Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inategemea kua hio shida ni of what nature.... Kuna ile kama inahusiana na chakula ndani, anaona tu aibu kusema nenda angalau kwa wazazi kaombe unga kidogo tumekwama... anaona bora akwambie kua "fanya maarifa"..... Kawaida ya mwanamke ambae ni mwerevu (walau that is what I think) ni kutambua kua sio kila siku mume wake ataweza provide - na kwamba hata kama anaweza inaweza tokea in rare cases akakwama. Daima kulinda heshima ndani ya ndoa yenu inatakiwa kua na akili ya ziada mkichwa na maarifa pia....
Hivo basi daima hata kama woote wanafanya kazi na woote wana provide, ni lazima aweke akiba pembeni popote pale ndani ya nyumba ambayo inakua ni kinga ya kutatua tatizo pale ambapo litajitokeza na woote wasiwe na pesa (yaani mume na yeye mwenyewe mke); Hio akiba sio wanaume woote hujua kua inakuwepo.... Inapotokea kua kuna siku mlikwama kabisa mara nyingi akina mama huchukua hio akiba kuokoa jahazi kwa kumshirikisha mumeo na kumwambia "mume wangu nimeazima kwenye kikundi chetu kile cha upaku" sababu ya kusema hivi sio kwamba humuamini mumeo.... No! Ila tu ni ile haitakiwi hajenge kichwani mwake kuna akiba ndani for next time akikwama he wont try harder..... Hivo baas mara nyingi wanaume husema hivo sababu wanakua weshawahi pita in jams na mke aliokoa jahazi.... Siamini kua hua wanasema hivo kwa maana kwamba nenda kwa mpango wa kando ukatafute pesa.
Boss it has been Long.... Usiku mwema.
Mwanamme anafikiri,anatafuta,anahenya,anateseka ili familia yake ipate kuishi (namzungumzia mtu wa aina hiyo)..Inafikia nyakati kila anachkifanya kinagonga mwamba,mambo si kama yalivyokuwa awali.....Kwa kiswahili cha kisiasa inabidi kufunga mkanda..tuingie kwenye dharula ya muda.
Mambo yasiyo ya kawaida katika familia kama kunywa chai,kununua nguo mpya,kutumia mafuta mengi kwenye mboga,viungo visivyo vya lazima kama pilipili hoho vyote vinasitishwa..Mwendo unakuwa ni wa kula ili kuishi.Na ni nani waziri wa jiko na mambo ya dharula ? - Ni mwanamke..ndipo mwanaume anatoa wito..fanya maarifa - yaani tumia kila kilichopo kwa akili.
kwa mjini
unaweza enda kopa kwa mangi
mme akipata pesa unaenda lipa
au unakopa kwa mama jirani
Inategemea kua hio shida ni of what nature.... Kuna ile kama inahusiana na chakula ndani, anaona tu aibu kusema nenda angalau kwa wazazi kaombe unga kidogo tumekwama... anaona bora akwambie kua "fanya maarifa"..... Kawaida ya mwanamke ambae ni mwerevu (walau that is what I think) ni kutambua kua sio kila siku mume wake ataweza provide - na kwamba hata kama anaweza inaweza tokea in rare cases akakwama. Daima kulinda heshima ndani ya ndoa yenu inatakiwa kua na akili ya ziada mkichwa na maarifa pia....
Hivo basi daima hata kama woote wanafanya kazi na woote wana provide, ni lazima aweke akiba pembeni popote pale ndani ya nyumba ambayo inakua ni kinga ya kutatua tatizo pale ambapo litajitokeza na woote wasiwe na pesa (yaani mume na yeye mwenyewe mke); Hio akiba sio wanaume woote hujua kua inakuwepo.... Inapotokea kua kuna siku mlikwama kabisa mara nyingi akina mama huchukua hio akiba kuokoa jahazi kwa kumshirikisha mumeo na kumwambia "mume wangu nimeazima kwenye kikundi chetu kile cha upaku" sababu ya kusema hivi sio kwamba humuamini mumeo.... No! Ila tu ni ile haitakiwi hajenge kichwani mwake kuna akiba ndani for next time akikwama he wont try harder..... Hivo baas mara nyingi wanaume husema hivo sababu wanakua weshawahi pita in jams na mke aliokoa jahazi.... Siamini kua hua wanasema hivo kwa maana kwamba nenda kwa mpango wa kando ukatafute pesa.
Boss it has been Long.... Usiku mwema.
Ila tukubaliane, huo wasiwasi wa TB kuhusu ku-take advantage hautakosekana kama mwanaume atahitaji kila mara mkewe 'afanye maarifa'. Ndo wakina marioo hao, yeye anauza sura kila siku hoping mkewe atamuweka mjini kwa maarifa. Ikila kwake usishangae, manake ile sense ya masculinity inapotea machoni kwa mkewe. Na mke anaanza kuona wale wawezeshaji ndo wako masculine (mangi included)
Kwa nini mume asiende kopa kwa Mangi yeye mwenyewe?
ladyfurahia naomba nikupe changamoto hapo. Siamini kuwq mwanaume anayeijali familia atasema "fanya maarifa " kila siku.Unavyomwambia mwanamke afanye maarifa wakati wewe yamekushinda
unamaanisha nini hapo? si atoke akatafute ili nae alete home?
sasa akileta unamuona ni mhuni wakati hata yeye ana kipato chake
ndo mana mm nasema nyie wanaume mnatufanya sie tuwe kwenye
mifumo yenu , mnatuweka katika nafasi ya mwisho sana wakati sie
ni walezi wakubwa wa familia kuliko nyie.
HATUTAKI KUKANDAMIZWA
ladyfurahia naomba nikupe changamoto hapo. Siamini kuwq mwanaume anayeijali familia atasema "fanya maarifa " kila siku.
Inatokea mara moja moja hana pesa, mtu hawezi kuwa, nacho kila siku. Na inawezekana katika yale matumizi anayotoa kila siku hutumii, yote, unajisevia kidogo. Angalau basi mambo yakiwa magumu, umpe tafu.
Hapa hatuongelei nani mlezi bora wa familia, bali mtoaji katika familia. Huyo mtoaji kuna, siku nae anakosa, hapo akisema fanya maarifq ndo wewe ujaribu au kuchukua savings zako, au kukopa nk..
Wanawake wanaolinda familia zao sidhani kama watapata shida kwa hilo, as long as it doesn't happen frequently!
maarifa ni mengi kwa mwanamke
hasa village girls
utaomba unga kwa jirani
utakuwa na bustani ya viazi
utakuwa na bustani ya mboga mboga
utakusanya kuni uuze
so many
Kuna baadhi ya familia ....mwanaume akishindwa baadhi ya majukumu yake hasa ya kipato ni kawaida kusikia mume akimwambia mkewe 'fanya maarifa' au ufanye maarifa basi'.......
Hivi hili hasa linaamaanisha nini?
Maarifa gani ambayo mwanaume akishindwa, mwanamke ndo ataweza?
Halafu unakuta mwanamke 'anafanya kweli maarifa' na maisha yanakwenda...
Sasa 'haya maarifa' ya wanawake ni yapi?