Kuna aliyenufaika na huu mfumo wa post code (anuani za makazi) hapa Tanzania?

Kuna aliyenufaika na huu mfumo wa post code (anuani za makazi) hapa Tanzania?

Hakuna faida yoyote kwakweli , flashback zile mambo ya MKUKUTA haijaleta positive impacts kwa wananchi 📌 things are tough 😓
 
Na vile vibati vyenyewe nilitoa hela yangu ili waweke mwanzo walichora ukuta na mkaa na nyumba ni mpya wapuuzi hata ustaarabu hawana
 
Habari wana Jf!
Moja kwa moja nende kwenye swali langu hapo juu.
Katika mtaa wetu tulibahatika kupitiwa na zoeli la anuani za makazi kama serikari ilivyotangaza.

Na ni kweli tuliandishwa na kupewa namba na majina ya mtaa yaliyochaguliwa.
Cha ajabu ni kwamba watu tumebaki na namba lakini hakuna kilichoingizwa kwenye mfumo.
Ukiuliza TCRA na kuwapa taarifa za kukosekana kwa tariifa za majina na mitaa husika wanasema, huu mfumo ni endelevu na kila mmoja atafikiwa.

Mbaya zaidi kuna baadhi ya mitaa imejirudia majina na mingine haipo kabisa.

Swali langu kwenu wanajamii wenzangu mlioitikia wito huu wa serikali yetu kutufikisha kwenye ulimwengu wa Technology;

Je! Hizi post code zimewasaidia?
Mnaoagiza vifurushi na bidhaa mbalimbali mtandaoni, bidhaa zenu zinawafukia mahali mlipo au ndio mchezo uleule wa kuzifuata kwenye makampuni husika?

Na je kwenye ujazaji wa anuani hizo kwa baadhi ya document kwenye makampuni ya biashara mtandao hakuna usumbufu?

Karibu kwa ufafanuzi!
Taaluma ya Mipangomiji ni taaluma ya Sayansi Asili (Natural Science) au Pure and Applied Science, siyo SIASA.
SAYANSI kwa kawaida huwa ina misingi yake ambayo ni lazima uifuate ili kupata matokeo yanayokusudiwa.
In short, Mipango-miji ni SAYANSI, ukifuata KANUNI 'Matokeo Chanya' utayapata, na Usipofuata Kanuni 'Matokeo Hasi' lazima utayapata.
 
Tanesco na mamlaka za maji wanafikaje kutowa huduma na Mita za maji wanasoma vipi?
Kwa sisi tuliounganishiwa umeme na maji tatizo likitokea ni lazima utoe maelezo ya kutosha ndio wakufikie. La sivyo utabaki na tatizo lako. Na ndio maana tunauliza faida yake iko wapi?
 
Taaluma ya Mipangomiji ni taaluma ya Sayansi Asili (Natural Science) au Pure and Applied Science, siyo SIASA.
SAYANSI kwa kawaida huwa ina misingi yake ambayo ni lazima uifuate ili kupata matokeo yanayokusudiwa.
In short, Mipango-miji ni SAYANSI, ukifuata KANUNI 'Matokeo Chanya' utayapata, na Usipofuata Kanuni 'Matokeo Hasi' lazima utayapata.
Uko mwaka wa ngapi huko chuo Mkuu!
Huu mfumo wa post code upo katika kundi lipi katika haya mawili uliyosema?
"Taaluma ya Mipangomiji ni taaluma ya Sayansi Asili (Natural Science) au Pure and Applied Science, siyo SIASA."
 
Pole yako sana, hujanielewa comment yangu hii, lakini sishangai kwa sababu najua sababu ya wewe kuwa na mtazamo wa namna hii ni kukosa "EXPOSURE." hapa duniani.
Endapo kama ungewahi kufika au kuishi kwenye nchi mojawapo iliyoendelea sana kwenye suala hili la Mipango-miji na Misimbo ya Makazi (Post-Codes &Area Codes), nadhani ungenielewa vizuri sana kwenye comment yangu hiyo ya hapo juu. Comment yagu ime-base kwenye "real experience" niliyopitia kwenye maisha yangu niliyopitia nilipokuwa kwenye nchi za wenzetu, wala siyo kupitia 'nadharia' za kufikirika za kusoma darasani
 
