Pengine kabla ya kulaumu mwingine, mmoja mmoja, tumefanikiwa vipi kutoka alipoachia yeye?Inshort Nyerere alikuwa anafanyia majaribio hizo siasa zake na uchumi labda zingefaulu tunge mponfeza lakini ndio zishafeli
Muda gani umepita tangu aache madaraka na pia tangu alipokufa?
Muda huo ungetosha kwa waliofuata kufanya tofauti?
Kuna vichwa maji wanajisifu kuwa, bwawa liliachwa likiwa limejengwa kwa 37% wao wamefikia 84% kwa miaka 2 tu! Swali ni je, ujenzi ulianza kuhesabiwa hatua gani? Site clearance? Mobilisation of resources? Au Ujenzi ulipoanza, ule wa kusimamisha tofali?
Ukishasafisha kiwanja, ukaweka vipimo sawa, ukachimba msingi na kupata picha, unaweka msingi, hatua inayochukua musa mrefu kuliko sehemu nyingine yoyote ya ujenzi; baada ya hapo, kupandisha ni kama kumsukuma mlevi.
Nyerere aliishia kwenye MSINGI, tumeshindwa kufanya finishing, kuna awamu ndo ikaja, ikatia ufa kwenye msingi wenyewe, sasa imebaki padogo tu LIUFA lenyewe liangushe banda walilopandisha kiholela.