Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Uzuri wangu mie nna kiherehere, sisubiri kuambiwa nifanye maarifa. Nasoma alama za nyakati tu na kuiwahi kuulinda mtima wa mwenzi wanga. Tena kwa kujikausha kabisa 'Baba, unadhani mie napenda nyama siku hizi. Wewe nenda, Mungu hatotuacha!'.
Asili ya mwanamke ni kuwa na akiba. Haiwezekani akakaa hata sh 100 hana, ikitokea emergency ya mafuta ya taa ashindwe hadi muzeiya arudi. Hakuna raha ya mapenzi kama kuwa na uhitaji, basi tu dunia imechafuka!

mimi kwa mangi na kwa wapemba naenda kukopa mwenyewe lol
maarifa yako kwa wamama wenzio tu lol
 
Yaani hapa I guess the Boss had his own premeditated ideas ya 'kufanya maarifa' lol
 
Kawaida akina mama ni mahodari wa kubargain...

Kama utaacha 5 thou... Kila siku,yeye kuna kiasi anasave daily ujue!

Na huwa wana michezo yao ya kupeana...

Kwa hiyo usishangae akifanikisha kufanya hayo maarifa..
 
Mkuu TB, umenirejesha nyuma kidogo enzi hizoo...!!!; wakati fulani mambo yalikuwa magumu kidogo, basi kuna siku nikakosa kabisa kitu cha kuacha home, nikasema leo 'fanya maarifa'. Niliporudi jioni nilikuta wali na kuku amejaa kwenye sufuria (Jogoo), nikamuuliza mwenzangu haya kulikoni akaniambia amepewa na jirani yetu bwana John (huyu jirani ni mshikaji ambae hana mke, mwangalizi wa nyumba ya jamaa fulani). Nilishikwa na hasira, nikachukua sufuria la wali na kuku nikaenda kutupa nje, halafu tukalala bila kula.

Asubuhi yake nikaenda kazini, yule John akanifuata kazini akiambatana na jirani mwingine; alikuja kuniomba msamaha kwa yaliyotokea na kunisihi kwamba kulikuwa hakuna baya lolote kati yake na mwenza wangu. Alinieleza kwamba siku ile mwenza wangu alikuja kumwomba kuchuma mboga ya majani (maana alikuwa na bustani ya mboga), yeye alimruhusu lakini wakati anaondoka aliamua kumpatia kuku kama zawadi kwenu japokuwa sikuwa na mahusiano ya karibu sana na wewe, lakini mwenza wako mara nyingi anakuja kuchuma mboga kwangu.

Nafikiri ili kuondoa utata wa mambo katika kufanya maarifa ni vyema kujadiliana kwa pamoja ni maarifa gani yatafanyika.
 
Wanawake wanakuwaga na VUBUBU! huwa wanatunza zile chenji ndogo ndogo kwa kudunduliza wakijua kuna kesho.....................
 
Mkuu TB, umenirejesha nyuma kidogo enzi hizoo...!!!; wakati fulani mambo yalikuwa magumu kidogo, basi kuna siku nikakosa kabisa kitu cha kuacha home, nikasema leo 'fanya maarifa'. Niliporudi jioni nilikuta wali na kuku amejaa kwenye sufuria (Jogoo), nikamuuliza mwenzangu haya kulikoni akaniambia amepewa na jirani yetu bwana John (huyu jirani ni mshikaji ambae hana mke, mwangalizi wa nyumba ya jamaa fulani). Nilishikwa na hasira, nikachukua sufuria la wali na kuku nikaenda kutupa nje, halafu tukalala bila kula.

Asubuhi yake nikaenda kazini, yule John akanifuata kazini akiambatana na jirani mwingine; alikuja kuniomba msamaha kwa yaliyotokea na kunisihi kwamba kulikuwa hakuna baya lolote kati yake na mwenza wangu. Alinieleza kwamba siku ile mwenza wangu alikuja kumwomba kuchuma mboga ya majani (maana alikuwa na bustani ya mboga), yeye alimruhusu lakini wakati anaondoka aliamua kumpatia kuku kama zawadi kwenu japokuwa sikuwa na mahusiano ya karibu sana na wewe, lakini mwenza wako mara nyingi anakuja kuchuma mboga kwangu.

Nafikiri ili kuondoa utata wa mambo katika kufanya maarifa ni vyema kujadiliana kwa pamoja ni maarifa gani yatafanyika.

