Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

CAG huyu kaja na ukaguzi wa miaka mitano yote, Je Hilo la Tr1.5 umeliskia Kwenye hii ripoti??
Kwani hizo EPA na ESCROW umezisikia kwenye hii CAG report 20/21? Usitake kupoteza hoja kwa vihoja.....!!!!
 
Uwanja wa Ndege wa chato, kama unajina la Magufuli, au mmiliki wake ni Magufuli huo ndi ufisadi haswaa

Yeye kajenga Kwa ajili ya nchi, hawautaki, waanzishe machimbo ya zege, maana zege lililolala hapo si mchezo
Kuna mikoa ambayo haina viwanja vya kiwango kile,, kuna wilaya nyingi kongwe (acha kijiji cha chato) hazina uwanja hata wa nyasi, , halafu leo unaenda kujenga uwanja wa ndege kijijini kwako kwa kulazimishia tu eti iwe kawaida?
Huo ni ufisadi.
Ufisadi maana yake uchafu(tafsiri ya kwenye Bible)

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wasingejaa iko Lugha ambayo ungeitumia kusema kuhusu msiba huo!! Maana wabongo bhana Ni shida!

Wasingejaa tungewapa kubwa yao, na hata kama wamejaa bado hatuachi kuweka ukweli wa dhalimu hadharani. Ndio maana unaona vilio vingi.
 
Mimi naendelea kufurahia Magufuli kuitwa Fisadi, maana yake Magufuli akiitwa fisadi, basi serikari inayomfuata ifanye mambo meengi na makubwa kuliko aliyofanya Magufuli Kwa miaka yake mitano

Usambazaji umeme na bei chipa ya kuunganishia watu, ziwe Chini zaidi yake na umeme usambazwe Kwa Kasi kuliko yeye

Hospital na vituo Vya Afya, madawa na mikopo pamoja na kulipa Ada za shule msingi Hadi sekondari uongezwe kuliko yeye

Miradi kama SGR, bwawa la umeme, madaraja ya juu mfugale yawe karibu Kila jiji nchini, ndiyo, si alikuwa fisadi?? Mfanye makubwa kuliko yeye

Madege mlete angalau 50, viwanja Vya Ndege msivikarabati Tu, jengeni hata 20 hivi, stend za mabasi zienee Hadi tarafani huko

Maji vijijini, kero hii iishe na muende mbali zaidi Kwa kusambaza mabomba huko, Miradi ya maji kutoka Victoria fanyeni haraka Sana ufike Dodoma

Kwa kufanya makubwa zaidi kumshinda fisadi Magufuli kutathibitisha mkisemacho hapa, la sivyo utakuwa ni ujinga na upumbavu
 
Ukiingia kule Twitter wamejazana kwa Msemaji wao Kigogo wanadanganyana tu. Instagram kule huwaambii kitu kuhusu JPM,Hamis Kigwangalah kauona moto wake. Pale kwa Millard Ayo chochote kinachomuhusu JPM kikipostiwa ndiyo utajua watu walikuwa wanampenda kiasi gani.
Halafu Watanzania walio wengi hawapo huko Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa!

Kila nikikumbuka msafara wa jeneza la marehemu kuongozwa na bodaboda....au ile boat parade ziwa Victoria....machozi yananilenga!
 
Kuna mikoa ambayo haina viwanja vya kiwango kile,, kuna wilaya nyingi kongwe (acha kijiji cha chato) hazina uwanja hata wa nyasi, , halafu leo unaenda kujenga uwanja wa ndege kijijini kwako kwa kulazimishia tu eti iwe kawaida?
Huo ni ufisadi.
Ufisadi maana yake uchafu(tafsiri ya kwenye Bible)

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Chato ya Magufuli haina tofauti na Gbadolite ya Dikteta Mobutu Seseseko Kuku wa Nzabanga pale Zairwa....kenge mumaji.!!!
 
Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli imeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.

Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.

Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za maghariba..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?

Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.

Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza magawanyiko mkubwa huko mbeleni.

Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania. Nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibu kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.

Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.

Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?

Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.

Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
kumbe unaelewa hataa biblia iliandika mema na mabaya nasi tutasema mema na mbaya lengo letu ni kujifunza siyo mnatak a asifiwe tutasema siyo kuopa eti kura ujngaa gani
 
Kuna mikoa ambayo haina viwanja vya kiwango kile,, kuna wilaya nyingi kongwe (acha kijiji cha chato) hazina uwanja hata wa nyasi, , halafu leo unaenda kujenga uwanja wa ndege kijijini kwako kwa kulazimishia tu eti iwe kawaida?
Huo ni ufisadi.
Ufisadi maana yake uchafu(tafsiri ya kwenye Bible)

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Wasio mafisadi ndio mfanye haya maendeleo Kwa Kasi kubwa ili kudhihilisha ufisadi wa JPM, jengeni viwanja Vya Ndege kila Kona ili hoja yenu ya kumwita fisadi iwe Sawa!! La hamuwezi, basi mwacheni apumzike
 
Nani apoteze muda kumshambulia maiti??

Watu wanafunguka na wataendelea kufunguka uovo wake wote aliofanya ili mjifunze kuwa wastaarabu mnapopata madaraka. Pambaf.
 
Hivi ile hela aliyokuwa akibeba mailioni kwenye Sandarusi halafu anagawa kama njugu mawe zilikuwa zinakuwa accounted kivp?? No cheque no any official transaction no nothing....!!! Halafu utasikia jiwe anasema....UKINUNUA DAI RISTI NA UKIUZA TOA RISTI......Lakini yeye akichukua au kutoa pesa ilikuwa hakuna cha receipt wala kumbukumbu yoyote....!! Je, ni fedha kiasi gani ya walipa kodi maskini imepotea kwa mtindo huo?
Wanaomtetea ni waovu kama yeye, uovu wa wazi kabisa unaonekana halafu mtu eti anamtetea.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Halafu Watanzania walio wengi hawapo huko Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa!

Kila nikikumbuka msafara wa jeneza la marehemu kuongozwa na bodaboda....au ile boat parade ziwa Victoria....machozi yananilenga!
Hivi huwajui Watz a.k.a Wabongo??? Ule ulikuwa ni unafiki wa hali ya juu sana kuwahi kushuhudiwa hapa duniani!!!
Kama unataka kuthibitisha hili we sikiliza hotuba za Mami Sameer, report ya CAG na michango ya Wabunge pale mjengoni!!!
Kila kitu kiko MUBASHARA...!!!
 
CCM kanda ya ziwa ni Magufuli. Kama hayupo jibu mnalo
Alipo gombea kikwete mbona alipata wabunge?
Alipogombea Mkapa mbona alipata wabunge?

Wacheni mambo yenu ya kipuuzi huko kupinga utawala uliopo kisa ukanda.

Safari hii ndiyo ishatoka hiyo subirini hadi 2025.
 
Chato ya Magufuli haina tofauti na Gbadolite ya Dikteta Mobutu Seseseko Kuku wa Nzabanga pale Zairwa....kenge mumaji.!!!
Sjajua huyu Magufuli alikuwa akitoa wapi Hizi pesa, maana zamani tuliaminishwa kwamba, pesa ni Hadi tupige magoti Kwa wazungu, ndio tufanye maendeleo,

Kwa kuwa yeye kafanya Kwa fujo na kujenga Jenga Miradi miingi Tu na Bado ameiba, basi nyinyi ambao kawachia mtaanzisha Miradi mikubwa na itajemgwa Ka Kasi kulikoni yeye,

Mkomesheni Kwa kujenga kila pahala viwanja Vya Ndege ili ijulikane Kweli alikuwa mpigaji
 
Kitendo cha kumsema vibaya marehemu si kizuri hata kidogo,, lakini kuna cha kujiuliza ni kwanini iwe kwa magufuli? Mbona kwa Mkapa haikuwa hivi? Au kwa kuwa amefariki akiwa madarakani? So kuna kitu cha kujifunza huenda kuna watu wameumizwa sana na utawala wake ingawa sioni kama ni busara na haki kumshambulia mtu ambaye hana uwezo tena wa kujitetea.
 
Back
Top Bottom