Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

mfano vunja kile kisanduku chako unachoweka vi mia mia, lakini ukimwambia direct hivi kwamba vunja hicho kisanduku hupati ng'o bora useme indirect kama ambavyo umesema hapo juu!
 
we huwezi maarifa kabisa?

Nitajibu vyema kama nikijua maarifa yanayozungumzwa. ila kama ni kuwezesha familia baba anaposhindwa ninaweza fanya maarifa. kwani na mimi nina kazi inayonipa kipato na kama mama wa nyumba yanipasa kutumia busara tele pale mwenzangu anapoishiwa. tatizo lenu wanaume siku hizi mkishaona mama anaweza kutoa basi kila wakati nyinyi mmekwama na kumsukumizia mwanamke majukumu tele.

ila kwa wale wanaume wanaojua wake zao hawana kazi yoyote wanapowaambia wakafanye maarifa kwa kweli siwaelewi kabisa
 
Wanawake huwa wanabana kiasi fulani cha pesa za matumizi ya nyumbani na kuzificha. Siku mume ukikwama mwanamke anazitoa zile pesa, wengine watajifanya wamekopa kwa wenzao
 
Wanawake tuna maarifa mengi ikiwemo kuweka akiba,mkitupaga matumizi hua tuna tabia ya kuweka,siku dingi akikwama mama unaingia kwny kibubu siku Zinasonga!
 
Tatizo wanawake wasio na busara kitendo cha kuambiwa hivyo ndiooo kwanza fungulia mbwa na dharau juu
 
wanawake wengi wa mjini
kufanya maarifa ni kwenda kwa kibuzi......ndo maana hili neno la kufanya maarifa linanitatiza mno...
Mhmmhmhm kuna tafiti yoyote imefanyika [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Maarifa ya kujiongeza ili kuokoa jahazi...ila sasa inategemea sasa na kazi kama mwanamke anayo ama laa!
 
Maarifa ni zile ulizoficha kwa ajili ya kitchen party
 
mwamie huyo Aisha kama mumewe amemuambia afanye maarifa anicheki inbox
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…