Mkuu TB, umenirejesha nyuma kidogo enzi hizoo...!!!; wakati fulani mambo yalikuwa magumu kidogo, basi kuna siku nikakosa kabisa kitu cha kuacha home, nikasema leo 'fanya maarifa'. Niliporudi jioni nilikuta wali na kuku amejaa kwenye sufuria (Jogoo), nikamuuliza mwenzangu haya kulikoni akaniambia amepewa na jirani yetu bwana John (huyu jirani ni mshikaji ambae hana mke, mwangalizi wa nyumba ya jamaa fulani). Nilishikwa na hasira, nikachukua sufuria la wali na kuku nikaenda kutupa nje, halafu tukalala bila kula.
Asubuhi yake nikaenda kazini, yule John akanifuata kazini akiambatana na jirani mwingine; alikuja kuniomba msamaha kwa yaliyotokea na kunisihi kwamba kulikuwa hakuna baya lolote kati yake na mwenza wangu. Alinieleza kwamba siku ile mwenza wangu alikuja kumwomba kuchuma mboga ya majani (maana alikuwa na bustani ya mboga), yeye alimruhusu lakini wakati anaondoka aliamua kumpatia kuku kama zawadi kwenu japokuwa sikuwa na mahusiano ya karibu sana na wewe, lakini mwenza wako mara nyingi anakuja kuchuma mboga kwangu.
Nafikiri ili kuondoa utata wa mambo katika kufanya maarifa ni vyema kujadiliana kwa pamoja ni maarifa gani yatafanyika.