Huwezi kuanza kufanya majadiliano maana wewe umeshindwa cha msingi kama unataka kula mwachie uhuru aamue mwenyewe afanye nini usimwingilie. Usitawaliwe na hisia mbaya kama ndio hivyo ulitakiwa kuchunguza na sio kumwaga chakula unamkatisha tamaa mkeo pale anapotaka kufanya maarifa wakati wewe umeshindwa
 
Maarifa="Mama saidi una vijidagaa untilie kwenye kibakuli"
 
Mi nadhani mwanamke akiwa ndani as a wife lazima atakua na vi-akiba vyake kidogo, na mara nyingi huwa hawatoi au kutumia hovyo coz hiyo ni akiba na huwa wanaitumia pale mipango ya siku ikigonga mwamba.

kwa hiyo kama siku mzee mzima akioshea/kufulia... then anamwambia mamaaa fanya maarifa kidogo ili mambo yaende sawa hapo ndio mke kwa busara anaweza kwenda kuchukua kiakiba chake coz anajua mzee leo hana kitu.

NB: hii ipo sana hasa kwa wana ndoa/aged ones....yaani kizazi kile cha enzi za mwalimu lakini hawa mabinti wa dot.com au hawa wa st.kayumba hili wao hawalijui, na ndio maana wanaume siku hizi wanapelekeshwa sana na hawa bangua kichwa...lol

Mwisho....kufanya maarifa haimaanishi kuwa aende nje ya ndoa yake kusaka pesa kwa buz kwa malipo ya kutoa uroda!

@boss umeelewa hapo??
 
wanawake wanakuwaga na vububu! Huwa wanatunza zile chenji ndogo ndogo kwa kudunduliza wakijua kuna kesho.....................

kiongozi hiyo ni apllicable kwa wanawake wa enzi za mwalimu but sio hawa wa st.kayumba type!! Hawa ni noma mkuu!
 
Huwezi kuanza kufanya majadiliano maana wewe umeshindwa cha msingi kama unataka kula mwachie uhuru aamue mwenyewe afanye nini usimwingilie. Usitawaliwe na hisia mbaya kama ndio hivyo ulitakiwa kuchunguza na sio kumwaga chakula unamkatisha tamaa mkeo pale anapotaka kufanya maarifa wakati wewe umeshindwa

Mkuu Nitonye; katika maisha si wakati wote huwa tunafanya maamuzi sahihi, kwahiyo huna sababu ya kumlaumu mtu katika maamuzi aliyochukua katika jambo fulani kwa wakati fulani. Katika maelezo yangu nimeeleza yule ndugu alikuja ki-ungwana na kuomba msamaha, nami niligundua sikufanya sahihi (ndiyo maana waswahili wanasema hasira - hasara, vilevile kumbuka tunajifunza kutokana na makosa). Yule jamaa alikuja kuwa rafiki yangu na maisha yaliendelea. Halafu huu unaozungumza ni mfumo DUME kwamba mwanamume ndiyo kila kitu, ni vyema kujenga utamaduni wa kujadiliana wakati wote na kufikia makubaliano ya pamoja iwe wakati mambo yako safi au mabaya.
 
ni kweli kabisa mpendwa

mpendwa,

maarifa mazuri hayo ila yapasa kuwa mwangalifu ili usilimbikize madeni hadi mkatamani kuhama hapo mtaani mnapoishi, si unajua lakini akina mangi wanavyodai pesa zao?

mpendwa,

kama mwanamke atachukulia hiyo kauli yako kama kibali cha kulala nje ya ndoa yake, basi jua kuwa huyo anayo hiyo tabia siku zote na ataendelea nayo hata siku ukijitosheleza kwa kila kitu na kufanya maarifa yote mwenyewe! hiyo ni tabia mpendwa, dhiki ya siku moja haiwezi kufikia hatua hiyo ya kutoka nje ya ndoa!

hapo kwenye nyekundu, mi nasema ni sahihi na halali kabisa kama culture yao hapo nyumbani inaruhusu! kila wanandoa wana ka-utamaduni kao ndani ya nyumba yao. maneno hayo yanatamkwa kila siku ndani ya nyumba zenye vipato vidogo japo kwa maneno tofauti na hayo...ila kama si utamaduni wenu kusema hivyo, unaweza kudaiwa talaka siku hiyo!! kwa hiyo wanandoa wawe makini hapo

mbarikiwe sana wapendwa,
Glory to God!
Miss Judith, hapo umemaliza kila kitu, hasa hilo la kusema "fanya maarifa" kwa lugha tafauti.
Ikiwa kumwambia mke fanya maarifa, na kama wanaume wengi wana hakika kuwa "kufanya maarifa "maana yake ni kumwambia mwanamke aende kugawa ugolo [Kongosho], basi wanaume wengi wasingekuwa wanatoa kauli hiyo, isipokuwa kama wapo, basi ni wale ambao hawaoni tabu na huwa ni faraja kwao kuwauza wake zao kwa maslahi yeo wenyewe.

Kwa mawazo yangu, hata ikifikia hadi ya mwanamume kakwama kweli, mke wake atakuwa wa kwanza kuielewa hiyo hali na hata haifikii mwanamume kumwambia afanye maarifa bali yeye mwenyewe, kwa faida ya watoto wao, atafanya maarifa yake kama aliyoyataja Kongosho #2,[URL="https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/222523-kumwambia-mwanamke-fanya-maarifa.html#post3307004"]#4, #10[/URL]ili jikoni kusilale paka.
Big up wamama wote [Nitonye#7]
 
maarifa gani ambayo mwanaume akishindwa ,mwanamke ndo ataweza?????????

halafu unakuta mwanamke 'anafanya kweli maarifa' na maisha yanakwenda...

