Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Hayo ni maoni yako tu.

Na hao unaowaita Watanzania wajinga na wasio na uelewa nao wanaweza kukuona wewe u mjinga na uliye na uelewa wa chini.

Kujiona una akili haimaanishi kwamba una akili kweli.

Haupo vile ujidhaniavyo.
Na ndio mjinga kiwango cha Paschal mayala.
Alafu anajifanyaga anamjua huyu Dicteta uchwara kutuzidi sisi.
 
Hayo ni matunda ya Magufuli mwenyewe. Alipokua madarakani alihubiri ukanda, uchama na upendeleo kwa wachache.

Acha taifa ligawanyike tu sababu ndio yalikua maono ya shujaa wa Afrika.
 
Kukariri na kurudia rudia tu maneno bila hata ya kujua maana yake!

FOH with your monkey see monkey do nonsense.
Usichukie bana na usipanic ukaanza kutukana mitusi hovyo, kama unataka kufa nawewe ili ukamtetee vizuri huko kuzimuni usitupigie kelele hapa.
 
Wajinga tu ndo wanamchukia magufuli. Watu mpaka sasa hivi tunalia. Haya maumivu ni zaidi ya maumivu
Sema ninalia.
Tunalia ndio nini?
Basi na mimi ngoja nikuunganishe kwenye langu.
Hatulii na tunatamani angechimbiwa Kaburi kilometa moja.
 
Nyie mnao taka huyo magufuli aonekane mungu mtu ndio wajinga sana mbona kikwete alisemwa sana tena akiwa hai na magufuli tena wazi wazi kwa vijembe mbona mlikaa kimya?

Nyie wasukuma tuondoleeni upuuzi wenu huyo mtu wenu kama mnaona ni malaika nendeni kaburini kwake mkamtukuzie huko huko tuondoleeni upumbavu wenu.

Mtu asiye taka kukaguliwa anafunga watu midomo watu wasiseme mapungufu yake sasa watu wameyakusanya maovu sasa wamepata nafasi ya kuyaongea sasa wanayaongea mnalalamika nini sasa.
Unachouza, nanunua!!
 
Ndiyo matunda ya kuziba watu midomo
Umezibwa mdomo kwa hiyo unapumulia chini au?

Kama ungezibwa midomo ungeweza kumtukana humu siku zote huko nyuma?
Kuweni wakweli na mambo ya hovyo acheni.
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.
Walikuwa wangapi hao watu.

Milioni 40?

Ukiona watu laki moja hao ndio "uraiani"?
 
Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli imeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.

Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.

Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za maghariba..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?

Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.

Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza magawanyiko mkubwa huko mbeleni.

Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania. Nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibu kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.

Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.

Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?

Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.

Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
Usiwe dwanzi, kibinadamu mema 10 hata 50 yanaweza kufutwa na ubaya mmoja tu! Sasa kwa bahati mbaya sana mabaya yake machache ni mazito mno kuliko makalvati, madege, maji, zahanati ma elimu bure! Kutembea miaka 5 unapandikiza chuki, kujimwambafy, kutokuheshimu katiba, ubabe, ukatili na kutokujali thamani ya uhai wa binadamu, watu wanapotea, watu wanauwawa, watu wanapigwa risasi anakaa kimya! Makalvati hayamlindi ng'o!
 
Nyani Ngabu et al pro magufulis

huyo mtu wenu angekuwa anakubalika kanda pendwa,basi kwenye GE 2020 wizi wa kura ambao siye wingine tulisaidia kuufanikisha basi ungetokea sehemu nyingine tu na si kanda ya ziwa.

ila uliza uambiwe!

si simiyu,geita,mwanza,mara,tabora au kagera kote kura za masandarusi ziliingizwa kwenye vituo.

sasa kama hao watu wengi wa mikoa karibu ya sita walishindwa nini kumjazia kura huyo mwana kanda ya ziwa mwenzao mpaka kutegemea kura za mifukoni?

kinachoshangaza kipi kilichowashinda hawa watu unaowaita wengi ambao walisindikiza jeneza lake wasiende kumjazia kura badala ya kutegemea za wizi?

uzuri ushaidi wa kura za wizi kuanzia picha mnato au vidio vyote vipo,tena hata huko kanda pendwa!

halafu the political cyber atmosphere on all online platforms ni tofauti na huko nje.

hakuna wasukuma wenye mawazo kama ya mleta mada.

eti wasukuma wanakasirika tukimpopoa aliekufa!

ukitaka kuamini,we subiria 2024 na 2025.
 
1.5 tirion ilipotea kipindi cha nani?
Na usituchanganye kabisa , Kikwete aliruhusu watu kujadiri Wizi kwenye Nchi yao, yeye hata Kukopa alikuwa anakopa kwa siri

Uchumi wa Gizani

Yaani maufisadi yoooote ya Kipindi cha Kikwete uliyoyasema , tuliyajua kwasababu Kikwete mwenyewe alitaka tuyajue, angetaka kuficha angeweza na angetoka madarakani bila kuwa na rekodi unazosema,

Kuficha tatizo, haina maana kwamba hakuna tatizo, limefichwa
Kinyesi ni kinyesi, hata ukikificha jikoni kitaendelea kunuka tu.
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.
Inawezekana alipendwa sana, lakini bado napinga kwamba ule wingi wa watu msibani ni sababu ya upendo! Siwezi kuamini kwamba wale wana familia watano waliokanyagwa hadi kufa, walimpenda sana mwendazake hata wakatoa maisha yao kwa ajili yake! Kuna walio mpenda, tunakubali, lakini waliokua hawampendi wapo, Twitter, Ufipa, Bungeni, kwenye cabinet yake mwenyewe, Kigwa, Kafupi na wengine wengi!
 
Umezibwa mdomo kwa hiyo unapumulia chini au?

Kama ungezibwa midomo ungeweza kumtukana humu siku zote huko nyuma?
Kuweni wakweli na mambo ya hovyo acheni.
Hamkutaka habari za kiuchunguzi hadi mkaanzisha magenge ya eti watu wasiojulikaana
 
"Kumshambulia hayati Magufuli kunaweza ligawa taifa..."?

Yeye alikuwa akiliunganisha taifa, au unayo maana nyingine ya kugawa taifa?

Alifanya kazi kubwa sana kuwagawa waTanzania kiasi cha kwamba kazi hiyo ndiyo itakayomwondolea hizi sifa ndogondogo za ujenzi wa vitu mnaoutanguliza mbele kama uzalendo wake.
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.
kwa sababu walijitokeza wengi barabarani?.
Watanzania tunapenda matukio na wapo wengi waliokwenda kushuhudia tukio la kihistoria la rais kufa madarakani
 
Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli imeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.

Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.

Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za maghariba..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?

Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.

Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza magawanyiko mkubwa huko mbeleni.

Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania. Nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibu kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.

Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.

Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?

Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.

Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
Maisha Ndo haya haya sa tuende wapi
 
Nashangaa unatusemea watu wa Kagera...mbona sisi hayo hatuyajui?
Wewe wa Chato Kagera inakuhusu nini? Tuache tunajua madhara ya tetemeko na matusi tuliyokumbana nayo toka kwa mtu tulitegemea atatufariji kama kiongozi.
 
Back
Top Bottom