Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Mkuu ile sadaka yako ya fomu kwa CCM mpaka leo hii ina kuuma! Ila naamini unge pata nafasi usinge andika haya hapa.lakini sasa chama alichokiasisi Mwalimu zile takrima zimegeuzwa ni michango ya lazima ya kuombea fomu ya uongozi, sasa fomu ya kugombea ubunge CCM inauzwa kwa Shilingi milioni 1!, kuna wakulima wangapi na wafanyakazi wanayo hiyo milioni moja ya kujaza fomu ya Ubunge?. Mwalimu Angekuwepo haya yangefanyika?.
Falsafa za Nyerere zitakufa kwa mafisadi na walamba asali tu siyo kwa watu wanaoamini katika kujenga misingi ya utu, uadilifu, umoja, kujitegemea, maendeleo ya wananchi kiujumla, uwajibikaji........huwezi kutegemea ajira za vijana kutoka kwenye uongozi unaoamini katika kulamba asali na kula kwa urefu wa kamba, na hapo ndo falsafa za Nyerere zinapotamalaki.Paskali bana, miaka hii kweli bado unasisitiza watu waishi kwa falsafa za Nyerere?! Kizazi kilichoamini falsafa za Nyerere kilishapita na waliobaki wako ukingoni. Zungumzia ajira ili watu wajikwamue na sio hizo falsafa za karne iliyopita.
Zidumu fikra za mwenyekitu. Huna kitu wewe ni zezeta tu kwa akili hizi ambazo CCM wanatufundisha.Wanabodi,
Kwa maslahi ya Taifa Jumapili hiiView attachment 2390581
View attachment 2390582
Karibu tena, kwenye makala nyingine ya “Kwa Maslahi kwa Taifa”, leo hii ni makala mwendelezo iliyoanzia wiki iliyopita, Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?. ikizungumzia kumuenzi muasisi wa taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kufuatia kumbukizi ya Baba wa Taifa kila Tarehe 14 October ni Nyerere Day, nikitafakari jinsi sisi Watanzania, Viongozi wetu na Chama chake CCM, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na kuuliza tumuenzi vipi Baba wa Taifa?. Jee tuendelee lumuenzi kwa mawazo mazuri tuu na kwa maneno tuu, kwa kupiga blah blah, "Mwalimu alikuwa hivi, Mwalimu alikuwa vile", au sasa tumuenzi kwa matendo kwa kuendelea kutenda kama Mwalimu, na ikiwezekana viongozi wetu wamuenzi Mwalimu kwa kumuishi!, na sio kwa hizi blah blah zinazoendelea sasa?.
Ukiondoa baadhi ya wazee wetu kama kina Ibrahim Kaduma na David Wakati waliotangulia mbele ya haki ambao walimuishi Mwalimu, na wachache waliobakia kama Mzee Joseph Warioba na Mzee Butiku, ni kiongozi gani mwingine yeyote aliye madarakani sasa ana muishi Mwalimu Nyerere?. John Pombe Magufuli angalau angalau Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!
Mimi ni mtu wa mastori story, hii simulizi ya Mwalimu, niliianza wiki iliyopita na niliishia nikiwa hostel za Chuo cha Uandishi wa Habari, TSJ enzi hizo kiko Ilala Shariff Shamba, nikapata ugeni wa kutembelewa na mtoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere, kunijulisha ninahitajika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere!, wale wa mastori mastori tuendelee, wale wa short and clear, unaweza ku jump into conclusion.
Kazi za Uandishi Kumcover Mwalimu
Mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kusafiri na Mwalimu safari ya Uswisi kwenye mkutano wa South South Commission uliofanyika jiji la Bern nchini Uswisi. Hivyo mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kufanya mahojiano na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere niliyoyafanyia jengo la The Bundes House, mjini Bern
Baada ya kurejea kutoka Uswisi, ndipo akaanza kuugua.
