Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Julius Kambarage Nyerere nilimuona mara nyingi akihutubia pale ikulu Dar miaka ile ya 1980 mwanzoni. Alijaliwa ushawishi katika hoja zake. Siku moja alihutubia kwa muda mrefu kidogo halafu ndege ikawa inakatiza juu angani, akasema Mungu ameileta ile ndege ili mimi nimalize kuhutubia!, wote tukaangua vicheko.
Akijiamini sana katika uwezo wake wa kujenga hoja na wa kumsikiliza mtoa hoja na kuja na majibu yenye mantiki ya kina.
Mwalimu Nyerere aliipenda mno Tanzania na alijaliwa pia uwezo wa maono aliouchanga na kazi ya kuongoza nchi nchanga kama yetu. Yapo maneno ya mwisho aliyosema pale uwanja wa ndege mwaka 1999 akiwa njiani kwenda London kutibiwa saratani na huko mauti yakamkuta, alisema kuwa hata akifa ataendelea kuiombea nchi hii!.
Mwalimu Nyerere alisema Uhuru wetu hautakuwa na maana kama majirani zetu wa kusini wanaendelea kuteseka. Haikuwa ajabu tukawa mstari wa mbele katika kupigania haki za kisiasa na kiuchumi za mataifa mengi ya kusini mwa afrika. Nazikumbuka ofisi za FRELIMO zilizokuwa pale mtaa wa Ohio zinatazamana na ubalozi wa Misri na pembeni kuna ubalozi wa Msumbiji.
Miaka ile mahali pale palikuwa na watu wanaingia na kutoka muda mwingi wa siku za kazi, na nje kulikuwa na ulinzi wa askari wa FFU. Palikuwa ndio ofisi zenye kutambulisha mapambano ya kidugu ya kuikomboa sehemu kubwa ya kusini mwa afrika.
Wapo wabunge wenye kuongea maneno ya kejeli wanapouongelea mchango wa Tanzania wa ukombozi wa kusini mwa afrika, wanasema ni hulka yake binafsi ya kupenda sifa iliyotupeleka huko na kujikuta tukitumia pesa nyingi ambazo zingeweza kutumika katika kuleta maendeleo ya Tanzania.
Kwamba Nyerere alipenda zaidi sifa za kimataifa na akaona ni kawaida tu kupeleka maaskari huko kusini mwa afrika, ni maneno yanayotoka vinywani mwa wabunge wanaowakilisha nchi hii haswa wanapokosa majibu ya maswali mengi wanayoulizwa na wapiga kura wao huko majimboni.
Hii Njaa iliyoipiga Malawi na kusababisha matatizo na umaskini wa ghafla kwa kiasi kikubwa msaada umetoka kwetu Tanzania. Na hawa Wamalawi ni Wanyasa ambao baadhi yao walifikia hatua ya kuwa sehemu ya serikali ya awamu ya kwanza.
Hii mipaka iliyowekwa na wakoloni ipo kwa maslahi yao kwanza na sio maslahi ya afrika. Waliichora wakiwa na malengo yao ya kufaidika na utajiri wa chini ya ardhi kuliko kuangalia itaathiri vipi ustawi wa jamii zinazotenganishwa na mipaka yenyewe.
Mwenda yupo Tanzania, yupo Malawi na yupo Zambia. Tambwe yupo Tabora na yupo DRC. Niyonzima yupo Ngara na yupo Rwanda. Hivyo kuamua kuwasaidia kijeshi yale mataifa ya kusini mwa afrika hakuna tofauti yoyote ile na kuamua kupeleka maelfu ya magunia ya mahindi kwa watu wale wale.
Nyerere aliiona afrika hii ya leo ikiwa katika vita nzito ya kujitambulisha kama sehemu tajiri na yenye kitu cha maana cha kuchangia, miaka ile akiwa pale Magogoni Ikulu. Kuliko wanasiasa wa kisasa wanavyoiona afrika na kushindwa kutambua maana ya uwepo wa ndugu halisi wanaotenganishwa na mipaka iliyowekwa kimaslahi tena miaka 139 iliyopita kule Ujerumani.
Endelea kulala mahali pema peponi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, maono yako yataendelea kuishi daima kwa wale wenye kupenda kufikiria kwa kina.