Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Najua hizo lakin2 ni sadaka , kwaajili ya ujenzi wa kanisa ambalo linajengwa..

Mi nimesali kwa Kuhani Musa ila sijawahi ingia ofisini kwake...

Nilikuwa naenda ibadani Tena kwa ku beep ila nimekua kiroho sababu ya mahubiri yake juu ya Yesu Kristo...
Advanced witch doctor under the umbrella [emoji2513] of Jesus Christ.
 
Ukifika pale Temboni unataka kumuona Kuhani Mussa Richard, kuna dau kama ilivyo kwa manabii wengine ila jamaa kaongeza kitu kinaitwa FAST TRACK. Hiyo ukitoa haina foleni, ile unamaliza kuhesabu pesa tu huyu hapa anakufanyia maombi.

Ila msisahau kubeba pesa za kununulia vifaa vya kiroho ambayo pia vina grade zake. Kuna vya matokeo ya papo hapo, na vile vya gradually Yaani mdogo mdogo.
Diamond pia matamasha yake VIP meza ni karibu milioni moja, Daimond anawakilisha ufalme wa shetani na Mussa anawakilisha ufalme wa Mungu.

#kupanga ni kuchagua.
 
Ndo hivyo wajinga ndio waliwao..na siku ya jumapili ukipita pale nje temboni kuna watu kibao wako na bahasha wanagawa huruhusiwi uende kanisan kwake bila kuwa na bahasha uweke hela yaani pale bahasha kwanza ndio kiapumbele.
Sasa kinachonisikitisha sijawahi ona gwajiama au mwamposa au huyo mwasha labda akishiriki ibada ya kuzika labda kafa muumini wake haijawahi tokea.
Iliniuma sana niliposhuhudia ndugu yangu wa damu kabisa aliyekuwa mmoja wa waumini wa Gwajiboy tena mwenye kacheo fulani hapo kanisani alipofariki mwaka 2015 kwaya tu ya kanisani kuja kutoa huduma ya uimbaji msibani walidai malipo. Bila malipo waligoma kuja ikabidi malipo yafanyike ndipo wakaja.
 
Hakuna pesa yoyote ukitaka kumuona Kuhani Musa
Usitapeliwe Sandali Ali wala usidanganyike
Hakuna fast track wala pesa ya vifaa vya kiroho maana kila ibada vinagawiwa buree labda utake vya ziada
Chawa wa kuhani akiwa kazini natamani nikufahamu kwa sura na ipo siku ntakufahamu tu. Hujielewi wewe.
 
Mwizi kivip na hajamlazimisha mtu aende?
Nisikilize, unapofanya kinyume na katiba ni kosa.

Na katika imani ukifanya kinyume na muongozo wa kitabu cha imani yako ni wizi.

Ni wapi imeandikwa mtu apeleke pesa aombewe?
 
Sasa una mdharau mtu kisa imani yake? Kila mtu kuna kitu ana kiamini kwa aina yake!
Halafu jf bhna ukiingia kichwa kichwa unaweza fikiri hawasali,hawaendi kwa manabii ,hawaendi kwa mitume,hawatoi michango ya harusi na hawapendi mambo ya dini hahahah!

Humu akili za kuambiwa changanya na zako…kuna chumvi nyingi zinazidishwa kwenye matukio….! Ukisoma coments za humu unaweza jiuliza hawa waumini manabii huwa wanawapata wapi? Na hawa waganga huwa wanapata wateja wapi? Kumbe ni hawa hawa wanaopinga sana ndio waumini wao!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sio kwel toka na miaka 9 huo ujinga niliachana nao ata sjui wanasali vp tena.
 
Mkuu, Imani yangu ni level za juu, siongei kwa hisia Nina nguvu za Rohoni...

Naweza kuona kuwa huyu ni Nabii feki au sio...

Hata wewe tukikutana na wewe nakujua mpaka ukoo wako...

Huna mamlaka ya kumuita mtu Wakala wa Ibilisi wakati hujapima Roho kwa njia ya Roho Mtakatifu
Una nguvu gani wewe,mnadanganyana kwwnye vijikanisa uvhwara
 
Diamond pia matamasha yake VIP meza ni karibu milioni moja, Daimond anawakilisha ufalme wa shetani na Mussa anawakilisha ufalme wa Mungu.

#kupanga ni kuchagua.
Kuhani Mussa anawakilisha ufalme wa MUNGU yupi?
Yule Mungu wa mbingu na nchi aliyewaonya watumishi wake wasitoze fedha au mungu wa duniani shetani?
Screenshot_20231116-194104.jpg


Hebu tulia kwa makini tafakari andiko hili
 
Huna mamlaka ya kumuita mtu Wakala wa Ibilisi wakati hujapima Roho kwa njia ya Roho Mtakatifu

Ila mbona kapima roho hapo? Kuijaribu roho ni kupima kama mtu husika mwenye dhamana anafundisha kwa mujibu wa neno la Mungu au la. Hapo utaweza kujua roho inayofanya naye kazi.
 
Najua hizo lakin2 ni sadaka , kwaajili ya ujenzi wa kanisa ambalo linajengwa..

Mi nimesali kwa Kuhani Musa ila sijawahi ingia ofisini kwake...

Nilikuwa naenda ibadani Tena kwa ku beep ila nimekua kiroho sababu ya mahubiri yake juu ya Yesu Kristo...

Hakuna sadaka ya kutajiwa kiwango. Yani lakini mbili iwe sadaka.
 
Back
Top Bottom