Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Sijawai kuifanya hii app,ngoja kidogo!
Vizuri sana usiijaribu ndugu yangu yaakakukuta kama yaliyomkuta babu wa watu..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijawai kuifanya hii app,ngoja kidogo!
hahaha yaani ulitakiwa ulipozaliwa uitwe Huba weye, Moyo wako wako,Stori zako,Sauti yako [emoji23] zimepambwa kwa manukato ya mahaba tu Kasie mahaba wee. Yaan ukiingia tu humu ndani ya Jf lazimia nisikie harufu ya huba lako.Hahahahahahahaa Dilekeni dikeleni...... hehehehee looh acha nicheke kwanza sio kwa mabusu hayo..... asante best naona mabusu motomoto ujue mie ni Kasie Mahaba. ...... hehehehehe shauri lako...
Umenifanya nikumbuke busu alilopewa Mange na Roma Mkatoliki atii mmwaah. .. heheheheheee
Umemtaja James Jeddah mjeda akija hapa ujiandae kupigana shauri yako, mie simoo.
Karibu niko fildi kukusanya dodoso kumeanza tena.
Asante kunimiss ndo mie hapa nimejaa telee
Hahahahaaa inabidi uombe kibali cha kunibatiza niitwe Hubaa hehehehehehahaha yaani ulitakiwa ulipozaliwa uitwe Huba weye,
Moyo wako wako,Stori zako,Sauti yako [emoji23] zimepambwa kwa manukato ya mahaba tu Kasie mahaba wee.
Yaan ukiingia tu humu ndani ya Jf lazimia nisikie harufu ya huba lako.
[emoji23] [emoji23] Ya JJ tuyaache maana najua utanitetea, jicho lako tu latosha kushusha munkari wa yule bwana,
Yeah usemacho ni kweli kabisaa....Daah habari ya madodoso umenikumbusha mbali sana,kuna experience unaipata huwezi kuipata kokote kule,ingawa watu hawawi wakweli sometimes ila ni kitu flani unique sana ktk kujifunza na kupata taarifa. All the best, usije walewesha wana kaya na hayo mahaba yako.......madodoso yatakosa udodosi [emoji23] [emoji23]
[/QUOTE] hahaha haya niambie hiko kibali naende kukiombea wapi,najitoa muhanga mie @HubaaHahahahaaa inabidi uombe kibali cha kunibatiza niitwe Hubaa
Moyo wako wako,Stori zako,Sauti yako [emoji23] zimepambwa kwa manukato ya mahaba tu Kasie mahaba wee. Yaan ukiingia tu humu ndani ya Jf lazimia nisikie harufu ya huba lako.
[emoji23] [emoji23] Ya JJ tuyaache maana najua utanitetea, jicho lako tu latosha kushusha munkari wa yule bwana,
Daah habari ya madodoso umenikumbusha mbali sana,kuna experience unaipata huwezi kuipata kokote kule,ingawa watu hawawi wakweli sometimes ila ni kitu flani unique sana ktk kujifunza na kupata taarifa. All the best, usije walewesha wana kaya na hayo mahaba yako.......madodoso yatakosa udodosi [emoji23] [emoji23]
hahaha haya niambie hiko kibali naende kukiombea wapi,najitoa muhanga mie @Hubaa
hahaha yule hana nguvu kwako,ahemi,hapumui wala hakooi,chezea kumbato la huba lako [emoji23] [emoji23] Idhin yako ndio jambo la msingi zaidi kwangu kuliko chochote,afu si unajua mi na yeye damu zetu haziendani kabisaa [emoji23] [emoji23] Kasie umeniuzia kesi ujue.Weeweee shauri yakooo, nime update hapo juu angalia quote nimeirekebisha.
Mtafute mtoa kibali yupoo....
Habari za jumapili wapendwa,
Leo nina kisa kioja swali...
Kwenye pilika pilika zangu za umesenja nikiwa fildi huko kukusanya dodoso kwa ajili ya miradi kadha wa kadha inayofadhiliwa na watu wa Mashariki ya mbali ndo nilikutana na kioja hiki.
Nilikaribia nyumba ya nne tangu nianze kukusanya dodoso nikiwa nimeambatana na mwenyeji wangu baada ya kunitambulisha yeye aliondoka kuendelea na shughuli zake na kuniacha mie niendelee na dodoso.
Baada ya dodoso kuisha nikiwa nataka kumuaga yule mwenye nyumba nirudi nilipofikia - nyumba ya kulala wageni... yule baba akaniambia mwanangu nina maswali.... nikamsikiliza na kumjibu kwa ufasaha. Akaniambia amejisikia tuu kunisimulia kisa alichokumbana nacho kwenye maisha yake na kumfanya hadi wakati huu hana familia. Ni babu mzee ambaye anajiweza kujimudu ila ndo anaishi mwenyewe na hana mtoto wala mke.