The Boss , umeishusha sana jinsia hiyo , ebu futa kauli hiyo aisee !!!
 
Miss Judith, hapo umemaliza kila kitu, hasa hilo la kusema "fanya maarifa" kwa lugha tafauti.
Ikiwa kumwambia mke fanya maarifa, na kama wanaume wengi wana hakika kuwa "kufanya maarifa "maana yake ni kumwambia mwanamke aende kugawa ugolo [Kongosho], basi wanaume wengi wasingekuwa wanatoa kauli hiyo, isipokuwa kama wapo, basi ni wale ambao hawaoni tabu na huwa ni faraja kwao kuwauza wake zao kwa maslahi yeo wenyewe.

Kwa mawazo yangu, hata ikifikia hadi ya mwanamume kakwama kweli, mke wake atakuwa wa kwanza kuielewa hiyo hali na hata haifikii mwanamume kumwambia afanye maarifa bali yeye mwenyewe, kwa faida ya watoto wao, atafanya maarifa yake kama aliyoyataja Kongosho #2,#4, #10ili jikoni kusilale paka.
Big up wamama wote [Nitonye#7]

mpendwa Mammamia,

asante sana kwa mchango ulioongezea. ubarikiwe sana.

kwanza, nikufahamiushe wewe na wanaJF wote kuwa kuna mabadiliko madogo kwenye ID yangu, tafadhari itazameni vizuri. ni katika kuwekana sawa tu wapendwa.

pili, nakuunga mkono kwa dhati kabisa hapo kwenye blue. hiyo ndiyo mantiki hasa ya kusema "na hao wawili watakuwa mwili mmoja" hivi jamani katika mwili huohuo mmoja, mkono uugue na mguu usijue hadi ipigwe mbiu?? mi nadhani ukata unapoingia nyumbani, labda watoto na wageni ndio wa kusubiri "kuambiwa" ila si mke manake nyumba kama process endelevu hali zote huwa zinajulikana automatically. hayo ya kutegeana hadi usikie kauli kama za "fanya maarifa" zaweza kutokana na mawasiliano mabaya kati ya wanandoa lakini si kawaida ya maisha ya pamoja katika uhalisia wake!

tatizo jingine kwenye mjadala huu ni pale unapokuta watu wana majibu vichwani yasiyofutika juu ya nini hasa maana ya maneno "fanya maarifa" ndani ya ndoa. nadhani hiyo ndiyo changamoto kubwa tuliyonayo hapa katika hii thread.

ubarikiwe sana mpendwa,

Glory to God!
 
mpendwa Mammamia,
mabadiliko madogo kwenye ID yangu,
ubarikiwe sana mpendwa,
Glory to God!
Samahani sana Ms. Judith, ingawa moyoni ninalijua hilo, lakini kwa mazowea kwenye keyboard mikono ya ilipata kigugumizi.
Asante sana kwa kutukumbusha.
Mungu akulinde muda wote na ubarikiwe sana mpendwa.
 
Mkuu TB, umenirejesha nyuma kidogo enzi hizoo...!!!; wakati fulani mambo yalikuwa magumu kidogo, basi kuna siku nikakosa kabisa kitu cha kuacha home, nikasema leo 'fanya maarifa'. Niliporudi jioni nilikuta wali na kuku amejaa kwenye sufuria (Jogoo), nikamuuliza mwenzangu haya kulikoni akaniambia amepewa na jirani yetu bwana John (huyu jirani ni mshikaji ambae hana mke, mwangalizi wa nyumba ya jamaa fulani). Nilishikwa na hasira, nikachukua sufuria la wali na kuku nikaenda kutupa nje, halafu tukalala bila kula.

Asubuhi yake nikaenda kazini, yule John akanifuata kazini akiambatana na jirani mwingine; alikuja kuniomba msamaha kwa yaliyotokea na kunisihi kwamba kulikuwa hakuna baya lolote kati yake na mwenza wangu. Alinieleza kwamba siku ile mwenza wangu alikuja kumwomba kuchuma mboga ya majani (maana alikuwa na bustani ya mboga), yeye alimruhusu lakini wakati anaondoka aliamua kumpatia kuku kama zawadi kwenu japokuwa sikuwa na mahusiano ya karibu sana na wewe, lakini mwenza wako mara nyingi anakuja kuchuma mboga kwangu.

Nafikiri ili kuondoa utata wa mambo katika kufanya maarifa ni vyema kujadiliana kwa pamoja ni maarifa gani yatafanyika.

aisee hii ni kali...lol
 
Back
Top Bottom