Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'


Ashadii hapa umemaliza kila kitu kabisa. Tatizo la the Boss anafikiria mpango wa kando lol. Afu wa mama huwa tunakuwa concern na kesho itakuwaje. Baadhi ya wababa akijua una haka ka akiba mbona atakubananisha umpe akalambe maji ya gold apunguze stress afu hyo kesho itajijua huko huko.
 
mimi sidhani mme akitamka fanya maarifa mke wangu anamaanisha awe na hicho mnaita kibuzi. kumbuka akiri ni nywele kila mmoja anazake, mwanamme anaweza kuwaza hadi mwisho bila kupata jawabu la kutatua matatizo katika familia yake na kwakuwa mke wake ndiyo msaidizi wake wa karibu ndiyo huhitimisha kwa kuomba msaada kwa mkewe namna watakavyo tatua matatizo yao. Kwa mke mvivu wa kufikiri na kufanya kazi atawaza kuwa na hicho kiitwacho kibuzi bali kwa yule mkakamavu, mjanja atafikiria pakutokea, yawezekana mmewe aliwaza kukaanga, kufunga na kuuza karanga rakini akaona aibu lakini kwa mke makini hilo si tatizo.
 

:A S-confused1:EDUCATION IS HOW CONFIDENT YOU ARE IN MAKING DECISION
 

Well said Mami!!! Mume wako ana kifaa trust me!!!
 

You said it right Mami!
 
Unavyomwambia mwanamke afanye maarifa wakati wewe yamekushinda
unamaanisha nini hapo? si atoke akatafute ili nae alete home?
sasa akileta unamuona ni mhuni wakati hata yeye ana kipato chake

ndo mana mm nasema nyie wanaume mnatufanya sie tuwe kwenye
mifumo yenu , mnatuweka katika nafasi ya mwisho sana wakati sie
ni walezi wakubwa wa familia kuliko nyie.
HATUTAKI KUKANDAMIZWA
 
ladyfurahia naomba nikupe changamoto hapo. Siamini kuwq mwanaume anayeijali familia atasema "fanya maarifa " kila siku.

Inatokea mara moja moja hana pesa, mtu hawezi kuwa, nacho kila siku. Na inawezekana katika yale matumizi anayotoa kila siku hutumii, yote, unajisevia kidogo. Angalau basi mambo yakiwa magumu, umpe tafu.

Hapa hatuongelei nani mlezi bora wa familia, bali mtoaji katika familia. Huyo mtoaji kuna, siku nae anakosa, hapo akisema fanya maarifq ndo wewe ujaribu au kuchukua savings zako, au kukopa nk..

Wanawake wanaolinda familia zao sidhani kama watapata shida kwa hilo, as long as it doesn't happen frequently!
 
Last edited by a moderator:
hapo nimekuelewa mkuu asante kwa kuniweka sawia
 
maarifa ni mengi kwa mwanamke
hasa village girls
utaomba unga kwa jirani
utakuwa na bustani ya viazi
utakuwa na bustani ya mboga mboga
utakusanya kuni uuze

so many

Na pia wamama wanajua kutunza akiba zao so pengine anaweza kua na hela bila baba kujua
 
Tatizo linakuja pale mwanaume anapoona kumbe inawezekana eeeh. Basi utafanya maarifa kila siku. Hawa waume wa Kibongo balaaa.
 

Kwanza tungewauliza nyie wanaume, au ungeuliza wanaume wenzako naamini wanayo majibu ya busara . Halafu wanaume wa siku hizi wana makusudi nyingi sana
 
Tatizo linakuja pale mwanaume anapoona kumbe inawezekana eeeh. Basi utafanya maarifa kila siku. Hawa waume wa Kibongo balaaa.

hahaa haaa hili dongo limetugusa wengi..
 
Kwanza tungewauliza nyie wanaume, au ungeuliza wanaume wenzako naamini wanayo majibu ya busara . Halafu wanaume wa siku hizi wana makusudi nyingi sana


we huwezi maarifa kabisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…