Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Hivi mwanaume unashindwaje hata kumfungulia biashara ya genge mkeo aache kuwa mama wa nyumbani.akiwa busy huko hata kukusaliti inakuwa ngumu kidogo hawezi kuacha genge akaenda Lodge ila Sasa akiwa mama wa nyumbani umekaribisha michepuko tayari na umeipa uhuru.akiwa na biashara yake hamwezi kukosa hela ndogo ndogo za chakula.hiko ndicho nikiwazacho
 
Hiiiiiii sasa mbona kama unataka kuhalalisha kitu kwa nguvu hutumaanishi hivyo bhana mnapotuaga asubuhi na kutuambia nenda kapambane ww unajua ni kwa namna ganii please usifanye hivyo!!
 
Kauli za hivyo kuna muda zinaumiza,.mtu unafanyaje maarifa wakati huna hata tuta moja la mchicha nje?..ni muhimu mke na mume kushirikiana kusaidia uchumi wa nyumbani kuwa sawa,.

Kuna vitu vinaweza kuepukwa,mfano mke ni mama wa nyumbani na mume ndio mtafutaji,si vibaya mume kumpa mkewe mtaji hata wa kupika chapati asbh hapo nyumbani kuepuka kauli sononeshi kama hizo..hapo hata ukimwambia mama flan fanya maarifa atafanya..sio fanya maarifa huku maarifa yenyewe hayapo,.lol
 
Umeoa na mke wako ni mama wa nyumbani. Katikati ya mwezi unajikuta una nauli tu ya kuendea kazini. Asubuhi unamuaga unamwambia hali ngumu afanye maarifa.

Mke amekopa kwa mangi. Kwa mapenzi aliyonayo kwako unakuta wali kuku na Miranda ya baridi. Huulizi hela alipata wapi. Mbona mnatuacha kwenye hali mbaya?
Wanaume wenye tabia hii bado wapo duniani? hata siamini
 
Kauli za hivyo kuna muda zinaumiza,.mtu unafanyaje maarifa wakati huna hata tuta moja la mchicha nje?..ni muhimu mke na mume kushirikiana kusaidia uchumi wa nyumbani kuwa sawa,.

Kuna vitu vinaweza kuepukwa,mfano mke ni mama wa nyumbani na mume ndio mtafutaji,si vibaya mume kumpa mkewe mtaji hata wa kupika chapati asbh hapo nyumbani kuepuka kauli sononeshi kama hizo..hapo hata ukimwambia mama flan fanya maarifa atafanya..sio fanya maarifa huku maarifa yenyewe hayapo,.lol
Wanafungua mianya ya udanganyifu wenyewe. Unakopa kwa Mangi mwisho unabadilisha njia.
 
Jamaa kamwambia mke wake " wanawake wanatoka wanarudi na chochote mfukoni nawe toka uangalie wanafanya nini ! Hapo hata tone la unga hakuna
 
Nilibahatika kuishi sana na Wanigeria. Wao formula yao ya maisha ni kuwa nwanaume lazima uwe na biashara.

Kazi na biashara viende pamoja. Hata kama unalipwa laki na nusu hiyo ni guarantor ya kuchulia mkopo wa kuongezea biashara.

Mke ndiye ubavu wako, atasimamia biashara wakati wewe uko kwenye paid job.
 
Hivi Mwanaume ananzaje kumwambia Mkewe kuwa hali ni ngumu hivyo akafanye utaratibu hali yakuwa unajuwa hana Kazi yoyote ya kumuingizia Kipato?
Hao wanaopewa kila Kitu Visilani haviishi huyo anaetumwa Kukopa kwa Mangi sijui dhamana yake inakuwaje, na anakuchukuliaje ww Mwanaume???
 
Akili zilizojaa fikra zinifu huwa hazina tafsiri nje ya uzinifu, hakuna uhusiano wowote wa kuwa mama wa nyumbani na kugawa mechi. Ukiwa mgawaji utagawa tu.
 
Nilibahatika kuishi sana na Wanigeria. Wao formula yao ya maisha ni kuwa nwanaume lazima uwe na biashara.

Kazi na biashara viende pamoja. Hata kama unalipwa laki na nusu hiyo ni guarantor ya kuchulia mkopo wa kuongezea biashara.

Mke ndiye ubavu wako, atasimamia biashara wakati wewe uko kwenye paid job.
Na nyie muwe ngangari sasa kama wake wa kinigeria. Tunafungua biashara zinakufa.

Mnakosea wapi?
 
Na nyie muwe ngangari sasa kama wake wa kinigeria. Tunafungua biashara zinakufa.

Mnakosea wapi?
Kabisa mkuu mnakopa bank mna za kukaanga chips, mama unampeleka school of Catarina hata miezi mitatu kuongeza ubunifu.
 
Kuna dada yeye nilimuona anashona nguo mbele ya nyumba. Alianza hivyo wateja wa kupinda khanga na vitenge.

Alibuni njia mpya, asubuhi akawa anakwenda sokoni ana nunua tiki time maji, tango, ndizi machungwa na bado. Anamenya yote anaweza kwenye sahani anafunika na cling film. Sahani sh 2000.
 
Back
Top Bottom