kiongozi wa umma alipewa miongozo mbalimbali Kama instruments za kumsaidia kufanya maamuzi yote aliyopaswa kufanya.

Sasa tukiangalia ubinadamu wake na Kama kiongozi aliyopaswa kuyafanya hapa ndipo tunapopima utendaji wake na kumpongeza kwa mazuri na kulaani mabaya yake.

Report ya CAG imeonesha pasipo kificho kwamba kumekuwa na madudu mengi Sana kwenye serikali ya mwendazake. Kibaya mwendazake alisema hadharani hakuna anayewaza kula fedha za umma. Report inatuonesha mabillion yameliwa na hayajawatokea kila palipo wazi Kama alivyosema mwenda zake.

Tukumbuke hii report ni ya 2019/2020 ambapo mwendazake aliisimamia mwanzo mwisho. Lakini pia report ilikua inafuatilia mapendekezo ya nyuma yaani 2016-2019 utekelezaji wake hatukusikia wakifungwa.

Hivyo Kama wezi alikaa nao alikula nao eg. Waziri wake Kigwangalla na hakuna hatua alichukua. Nani alaumiwe?

Kwa hiyo serikali ya Magufuli ilikua ya kifisadi Kama zilivyokuwa hizo zingine. Lakini hii imekula zaidi ya hizo zingine.

Hoja eti kando ya ziwa ndio Muhimili wa CCM huo ni uongo. Ukitaka nikuthibitishie nitafanya hivyo.

Pili eti umati mwingi uliojittokeza kuaga ulikua unamsupport Magufuli sio kweli. Kwa sababu wengi wa watanzania hawakuwahi kuona au kusikia Rais aliyeko madarakani kafa. Hivyo wapo kweli waliokua mashabiki wake lakini wapo wengi Sana walioenda tu kuona imekuaje. Lakini wapo waliokuwa na chuki nae walioenda kuhakikisha ni kweli amekufa?
Hivyo ummati wa msiba hauwezi kukupa picha nzuri hata kidogo.

Hebu Rudi nyuma miezi 6 wakati wa kampeni bila malori kulikua na Hali gani? Kwa Nini wanafunzi na walimu walilazimishwa kwenda kwenye kampeni?

Ni hayo kwa leo
 
Ligawike Mara nyingine?
 
Aliyeondoka ashaondoka hana chake.
Ukitenda mema umeitengenezea jina jema uzao wako.Uzao wa idi amin,bokasa, hitler hauna thamani kwenye Jamii kama uzao wa bob marley, mandela,ghandi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…