Inategemea kua hio shida ni of what nature.... Kuna ile kama inahusiana na chakula ndani, anaona tu aibu kusema nenda angalau kwa wazazi kaombe unga kidogo tumekwama... anaona bora akwambie kua "fanya maarifa"..... Kawaida ya mwanamke ambae ni mwerevu (walau that is what I think) ni kutambua kua sio kila siku mume wake ataweza provide - na kwamba hata kama anaweza inaweza tokea in rare cases akakwama. Daima kulinda heshima ndani ya ndoa yenu inatakiwa kua na akili ya ziada mkichwa na maarifa pia....
Hivo basi daima hata kama woote wanafanya kazi na woote wana provide, ni lazima aweke akiba pembeni popote pale ndani ya nyumba ambayo inakua ni kinga ya kutatua tatizo pale ambapo litajitokeza na woote wasiwe na pesa (yaani mume na yeye mwenyewe mke); Hio akiba sio wanaume woote hujua kua inakuwepo.... Inapotokea kua kuna siku mlikwama kabisa mara nyingi akina mama huchukua hio akiba kuokoa jahazi kwa kumshirikisha mumeo na kumwambia "mume wangu nimeazima kwenye kikundi chetu kile cha upaku" sababu ya kusema hivi sio kwamba humuamini mumeo.... No! Ila tu ni ile haitakiwi hajenge kichwani mwake kuna akiba ndani for next time akikwama he wont try harder..... Hivo baas mara nyingi wanaume husema hivo sababu wanakua weshawahi pita in jams na mke aliokoa jahazi.... Siamini kua hua wanasema hivo kwa maana kwamba nenda kwa mpango wa kando ukatafute pesa.
Boss it has been Long.... Usiku mwema.