Uzuri wangu mie nna kiherehere, sisubiri kuambiwa nifanye maarifa. Nasoma alama za nyakati tu na kuiwahi kuulinda mtima wa mwenzi wanga. Tena kwa kujikausha kabisa 'Baba, unadhani mie napenda nyama siku hizi. Wewe nenda, Mungu hatotuacha!'.
Asili ya mwanamke ni kuwa na akiba. Haiwezekani akakaa hata sh 100 hana, ikitokea emergency ya mafuta ya taa ashindwe hadi muzeiya arudi. Hakuna raha ya mapenzi kama kuwa na uhitaji, basi tu dunia imechafuka!
mimi kwa mangi na kwa wapemba naenda kukopa mwenyewe lol
maarifa yako kwa wamama wenzio tu lol
thanx Judy kwa mchango wako.....
maarifa ni kuwa na kibuzi,lol
na mimi naona weengi ndo wanachofanya...
utamchotea mtu maji upate hela
utapita kwa watu kufua nguo
utachoma chapati, mandazi and the like
utapika uji uuze stend jioni
Mkuu TB, umenirejesha nyuma kidogo enzi hizoo...!!!; wakati fulani mambo yalikuwa magumu kidogo, basi kuna siku nikakosa kabisa kitu cha kuacha home, nikasema leo 'fanya maarifa'. Niliporudi jioni nilikuta wali na kuku amejaa kwenye sufuria (Jogoo), nikamuuliza mwenzangu haya kulikoni akaniambia amepewa na jirani yetu bwana John (huyu jirani ni mshikaji ambae hana mke, mwangalizi wa nyumba ya jamaa fulani). Nilishikwa na hasira, nikachukua sufuria la wali na kuku nikaenda kutupa nje, halafu tukalala bila kula.
Asubuhi yake nikaenda kazini, yule John akanifuata kazini akiambatana na jirani mwingine; alikuja kuniomba msamaha kwa yaliyotokea na kunisihi kwamba kulikuwa hakuna baya lolote kati yake na mwenza wangu. Alinieleza kwamba siku ile mwenza wangu alikuja kumwomba kuchuma mboga ya majani (maana alikuwa na bustani ya mboga), yeye alimruhusu lakini wakati anaondoka aliamua kumpatia kuku kama zawadi kwenu japokuwa sikuwa na mahusiano ya karibu sana na wewe, lakini mwenza wako mara nyingi anakuja kuchuma mboga kwangu.
Nafikiri ili kuondoa utata wa mambo katika kufanya maarifa ni vyema kujadiliana kwa pamoja ni maarifa gani yatafanyika.
wanawake wanakuwaga na vububu! Huwa wanatunza zile chenji ndogo ndogo kwa kudunduliza wakijua kuna kesho.....................
Huwezi kuanza kufanya majadiliano maana wewe umeshindwa cha msingi kama unataka kula mwachie uhuru aamue mwenyewe afanye nini usimwingilie. Usitawaliwe na hisia mbaya kama ndio hivyo ulitakiwa kuchunguza na sio kumwaga chakula unamkatisha tamaa mkeo pale anapotaka kufanya maarifa wakati wewe umeshindwa
Miss Judith, hapo umemaliza kila kitu, hasa hilo la kusema "fanya maarifa" kwa lugha tafauti.ni kweli kabisa mpendwa
mpendwa,
maarifa mazuri hayo ila yapasa kuwa mwangalifu ili usilimbikize madeni hadi mkatamani kuhama hapo mtaani mnapoishi, si unajua lakini akina mangi wanavyodai pesa zao?
mpendwa,
kama mwanamke atachukulia hiyo kauli yako kama kibali cha kulala nje ya ndoa yake, basi jua kuwa huyo anayo hiyo tabia siku zote na ataendelea nayo hata siku ukijitosheleza kwa kila kitu na kufanya maarifa yote mwenyewe! hiyo ni tabia mpendwa, dhiki ya siku moja haiwezi kufikia hatua hiyo ya kutoka nje ya ndoa!
hapo kwenye nyekundu, mi nasema ni sahihi na halali kabisa kama culture yao hapo nyumbani inaruhusu! kila wanandoa wana ka-utamaduni kao ndani ya nyumba yao. maneno hayo yanatamkwa kila siku ndani ya nyumba zenye vipato vidogo japo kwa maneno tofauti na hayo...ila kama si utamaduni wenu kusema hivyo, unaweza kudaiwa talaka siku hiyo!! kwa hiyo wanandoa wawe makini hapo
mbarikiwe sana wapendwa,
Glory to God!
maarifa gani ambayo mwanaume akishindwa ,mwanamke ndo ataweza?????????
halafu unakuta mwanamke 'anafanya kweli maarifa' na maisha yanakwenda...
Miss Judith, hapo umemaliza kila kitu, hasa hilo la kusema "fanya maarifa" kwa lugha tafauti.
Ikiwa kumwambia mke fanya maarifa, na kama wanaume wengi wana hakika kuwa "kufanya maarifa "maana yake ni kumwambia mwanamke aende kugawa ugolo [Kongosho], basi wanaume wengi wasingekuwa wanatoa kauli hiyo, isipokuwa kama wapo, basi ni wale ambao hawaoni tabu na huwa ni faraja kwao kuwauza wake zao kwa maslahi yeo wenyewe.
Kwa mawazo yangu, hata ikifikia hadi ya mwanamume kakwama kweli, mke wake atakuwa wa kwanza kuielewa hiyo hali na hata haifikii mwanamume kumwambia afanye maarifa bali yeye mwenyewe, kwa faida ya watoto wao, atafanya maarifa yake kama aliyoyataja Kongosho #2,#4, #10ili jikoni kusilale paka.
Big up wamama wote [Nitonye#7]
Samahani sana Ms. Judith, ingawa moyoni ninalijua hilo, lakini kwa mazowea kwenye keyboard mikono ya ilipata kigugumizi.mpendwa Mammamia,
mabadiliko madogo kwenye ID yangu,
ubarikiwe sana mpendwa,