Basi mpenda masimulizi mie nikarudi kuketi nimsikilize babu ananisimulia nini.
Mwanangu, usemi wa kumwambia aliyekuwa mke wangu kipindi hicho umenifanya hadi leo sina familia Maana niliumia sana na sikuwa nimemaanisha alichokielewa mwanamke yule.
Huo mwaka hali ilikuwa ngumu mazao shambani hayakukubali biashara ya samaki mtoni pia ilikuwa ngumu. Nakumbuka siku hiyo nilirudi nyumbani saa kumi alasiri nikiwa sina kitu kwa ajili ya familia kula, nikamwambia mke wangu "FANYA MAARIFA BASI LEO TULE "nimerudi mikono mitupu.
Mke wangu aliguna na kubinjua midomo huku akinitizama kwa jicho la upande.... nakumbuka hakuniambia anaenda wapi ila alijitanda khanga na alitoka. Nilisikia harufu ya marashi aliyopaka baada ya kupiga hatua takriban tatu hivi. Nikakaa uani kusubiri maarifa ya mke wangu, kweli saa 12 jioni alirudi na kibaba cha mahindi, unga na choroko na usiku ukapita. Hilo ndo lilikuwa kosa langu tangu hapo mke wangu alianza kutembea na wanaume pale kijijini akisingizia anafanya maarifa tusilale njaa hata kama nikirudi na kitoweo nyumbani. Hali ile sikuweza kuivumilia nilimrudisha kwao na hatukuwa tumebarikiwa watoto. Tangu hapo sikutaka tena kuishi na mwanamke.
Sasa mwanangu hebu niambie. .. kwanza wewe una watoto? Nikamwambia hapana, umeolewa? Nikamwambia hapana...
Ila hivi mwanaume akamwambia mwanamke wake FANYA MAARIFA huwa mnaelewa kuwa amekutuma ukatembee na wanaume ndo ulete chakula nyumbani? Nikamwambia baba hapana si unaona mie niko kazini hapa ndo nipate mlo wangu japo sina wanaonitegemea.
Wewe unaelewaje?
Nikamwambia ningekuwa mie ningeenda kwa mwanamke mwenzangu pale kijijini aniazime kibaba cha unga na maharage au kunde kisha ukipata namrejeshea na si kwenda kukiuza kwa wanaume.
Haya mwanangu nakutakia kazi njema. Nikamjibu asante baba.
Swali kwa wakaka.....
Huwa inatokea siku hauna kitu na unaomba mwenzi wako aku assist? Anapokeaje ombi lako? Je ni fedheha kwako?
Swali kwa wadada na wamama....
Kufanya maarifa unaelewaje hasa ukiambiwa na mwenza wako siku anapokuwa hana kitu. Ni sawa au unaona si sawa?
Wiki moja baadae nikiwa kwenye sehemu ya umma wa watu wengi, mschana mmoja akiwa anaongea na wenzie akasema... mie bwana angu akiniambia mke wangu leo sina kitu fanya maarifa.... naenda kutembea na bwana nyuma yake tuu hapo mtaa wa pili wala siendi mbali....
Unafikiri kwanini huyu mschana amewaza hivi?
Kasie Mahaba.
Hahahahahaaa wee babu umeibukia wapi? Hivi upoo? Nilijua nawe umekumbwa na gonjwa la kuogopa uhenga na kuja na NEW ID. .....
Maana humu unashangaa ID huijui na ni ngeni ila utasikia... Kasie za siku nyingi... nimekumiss....
Nashukuru kukuona bado upo japo si kama enzi zako zile ulikuwa akitivu hadi rahaa...
Back to the topic, kiukweli hata sikujua kama ulishaweka bandiko linalofanania na alikoweka Kasie.
Mie nilikutana na huo mkasa nikiwa fildi kukusanya dodoso wiki kadhaa zilizopita.
Wasalimie .........
Kasie Mahaba.
The Boss Wanawake wana maarifa mengi sana,Muuza genge anafahamiana naye, muuza bucha anataniana naye, Kwa mangi ndio usiseme, Vibubwi ndio wenyewe, Kwenye michezo ya kina Mama anacheza michezo Mitatu majina mawilimawili yote anapokea,VICOBA ndio anakowekeza, Vyama vya wamama mitaani huko nako wamo. Maarifa ya mwisho ni yeye mwenyewe...
Sasa 'haya maarifa' ya wanawake ni yapi?
Nimo kwny jamii mkuu kwanini nisiyajue, Nina ndg, marafiki na majiraniKapeace my dia unayajuaje haya?
Mi najua kuwajibika mama, usinitemee makohozi hayoMwanaume asiyejua kuwajibika kwa ajili ya familia yake sielewi nimuweke kundi gani wanakera wanakera mpaka basi yaani unatamani hata umtemee makohozi, yaani mume wa ivo putuuuuu