Kumuelewa vyema Hayati Mwalimu Julius Nyerere upeo uwe mkubwa

Kumuelewa vyema Hayati Mwalimu Julius Nyerere upeo uwe mkubwa

Hii nukuu nimeikuta huko twitter na imenitafakarisha sana.

"Utii ukizidi unakuwa Uwoga, Uwoga huzaa Unafiki na Kujipendekeza, mwishowe ni mauti," Mwalimu Julius Nyerere.

Mlale unono!
 
Kwakuwa tupo mamilioni ya watu na hatuwezi kuwa na mawazo na mitazamo inayolingana na kwakuwa kila mtu ana haki ya kutoa mawazo na maoni kwa kadri anavyoona inafaa binafsi naheshimu maoni yako lakini kwangu ni tofauti kabisa.
Namuona ni aina ya kiongozi aliyeshindwa kutimiza hata malengo yake mwenyewe acha matumaini makubwa waliyokuwa wananchi baada ya kufanikiwa kumuondoa mkoloni.
Matumaini ya kuwa na uhuru,matumaini ya kuwa maendeleo ya kiuchumi,kielimu n.k lakini yote yalipotea na nchi ilirudi nyuma na haikuwahi kusonga mbele tena.
Matokeo yake malengo ya viongozi wetu sasa yamebadilika si tena kupiga vita umaskini, ujinga na maradhi bali sasa malengo ni kushika dola kwa njia yoyote huku baadhi yao wakiyatamka hayo waziwazi bila kificho.
 
Back
Top Bottom