Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Mkuu, Imani yangu ni level za juu, siongei kwa hisia Nina nguvu za Rohoni...

Naweza kuona kuwa huyu ni Nabii feki au sio...

Hata wewe tukikutana na wewe nakujua mpaka ukoo wako...

Huna mamlaka ya kumuita mtu Wakala wa Ibilisi wakati hujapima Roho kwa njia ya Roho Mtakatifu

Hata wafuasi wa kibwetere walikuwa wabishi hivi hivi?. Ila waliujua ukweli mwishoni wakiwa maiti.
 
Kabla ya kumpinga Nabii acha hisia na maneno ya watu acha mazoea na kukariri..
Manabii wa kweli wapo na wa uongo wapo.

Jukumu ni lako kuomba mwalimu Roho Mtakatifu akujulishe na atakujulisha kuwa Nabii ni wa kweli ama sio wa kweli...

Tatizo letu hatusomi maandiko. Nabii gani kwenye Biblia alikuwa ana chunga kanisa?. Nabii kazi yake ni kuwaambia watu Siri za Mungu na mambo makubwa yajayo.

Sasa Nabii wa siku hizi, kwanza anakuuliza tunafahamiana?. Tumewahi kuongea sehemu?. Halafu anaanza kusema naona alama ya free mason kwako. Yani full utapeli na mikogo. Nabii ni mdomo wa Mungu kwenda kwa wafalme , raia, watumishi etc ili kulijenga taifa la Mungu na Ufalme wa Mungu. Tujifunze kutoka kwa Nabii Yonah.
 
Nimepitia comments lakin sioni mantiki ya mtu ambae hawezi kutoa hela kumuona kuhani au mtumishi yoyote kumsema vibaya yule ambae yeye binafsi anaweza. halafu hiyo laki2 unayoongelea ndogo sana, usicheze kabisa na imani ya mtu.

Imani kwenye laki mbili?. Yesu aliponya watu Bure, matapeli wa siku hizi hata hawaponyi ila wanataka pesa kwanza.
 
MUNGU si kigeugeu.
Hawezi kupingana na neno lake.
Kama kuna mtu anawatoza pesa kwa njia yoyote ile ili awape vifaa vya kiroho huyo ni wakala wa Ibilisi haijalishi watu wanapona au la.
My father ni mganga nguli mpaka vichaa wanapona kwahiyo uponyaji sio kigezo kusema fulani ana MUNGU.
Muda mwingine muache kuenenda kwa hisia .
View attachment 2815751
Freely "ye have" uhuni ulianza kitambo
 
Imani kwenye laki mbili?. Yesu aliponya watu Bure, matapeli wa siku hizi hata hawaponyi ila wanataka pesa kwanza.
Hamna madhabahu isiyotaka sadaka mkuu, hata ya kiganga nayo inademand sadaka, ni uamuzi tu. Ila pia kwa siku za sikuhizi kuendesha kanisa nalo gharama, kuna mdau niliona ameongelea kanisa hilo lina ujenzi, kanisa halikosi wafanyakazi wanaolipwa, gharama kama za umeme etc. Pia nawaza mfano kama ibada inahudhuriwa na maelfu ya waumini, mlango wa ofisi ukiwa wazi tu itakuwa fujo, mwenye shida nzito na imani ataeka hiyo 200k ubaoni asikilizwe fasta..
 
Na nyie wafanya hayo bure mjitathimini kama mnacho .mlichopewa

Watu wanakuja kwenu watoa bure hawapati ufumbuzi

Kelele tu ohhh tumepewa bure tunatoa bure kiko wapi hicho mnatoa bure mtu anakuja kwenu haponi ,shida zake hazitoki miaka

Akina Petro walisema kwa yule kiwete kuwa tutazame sisi tuna kitu wakijiamini wana kitu wakasema tulichonacho tunakupa bure kwa Jina la Yesu inuka na kiwete akainuka Sababu akina Petro walijua wana kitu na waweza toa bure bila shida na mtu changamoto yake ikaisha kufumba na kufumbua

Mnacho hicho cha kutoa mtu akija kwenu na mashida kibao kama petro alitamka ? au na nyie matapeli tu hamna hata cha kutoa mnatafuta waumini tu? Matapeli nyie

Na nyie kama hamna kitu cha kutoa kama Petro aliyetamka tulichonacho tunakupa na nyie ni matapeli tu wanaotumia injili kutapeli watu hamna tofauti yeyote

Wewe ni mpinga Kristo?. Kristo mwenyewe kasema mmepewa Bure toeni Bure, halafu wewe inapinga hilo. Tatizo Hawa manabii wa kitapeli wameharibu akili mpaka mnalikataa Neno.
 
Hamna madhabahu isiyotaka sadaka mkuu, hata ya kiganga nayo inademand sadaka, ni uamuzi tu. Ila pia kwa siku za sikuhizi kuendesha kanisa nalo gharama, kuna mdau niliona ameongelea kanisa hilo lina ujenzi, kanisa halikosi wafanyakazi wanaolipwa, gharama kama za umeme etc. Pia nawaza mfano kama ibada inahudhuriwa na maelfu ya waumini, mlango wa ofisi ukiwa wazi tu itakuwa fujo, mwenye shida nzito na imani ataeka hiyo 200k ubaoni asikilizwe fasta..

Unaelewa maana ya sadaka?. Biblia ipo wazi sadaka ni Siri, hata mkono mwingine usijue. Sasa unapoweka kiwango Cha pesa kwaajili ya maombi , hivyo sio sadaka ni mchango au tozo.
 
Hamna madhabahu isiyotaka sadaka mkuu, hata ya kiganga nayo inademand sadaka, ni uamuzi tu. Ila pia kwa siku za sikuhizi kuendesha kanisa nalo gharama, kuna mdau niliona ameongelea kanisa hilo lina ujenzi, kanisa halikosi wafanyakazi wanaolipwa, gharama kama za umeme etc. Pia nawaza mfano kama ibada inahudhuriwa na maelfu ya waumini, mlango wa ofisi ukiwa wazi tu itakuwa fujo, mwenye shida nzito na imani ataeka hiyo 200k ubaoni asikilizwe fasta..
Huko kwenye biblia nabii gani alikua kaanzisha kanisa nakuliendesha kw michango
 
Ajabu, mbona anapingana na wachawi na waganga?

Tena anafichua Siri za wachawi na waganga, na anawataja...

Wengine ni Watoto wadogo...
Umenikumbusha mke wangu aliingia kanisa la nabii mmoja nikiwa masomoni, narudi nakuta mambo yamebadilika. Nikampa yellow kadi ya kwanza, nikaongeza ya pili na nikamwambia jiandae kupanda basi. Akanyooka sasa karudi kanisa lake la Catholic na akili zimemrudi.
 
Ukifika pale Temboni unataka kumuona Kuhani Mussa Richard, kuna dau kama ilivyo kwa manabii wengine ila jamaa kaongeza kitu kinaitwa FAST TRACK. Hiyo ukitoa haina foleni, ile unamaliza kuhesabu pesa tu huyu hapa anakufanyia maombi.

Ila msisahau kubeba pesa za kununulia vifaa vya kiroho ambayo pia vina grade zake. Kuna vya matokeo ya papo hapo, na vile vya gradually Yaani mdogo mdogo.
Acha mazuzu wapigwe tu
Hamna namna
 
Back
Top Bottom