Nimekuwa nikiangalia namna ambavyo wizara ya utalii na mali asili wamekuwa wakim-treat raisi wetu kwenye mambo yao ya Royal tour nikajiuliza maswali mengi sana.
Hivi kwenye hii movie, raisi Samia amepewa hadhi ipi? Je, ni mhusika wa kawaida tu ama mhusika ambaye pia ni raisi?
Maswali yangu haya ni kutokana na namna ambavyo Rais wetu amekuwa akivalishwa.
Mara nyingi amekuwa akivalishwa nguo ama vitu vinavyomdhalilisha utu wake ama kuudhalilisha uraisi.
Kule mafia walimvalishia life jacket under size ambayo ilimfanya mama sehemu yake ya mbele kifuani kuwa wazi kabisa. Pia nguo walizomvalisha za maafisa wa wanyapori hazina staha kabisa.
Uwiano wa eneo la juu na la chini la mama haliko sawa kwa sababu ya mavazi haya. Kiukweli hayapendezi na hayana heshima kabisa.
Sasa haya yote yanatokea huku watumishi wa Ikulu pamoja na TISS wenye dhamana ya kuulinda utu wa raisi wakiwepo.
Je, haya yanatokea kwa bahati mbaya au ndivyo yalivyopangwa yatokee?
TISS mjirerekwbiahe, mheshimuni raisi na kumlinda, ifanyeni kazi yenu mlioaminiwa kuifanya ya kumtunza raisi kwa umakini.