Wanabodi,
Kwa maslahi ya Taifa Jumapili hii
View attachment 2390581
View attachment 2390582
Karibu tena, kwenye makala nyingine ya “Kwa Maslahi kwa Taifa”, leo hii ni makala mwendelezo iliyoanzia wiki iliyopita,
Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?. ikizungumzia kumuenzi muasisi wa taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kufuatia kumbukizi ya Baba wa Taifa kila Tarehe 14 October ni Nyerere Day, nikitafakari jinsi sisi Watanzania, Viongozi wetu na Chama chake CCM, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na kuuliza tumuenzi vipi Baba wa Taifa?. Jee tuendelee lumuenzi kwa mawazo mazuri tuu na kwa maneno tuu, kwa kupiga blah blah, "Mwalimu alikuwa hivi, Mwalimu alikuwa vile", au sasa tumuenzi kwa matendo kwa kuendelea kutenda kama Mwalimu, na ikiwezekana viongozi wetu wamuenzi Mwalimu kwa kumuishi!, na sio kwa hizi blah blah zinazoendelea sasa?.
Ukiondoa baadhi ya wazee wetu kama kina Ibrahim Kaduma na David Wakati waliotangulia mbele ya haki ambao walimuishi Mwalimu, na wachache waliobakia kama Mzee Joseph Warioba na Mzee Butiku, ni kiongozi gani mwingine yeyote aliye madarakani sasa ana muishi Mwalimu Nyerere?. John Pombe Magufuli angalau angalau
Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!
Mimi ni mtu wa mastori story, hii simulizi ya Mwalimu, niliianza wiki iliyopita na niliishia nikiwa hostel za Chuo cha Uandishi wa Habari, TSJ enzi hizo kiko Ilala Shariff Shamba, nikapata ugeni wa kutembelewa na mtoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere, kunijulisha ninahitajika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere!, wale wa mastori mastori tuendelee, wale wa short and clear, unaweza ku jump into conclusion.
Kazi za Uandishi Kumcover Mwalimu
Mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kusafiri na Mwalimu safari ya Uswisi kwenye mkutano wa South South Commission uliofanyika jiji la Bern nchini Uswisi. Hivyo mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kufanya mahojiano na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere niliyoyafanyia jengo la The Bundes House, mjini Bern
Baada ya kurejea kutoka Uswisi, ndipo akaanza kuugua.
Mwalimu alipozidiwa na kupelekwa kutibiwa hospital ya St. Thomas, jijini London nchini Uingereza, ni mimi tena ndie mwandishi pekee wa Tanzania, aliyemtembelea St Thomas Hospital, nikiwa ndie mwandishi pekee wa Tanzania kutoka private media, aliyeandamana na Rais Mkapa ziarani Marekani kwenye Unga, wakati wa kurejea nchini tukapitia London kumuona Mwalimu na kurejea nyumbani ambapo mwanzoni mwa Octoba na haikupita wiki, Mwalimu akafariki.
Niliandaa a video documentary ya msiba wa Baba wa Taifa, tangu kuwasili kwa mwili, kuagwa uwanja wa taifa, nikamsindikiza mpaka Butiama kwenye makao yake ya milele.
Swali la kumhusu Mwalimu, je viongozi wetu wanamuenzi kwa kumuishi, au wana muenzi kwa mawazo tuu na maneno lakini sio kwa vitendo? Naombeni mnitajie hata kiongozi wetu mmoja tuu anayemuishi Nyerere kwa mawazo, maneno na matendo?
Jee chama alichokiasisi na kukiacha Mwalimu Nyerere, Chama cha Mapinduzi, CCM, kinamuenzi Mwalimu kwa vitendo?, kinamuishi kwa kufuata falsafa yake?, Jee hii CCM ya sasa ndie ile CCM aliyoiacha Mwalimu?.
CCM ya Mwalimu ilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi, sifa ya kugombea uongozi ilikuwa ni uwezo wa uongozi na uzalendo wako kwanza kwa nchi yako, kisha kwa chama chako, Jee sasa sifa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi CCM bado ni zile zile au sasa ili kuchaguliwa kiongozi sifa kuu ni una mkono mrefu kiasi gani kuwapatia takrima wajumbe?.
Mwalimu aliichukia rushwa kwa dhati, baada ya kufariki, tukaibariki rushwa kwa kuipa jina zuri la “takrima” tukapitisha na sheria kuiruhusu!. Kelele zikapigwa, sheria ile ikafutwa, lakini sasa chama alichokiasisi Mwalimu zile takrima zimegeuzwa ni michango ya lazima ya kuombea fomu ya uongozi, sasa fomu ya kugombea ubunge CCM inauzwa kwa Shilingi milioni 1!, kuna wakulima wangapi na wafanyakazi wanayo hiyo milioni moja ya kujaza fomu ya Ubunge?. Mwalimu Angekuwepo haya yangefanyika?.
Hitimisho
CCM, serikali yetu, viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla, tumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sio tuu kwa mawazo, na maneno, bali kwa matendo na ikibidi kumuishi, tutabarikiwa, na Taifa litabarikiwa!, tukiendelea kumuenzi hivi kwa mawazo tuu na maneno, lakini matendo ni tofauti, taifa letu na chama chetu na viongozi wetu, tutaendelea kupata kichapo cha bakora za kitu kinachoitwa karma.
Wasalaam.
Paskali