Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KUMSIFIA RAIS SAMIA KILA USIMAMAPO MBELE YAKE SIO KOSA; HAIKUANZA LEO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kumtukuza Rais, kumsifu na kumlambalamba miguu, kumpangusa pangusa na kitambaa, kumfagilia, kumpepea, na kumpamba ni mambo ambayo yalikuwepo tangu zamani. Wala hatajaanza Kwa hawa Ndugu zetu wanaohangaika kwenye majukwaa ya siasa ili tuu Rais afurahi nao wapatemo Kula.
Najua hiyo tabia haiwezi kuwafurahisha Watu wote hasa wasiohusika na mambo ya Utawala. Ila kwenye Siasa ni Jambo la kawaida kumsifia Mtawala Mkuu.
Kumsifia mfalme au Rais inamaana gani kisiasa na kiutawala?
1. Kumuunga mkono na kumsapoti Kwa kazi anazozifanya. Kiashiria kuwa upo upande wake.
2. Kumfariji na kumpa Moyo. Kumsifia Mfalme au Rais ni kujaribu kumzuia asikate tamaa. Kuongoza na kutawala ni Jambo kubwa. Zipo changamoto nyingi Mno. Hivyo Sifa ni sehemu ya kumtia moyo WA kusonga Mbele.
3. Ishara ya kumheshimu na kuheshimu anachokifanya. Sifa na utukufu ni ishara ya kumheshimu MTU na kile akifanyacho. Kiutawala Sifa hutolewa kama sehemu ya kuonyesha heshima Kwa Mtawala au kiongozi wako. Mtawala Mkuu ambaye ni Mungu naye hupewa Sifa na utukufu Kwa namna mbalimbali.
Ingawaje kila atakachokifanya Mtawala Kwa Watu wake ni wajibu na sehemu ya majukumu yake lakini haiondoi ukweli kuwa Wakisifiwa hufurahi.
Kusimama Mbele ya Watawala na kupewa nafasi ya kuongea inahitaji Umakini, Werevu na Hekima.
Hata hivyo sio kila Sifa ambazo Watu huzitoa Mbele ya Watawala huchukuliwa Serious. Taikon nimezigawa Sifa katika makundi yafuatayo;
1. Sifa kama Shukrani na kuonyesha heshima, kutia moyo na kuhamasisha
2. Sifa kama kujipendekeza na kutaka upendeleo fulani
3. Sifa kama kijembe na kejeli
4. Sifa kama hofu au woga
5. Sifa kama kioja au kichekesho.
Watawala unapowasifia watakuweka katika moja ya makundi hayo. Mimi nikimsifia Rais ni tofauti na MTU mwingine atakavyomsifia Rais. Ni Kutokana na vile mazingira, Hali ya mtu, na jinsi Rais anavyomchukulia MTU. Sio kila mtu anayemsifia Mtawala basi Mtawala atafurahi.
Huwezi ishi au fanya kazi na Rais alafu usimsifie au kumtukuza. Jambo Hilo haliwezekaniki. Na hii ni Kwa sababu, wewe ni sehemu ya Mtawala. Unaweza kuwa upande wa Mtawala direct au indirect. Kitendo cha kupewa nafasi ya kuzungumza Mbele ya Rais au Mtawala mpaka hapo unapaswa kutoa shukrani kwani hiyo uliyopewa na heshima hivyo lazima urudishe heshima.
Tukirejea kwenye Rejea za vitabu Kwa wapenda Rejea, nitatumia kitabu cha Biblia ambacho kinarejea za kiuongozi na kiutawala.
Nabii Daniel Vs Mfalme Nebukadreza.
Daniel ni Nabii, ninaposema Nabii nazungumzia Namba moja wa Kiroho hapa Duniani. Watawala na wafalme wanajua Ninachokisema,
Ikiwa Nabii Daniel alikuwa anamsifia na kumtukuza Mfalme Nebukadreza Kwa maneno ya heshima na taadhima, unafikiri alikuwa na nidhamu ya woga? Hahaha! Daniel hakuwahi kuwa na Nidhamu ya woga bali alikuwa anatoa heshima inayolingana na Mhusika(Mfalme).
Pia Mhusika Nabii Yusufu na Farao.
Ingawaje Wahusika hao hawakuwa ni taifa moja na hao wafalme, wala hawakuwa dini moja na hao wafalme lakini wakuwapa Sifa pale kulikohitajika Sifa. Na pia waliwakosoa pale kuliko hitajika kukosolewa.
Kumsifu Mtawala sio kosa Ila kumsifusifu Hilo linaweza kuwa Kosa. Sio kosa kisheria Bali kosa katika Kanuni ya Msawazo au Kanuni ya kiasi
Halikadhalika kukosoa Mtawala sio kosa. Lakini kukosoakosoa kila mara linaweza kuwa Kosa katika Kanuni ya Msawazo au Kanuni ya kiasi.
Kila Jambo lifanyike Kwa kiasi.
Kumsifu kila mara Rais hata yeye mwenyewe hawezi kufurahia, halikadhalika kumkosoa kila mara hawezi kufurahia.
Hallelujah!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam