Kumuenzi Hayati Magufuli, mkoa wa Chato uitwe Magufuli

Kumuenzi Hayati Magufuli, mkoa wa Chato uitwe Magufuli

Naunga mkono hoja na makao makuu ya huo mkoa utakaoitwa magufuli yawe ni hapo chato.
 
Kuna mkoa kama Morogoro ni mkubwa sana, sidhani kama Geita kuna haja hiyo currently
 
Sijui kuna watu wanawazaga kwa Njia ya Haja Kubwa? Mtoa mada na MATAGA mnatia kinyaa
 
Kwanza hamna mkoa wa Chato Wilaya ya Chato Mkoa Geita mafii ya Ngedhere kkabisaa!!
 
Huyo mungu wenu kashaenda kubalini matokeo tu
 
Njia bora ya kumuenzi mtu sio kuweka monuments. Njia sahihi ni kutimiza ni kuuvaa ujasiri wake, kutenda kwa ushujaa na kutimiza maono yake.

Maono ya Magufuli ilikuwa kuifanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi advanced. Hilo lengo halihitaji watu wapuuzipuuzi wanaojiangalia wao tu, na wanaoangalia leo tu.

Tanzania imejaa watu wa namna hiyo, ndio maana utawasikia wanamwomba mama Samia eti aachane na mamiradi makubwamakubwa maana yanazoa hela nyingi mtaani, afterall maisha yenyewe ni mafupi, kwa nini tujitese! Watu wenye mioyo ya namna hiyo hawana nafasi kwenye Tanzania ya maono ya Magufuli.

Marekani wangekuwa hivyo wangepeleka vyombo Mars?
 
Tusianze kuuita mikoa majina ya wanasiasa maana kila siku tutaishia kubadilisha majina. Tubakize utamaduni uleule wa majina. Kama mtu kafanya mazuri yataonekana. Tusifanye vitu kwa hisia za misiba bila kufikiria vizuri
Ukila nyama ya mtu hutataka kuacha, wameanza uharibifu huo Dar kwa kuharibu maeneo tofauti na maarufu kwa kuyapa majina yao sasa wanataka kuhamisha kwenye mikoa, wataenda wilayani, wataenda tarafani, wataenda katani, vijijini na mwisho watamalizia na jina la nchi. Ubinafsi ni ugonjwa mbaya sana. TAZARA Bridge, Unungo Interchange, NSSF/Kigamboni Bridge.
 
Kazi iliyotukuka aliyoifanya Hayati Dokta John Joseph Pombe Magufuli tangia akiwa waziri hadi alipokuwa Rais wa awamu ya tano ni kubwa mno na inaonekana...
Ni upuuzi mtupu Magu alifanya mabaya mengi tu na yataanza kuanikwa hivi punde.
 
Baada ya mwez naomba muweka picha hapa kuonyesha CIA ilivyo bussy 24hrs kama amsterdam airpot na ndege kama KLM pamoja na Qutar airlines zikifanya landing na ku flight
 
Kazi iliyotukuka aliyoifanya Hayati Dokta John Joseph Pombe Magufuli tangia akiwa waziri hadi alipokuwa Rais wa awamu ya tano ni kubwa mno na inaonekana
Ingawa amelala mauti, jina lake, maono yake, miradi aliyoisimamia akiwa madarakani na Jitihada zake katika kulinda , kusimamia na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa maendeleo ya nchi vitabaki kumbulumbu ya kudumu kwa vizazi hadi vizazi
Katika shughuli ya Mazishi, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amejibu ombi la sana chato la kuifanya chato kuwa mkoa.
Kwa mtazamo wangu, huo mchakato na vigezo vya kuifanya chato kuwa mkoa vikikamilika, Napendekeza Jina la huo mkoa kuwa ni Magufuli.
Mheshimiwa Rais Samia ameahidi kumuenzi Hayati Dokta Magufuli kwa kuifanya chato kuwa mkoa, mkoa huo ukiitwa Magufuli, kumuenzi kutaimarika zaidi. Pia katika mkoa huo, pawepo jumba la makumbusho ya Jemedari Magufuli.
Upuuzi huh utawaisha lini? Yani kila kitu anataka kipewe jina lake? Ndo itasidia kumfufua?????
 
Back
Top Bottom