Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Bila hivo atajenga kwao kwa zile tu miamia anazochikchia akienda gengeni afu aanze kuleta zarau kwa mwanaume....lazima nae ajikamue, tena inatakiwa ata wiki nzima unamkomalia afanye maarifa
 
Maarifa ni kwenda kuchukua vile vinchenchi chenchi vinavyobakigi na kwenda kununua chakula familia isishinde/isilale njaa
 
maarifa ni mengi kwa mwanamke
hasa village girls
utaomba unga kwa jirani
utakuwa na bustani ya viazi
utakuwa na bustani ya mboga mboga
utakusanya kuni uuze

so many
Umejibu vyema sana Kiongozi.

Shukran
 
Inawezekana kukopa au kwa vile Wengi wanacheza michezo ya upatu basi wanaweza kufanya maarifa huko ukitilia maanani maarifa yenyewe ni dharura tu si kila siku
 
Pamoja kuwa mwanamke ndo bingwa wa kutumia hovyo lkn bado anashikilia record ya kuwa bingwa wa budget..anaweza kuchuma mchicha pori akanunua unga wa mia nne mkala....ila we umewaza kifuksa watakujibu wafuksa wenzako
 
Mwanamme anafikiri,anatafuta,anahenya,anateseka ili familia yake ipate kuishi (namzungumzia mtu wa aina hiyo)..Inafikia nyakati kila anachkifanya kinagonga mwamba,mambo si kama yalivyokuwa awali.....Kwa kiswahili cha kisiasa inabidi kufunga mkanda..tuingie kwenye dharula ya muda.

Mambo yasiyo ya kawaida katika familia kama kunywa chai,kununua nguo mpya,kutumia mafuta mengi kwenye mboga,viungo visivyo vya lazima kama pilipili hoho vyote vinasitishwa..Mwendo unakuwa ni wa kula ili kuishi.Na ni nani waziri wa jiko na mambo ya dharula ? - Ni mwanamke..ndipo mwanaume anatoa wito..fanya maarifa - yaani tumia kila kilichopo kwa akili.
Waziri wa jiko na mambo ya dharula😂😂
 
Wanawake walio wengi hususani wa mjini hapo unakuwa umempa fursa ya kumchuna buzi lake na maisha yanasonga🙌
 
Umeoa na mke wako ni mama wa nyumbani. Katikati ya mwezi unajikuta una nauli tu ya kuendea kazini. Asubuhi unamuaga unamwambia hali ngumu afanye maarifa.

Mke amekopa kwa mangi. Kwa mapenzi aliyonayo kwako unakuta wali kuku na Miranda ya baridi. Huulizi hela alipata wapi. Mbona mnatuacha kwenye hali mbaya?
 
Back
Top Bottom