Kumvisha Rais Life Jacket inayobana kiasi hiki sio sawa

Kumvisha Rais Life Jacket inayobana kiasi hiki sio sawa

Nyie wanenguaji huwa mnanengua hata mtu akipiga chafya. Ni lazima kila utawala na ninyi kuwepo?

Mnakosa akili na ubunifu mnaongezea Tozo na Kodi kwa maskini muwe mnazunguka zunguka tu nchi mbalimbali...
Sasa umeandika nini,kwambamba,tunaongeza tozo , kwani sie tumekua MWIGULU, Ya muwe madarakani na mvulunde,then lawama wapatiwe wenye nchi, au umelewa
 
Yupo field. Ukifika field unakabiliana na mazingira uliyoyakuta huko.
 
Watu wa karibu na Raisi inabidi wanunue life jacket za kisasa za Personal Floating Devices (PFD) ambazo ni rahisi kuvaa, zinamuweka mvaaji kuwa comfortable muda wote na zina chukua eneo dogo la mwili.

images (16).jpeg


images (18).jpeg



Sasa kutokana na teknolojia hizo ni life jacket za kawaida, siku za karibuni zinatumika Sana PFD. Watu wa Melini, boti za utalii, watu mashuhuri na viongozi hutumia personal floating device hii inafaa kwa watu wenye miili midogo, ya Kati na mikubwa.

Kwa mheshimiwa Raisi pale wangempatia Ultra Slim Belt inflatable life jacket ambayo anavaa kiunoni kama zile beji za kina mama za kuwekea pesa.

images (17).jpeg
images (20).jpeg
 
Bulletproof life jacket iko ndani hiyo ya nje ni formality tu 😁😁😁😁
Watanzania tanapenda kuangaliana huyu kavaaje yule kavaa nini... Sometime tunakuwa waji...nga bila kujijua.
 
Nchi hii imekuwa na mambo mengi sana hvi karibuni.
 
Huwa najiuliza, ukiwa Rais, kuna sheria inayokataza kutumia akili zako? Au akili zinawekwa shelf za pale Hazina? Maana utasikia anashauriwa vibaya! Wanamzunguka! Wamemfanyia vile, yeye hana tafakari yake!?!! Sasa hapa wanalaumiwa waliomvalisha, yeye Rais wakati anavaa haoni kuwa hii nguo inabana?
 
Nimekuwa nikiangalia namna ambavyo wizara ya utalii na mali asili wamekuwa wakim-treat raisi wetu kwenye mambo yao ya Royal tour nikajiuliza maswali mengi sana.

Hivi kwenye hii movie, raisi Samia amepewa hadhi ipi? Je, ni mhusika wa kawaida tu ama mhusika ambaye pia ni raisi?
Maswali yangu haya ni kutokana na namna ambavyo Rais wetu amekuwa akivalishwa.

Mara nyingi amekuwa akivalishwa nguo ama vitu vinavyomdhalilisha utu wake ama kuudhalilisha uraisi.

Kule mafia walimvalishia life jacket under size ambayo ilimfanya mama sehemu yake ya mbele kifuani kuwa wazi kabisa. Pia nguo walizomvalisha za maafisa wa wanyapori hazina staha kabisa.

Uwiano wa eneo la juu na la chini la mama haliko sawa kwa sababu ya mavazi haya. Kiukweli hayapendezi na hayana heshima kabisa.

Sasa haya yote yanatokea huku watumishi wa Ikulu pamoja na TISS wenye dhamana ya kuulinda utu wa raisi wakiwepo.

Je, haya yanatokea kwa bahati mbaya au ndivyo yalivyopangwa yatokee?

TISS mjirerekwbiahe, mheshimuni raisi na kumlinda, ifanyeni kazi yenu mlioaminiwa kuifanya ya kumtunza raisi kwa umakini.
 
Acha ujuaji wa kishamba wewe!

Hili tatizo la kujitia unaelewa kila kitu linaboa sana!
Nguo alizovishwa Rais zinakusudi maalum, haikuwa lengo kuwa ni vazi la mtoko!

Lile ni vazi maalum kama zilivyo combart!
Hata kama unapenda style ya mavazi huwezi shona kimini cha combat!

Ujuaji ujuaji mwingi haufai
 
Back
Top Bottom