Mwalimu alipozidiwa na kupelekwa kutibiwa hospital ya St. Thomas, jijini London nchini Uingereza, ni mimi tena ndie mwandishi pekee wa Tanzania, aliyemtembelea St Thomas Hospital, nikiwa ndie mwandishi pekee wa Tanzania kutoka private media, aliyeandamana na Rais Mkapa ziarani Marekani kwenye Unga, wakati wa kurejea nchini tukapitia London kumuona Mwalimu na kurejea nyumbani ambapo mwanzoni mwa Octoba na haikupita wiki, Mwalimu akafariki.
Niliandaa a video documentary ya msiba wa Baba wa Taifa, tangu kuwasili kwa mwili, kuagwa uwanja wa taifa, nikamsindikiza mpaka Butiama kwenye makao yake ya milele.
Swali la kumhusu Mwalimu, je viongozi wetu wanamuenzi kwa kumuishi, au wana muenzi kwa mawazo tuu na maneno lakini sio kwa vitendo? Naombeni mnitajie hata kiongozi wetu mmoja tuu anayemuishi Nyerere kwa mawazo, maneno na matendo?
Jee chama alichokiasisi na kukiacha Mwalimu Nyerere, Chama cha Mapinduzi, CCM, kinamuenzi Mwalimu kwa vitendo?, kinamuishi kwa kufuata falsafa yake?, Jee hii CCM ya sasa ndie ile CCM aliyoiacha Mwalimu?.
CCM ya Mwalimu ilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi, sifa ya kugombea uongozi ilikuwa ni uwezo wa uongozi na uzalendo wako kwanza kwa nchi yako, kisha kwa chama chako, Jee sasa sifa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi CCM bado ni zile zile au sasa ili kuchaguliwa kiongozi sifa kuu ni una mkono mrefu kiasi gani kuwapatia takrima wajumbe?.
Mwalimu aliichukia rushwa kwa dhati, baada ya kufariki, tukaibariki rushwa kwa kuipa jina zuri la “takrima” tukapitisha na sheria kuiruhusu!. Kelele zikapigwa, sheria ile ikafutwa, lakini sasa chama alichokiasisi Mwalimu zile takrima zimegeuzwa ni michango ya lazima ya kuombea fomu ya uongozi, sasa fomu ya kugombea ubunge CCM inauzwa kwa Shilingi milioni 1!, kuna wakulima wangapi na wafanyakazi wanayo hiyo milioni moja ya kujaza fomu ya Ubunge?. Mwalimu Angekuwepo haya yangefanyika?.
Hitimisho
CCM, serikali yetu, viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla, tumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sio tuu kwa mawazo, na maneno, bali kwa matendo na ikibidi kumuishi, tutabarikiwa, na Taifa litabarikiwa!, tukiendelea kumuenzi hivi kwa mawazo tuu na maneno, lakini matendo ni tofauti, taifa letu na chama chetu na viongozi wetu, tutaendelea kupata kichapo cha bakora za kitu kinachoitwa karma.
Wasalaam.
Paskali
Falsafa za Nyerere zitakufa kwa mafisadi na walamba asali tu siyo kwa watu wanaoamini katika kujenga misingi ya utu, uadilifu, umoja, kujitegemea, maendeleo ya wananchi kiujumla, uwajibikaji........huwezi kutegemea ajira za vijana kutoka kwenye uongozi unaoamini katika kulamba asali na kula kwa urefu wa kamba, na hapo ndo falsafa za Nyerere zinapotamalaki.
Kwa hiyo falsafa inayoenda na wakati ni kulamba asali na kula kwa urefu wa kamba, basi umeeleweka mkuu....Ni kweli, lakini falsafa za karne iliyopita kwenye kizazi hiki boss? Au mmeishiwa na hoja ndio mnakuja na hizi story za zama damu?
Wanabodi
CCM, serikali yetu, viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla, tumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sio tuu kwa mawazo, na maneno, bali kwa matendo na ikibidi kumuishi, tutabarikiwa, na Taifa litabarikiwa!, tukiendelea kumuenzi hivi kwa mawazo tuu na maneno, lakini matendo ni tofauti, taifa letu na chama chetu na viongozi wetu, tutaendelea kupata kichapo cha bakora za kitu kinachoitwa karma.
Wasalaam.
