Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2


Hata wafuasi wa kibwetere walikuwa wabishi hivi hivi?. Ila waliujua ukweli mwishoni wakiwa maiti.
 
Kabla ya kumpinga Nabii acha hisia na maneno ya watu acha mazoea na kukariri..
Manabii wa kweli wapo na wa uongo wapo.

Jukumu ni lako kuomba mwalimu Roho Mtakatifu akujulishe na atakujulisha kuwa Nabii ni wa kweli ama sio wa kweli...

Tatizo letu hatusomi maandiko. Nabii gani kwenye Biblia alikuwa ana chunga kanisa?. Nabii kazi yake ni kuwaambia watu Siri za Mungu na mambo makubwa yajayo.

Sasa Nabii wa siku hizi, kwanza anakuuliza tunafahamiana?. Tumewahi kuongea sehemu?. Halafu anaanza kusema naona alama ya free mason kwako. Yani full utapeli na mikogo. Nabii ni mdomo wa Mungu kwenda kwa wafalme , raia, watumishi etc ili kulijenga taifa la Mungu na Ufalme wa Mungu. Tujifunze kutoka kwa Nabii Yonah.
 
Hivyo vifaa vya kiroho kama huombi kwa jina la YESU havitakusaidia...

Haviwezi kuwa hirizi maana unaomba kwa jina la YESU..

Jina la Yesu Kristo alihitaji usaidizi. Kwani utumie jina la Yesu kwenye hirizi?. Hivyo dhambi mbaya sana.
 
Nimepitia comments lakin sioni mantiki ya mtu ambae hawezi kutoa hela kumuona kuhani au mtumishi yoyote kumsema vibaya yule ambae yeye binafsi anaweza. halafu hiyo laki2 unayoongelea ndogo sana, usicheze kabisa na imani ya mtu.

Imani kwenye laki mbili?. Yesu aliponya watu Bure, matapeli wa siku hizi hata hawaponyi ila wanataka pesa kwanza.
 
Freely "ye have" uhuni ulianza kitambo
 
Imani kwenye laki mbili?. Yesu aliponya watu Bure, matapeli wa siku hizi hata hawaponyi ila wanataka pesa kwanza.
Hamna madhabahu isiyotaka sadaka mkuu, hata ya kiganga nayo inademand sadaka, ni uamuzi tu. Ila pia kwa siku za sikuhizi kuendesha kanisa nalo gharama, kuna mdau niliona ameongelea kanisa hilo lina ujenzi, kanisa halikosi wafanyakazi wanaolipwa, gharama kama za umeme etc. Pia nawaza mfano kama ibada inahudhuriwa na maelfu ya waumini, mlango wa ofisi ukiwa wazi tu itakuwa fujo, mwenye shida nzito na imani ataeka hiyo 200k ubaoni asikilizwe fasta..
 

Wewe ni mpinga Kristo?. Kristo mwenyewe kasema mmepewa Bure toeni Bure, halafu wewe inapinga hilo. Tatizo Hawa manabii wa kitapeli wameharibu akili mpaka mnalikataa Neno.
 

Unaelewa maana ya sadaka?. Biblia ipo wazi sadaka ni Siri, hata mkono mwingine usijue. Sasa unapoweka kiwango Cha pesa kwaajili ya maombi , hivyo sio sadaka ni mchango au tozo.
 
Huko kwenye biblia nabii gani alikua kaanzisha kanisa nakuliendesha kw michango
 
Ajabu, mbona anapingana na wachawi na waganga?

Tena anafichua Siri za wachawi na waganga, na anawataja...

Wengine ni Watoto wadogo...
Umenikumbusha mke wangu aliingia kanisa la nabii mmoja nikiwa masomoni, narudi nakuta mambo yamebadilika. Nikampa yellow kadi ya kwanza, nikaongeza ya pili na nikamwambia jiandae kupanda basi. Akanyooka sasa karudi kanisa lake la Catholic na akili zimemrudi.
 
Acha mazuzu wapigwe tu
Hamna namna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…