Paskali
Yeye Mwalimu alikubali kukosolewa?
Hii ilikuwa makala utangulizi, makala mwendelezo ni hii Tumuenzi Vipi Baba wa Taifa?, Kwa Mawazo na Maneno tu, Au Kwa Matendo? Wito Kwa Viongozi Wetu, Muenzini Mwalimu kwa Kumuishi na Sio kwa Blah Blah! nimeisha muomba mode aziunganishe.View attachment 2386662View attachment 2386672
Karibuni tena kwenye makala zangu za “Kwa Maslahi kwa Taifa”, zinazozungumzia mada mbalimbali kuhusu taifa letu ziwe ni za kisiasa, za kiuchumi au za Kijamii, baada ya leo ni kuhusu kumuenzi Mwalimu Nyerere, kwa vile Tarehe 14 October ni Nyerere Day, leo naomba tutafakari jinsi sisi Watanzania, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, jee tunamuenzi kweli, kwa mawazo maneno na matendo?,
Mwalimu Nyerere sio tuu alikuwa ni muasisi wa CCM, mpaka kifo chake aliiamini CCM, hivyo hata baada ya nchi Tanzania, kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992, bado Mwalimu aliamini kuwa Wapinzani wanaweza kuleta wabunge bora, na hili tumelishuhudia kwa baadhi ya wabunge wa upinzani,walikuwa ni wabunge bora kabisa, lakini kwenye uraisi wa JMT, Mwalimu Nyerere aliamini “Rais bora atatoka CCM pekee”. Jee kuna Wana CCM wanao maishi Baba wa Taifa kwa mawazo, maneno na matendo?, ama watu tunamuenzi Mwalimu kwa mawazo na maneno tuu, lakini matendo na kumuishi....!.
Mimi ni mtu wa mastory mastory, yaani ni story teller, hivyo kama wewe sio mtu wa mastory story, katishia hapa, nenda mwisho, wale wa mastory mastory, tuendelee...
Jinsi Nilivyo Mfahamu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Baada ya sekondari nikajiunga na chuo cha Uandishi habari TSJ, ndipo Jumapili moja asubuhi, nikaja kuamshwa na mlinzi wa hostel, kuna nina mgeni!, si unajua tena mambo ya ujana, na hostel, ukisikia tuu una ugeni basi unajua ni ugeni wa type gani, ila asubuhi, tena Jumapili, asubuhi ni hatari!, kunaweza kutokea ajali!.
Kufika nikakuta jamaa fulani mweupe ana bonge la afro na gari sports car nyekundu na kujitambulisha Mimi ni Madaraka Nyerere, mtoto wa Nyerere, anahitajika Msasani kwa Nyerere!.
Naomba niishie hapa, tukutane wiki ijayo mjue niliitiwa nini Msasani kwa Nyerere?, Jee nilikwenda?, Nilimuona Mwalimu Nyerere?.
Nawatakia Nyerere Day Njema.
Paskali.
Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa matendo na kumuishi na sio kwa maneno tuu!.leo ni kuhusu kumuenzi Mwalimu Nyerere, kwa vile Tarehe 14 October ni Nyerere Day, leo naomba tutafakari jinsi sisi Watanzania, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, jee tunamuenzi kweli, kwa mawazo maneno na matendo?,
Mwalimu Nyerere sio tuu alikuwa ni muasisi wa CCM, mpaka kifo chake aliiamini CCM, hivyo hata baada ya nchi Tanzania, kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992, bado Mwalimu aliamini kuwa Wapinzani wanaweza kuleta wabunge bora, na hili tumelishuhudia kwa baadhi ya wabunge wa upinzani,walikuwa ni wabunge bora kabisa, lakini kwenye uraisi wa JMT, Mwalimu Nyerere aliamini “Rais bora atatoka CCM pekee”. Jee kuna Wana CCM wanao muishi Baba wa Taifa kwa mawazo, maneno na matendo?, ama watu tunamuenzi Mwalimu kwa mawazo na maneno tuu, lakini matendo na kumuishi....!.
Nawatakia Nyerere Day Njema.
Paskali.