Hapa Manzese kata ya midizini kuna mitaa kadha ilivumbuliwa wakati wa zoezi hilo la sensa ya makazi Kama vile Pilot,Sokoni,Mwendokasi etc na vibao vimewekwa ila ajabu ukifuatilia barua ya utambulisho serikali ya mtaa wako Jina linalotumika ni lile lile la zamani " Midizini" na namba ya zamani, hilo lipo hata ukijaza taarifa za RITA au Uhamihaji.
Kifupi anwani mpya za mitaa hazitambuliki na system za taasisi za serikali yenyewe
 
kuna vitu vingi sana umeuliza unaweza kuspecify concern ni ipi
moja umesema kuna maeneo yana post code, unakaa kata ipi na mtaa upi ambao hauna post code?
weka jina la eneo lako ili tusearch kwenye website tujue ukweli
pili umeuliza kuhusu faida za post code , upo serious hujui?
Kipi usichelewa uelekezwe?
Nimeongelea waliojisajiri lakini taarifa zao hazipatikani, mitaa kujirudia majina na mingine kutopatikana kulinganga na majina yaliyopo, nimeuliza wajasilia mali wanao agiza bidhaa nje ya nchi kama mfumo huu umewasaidia kuwafikishia bidhaa zao katika anuani husika,( na hawa ndio wanajua vizuri faida ya postcode)
Najua kata zote ukiangalia kwenye website yao zipo.
Sasa kama kila mmoja ana anuani binafsi za mbona mashirika mengi yanashindwa kuzitumia na wakati wana taarifa zako zote?
TCRA wenyewe ukiwauliza wanakupa namba za maofisa wa kata husika uongee nao. Ukiuliza wanakuambia zoezi hili ni endelevu watafika katika huo mtaa husika na wataalam wa TEHAMA. Ukipewa jibu hilo ndio nitolee
 
Pole yako sana, hujanielewa comment yangu hii, lakini sishangai kwa sababu najua sababu ya wewe kuwa na mtazamo wa namna hii ni kukosa "EXPOSURE." hapa duniani.
Endapo kama ungewahi kufika au kuishi kwenye nchi mojawapo iliyoendelea sana kwenye suala hili la Mipango-miji na Misimbo ya Makazi (Post-Codes &Area Codes), nadhani ungenielewa vizuri sana kwenye comment yangu hiyo ya hapo juu.
Sawa mkuu! tusirumbane.
Moja ya faida nilizoziona kwenye nchi za wenzetu ndio kilichopelekea niulize hapa kwetu Tanzania.
 
Sawa mkuu! tusirumbane.
Moja ya faida nilizoziona kwenye nchi za wenzetu ndio kilichopelekea niulize hapa kwetu Tanzania.
Tz haikufanikiwa kwenye suala hili la Postcodes kwa sababu Serikali ilikurupuka Kisiasa ktk kutekeleza Jambo hili la kisayansi, walipaswa Kwanza Kufanya Miradi ya Mipango-miji ndipo lingekuja suala hili la Postcodes. Msingi mkuu kabisa wa Postcodes mahali popote pale duniani ni Mipangomiji, endapo kama hakuna Mipango-miji basi hakuna Mradi wowote wa Postcodes unaoweza kuwa "viable."
 
Huna akili, mtu yeyote mwenye exposure aliyesafiri duniani anajuwa faida za post code.

Ndugu zenu wengine wapo ulaya muda huu kazi yao ni zao la post code Wanasambaza magazeti na brochure mbalimbali na baiskeli mitaani kila nyumba.

Ni mjinga peke yake ndio hawezi kujuwa faida za Post code.

Kuna wakati nilikuwa nadhani una akili kwa kuangalia username yako lakini nawe leo na conclude categorically....WEWE HUNA AKILI TIMAMU.
 
Habari wana JF,

Moja kwa moja nende kwenye swali langu hapo juu.

Katika mtaa wetu tulibahatika kupitiwa na zoeli la anuani za makazi kama serikari ilivyotangaza.

Na ni kweli tuliandishwa na kupewa namba na majina ya mtaa yaliyochaguliwa. Cha ajabu ni kwamba watu tumebaki na namba lakini hakuna kilichoingizwa kwenye mfumo.

Ukiuliza TCRA na kuwapa taarifa za kukosekana kwa tariifa za majina na mitaa husika wanasema, huu mfumo ni endelevu na kila mmoja atafikiwa.

Mbaya zaidi kuna baadhi ya mitaa imejirudia majina na mingine haipo kabisa.

Swali langu kwenu wanajamii wenzangu mlioitikia wito huu wa serikali yetu kutufikisha kwenye ulimwengu wa Technology; je! Hizi post code zimewasaidia?

Mnaoagiza vifurushi na bidhaa mbalimbali mtandaoni, bidhaa zenu zinawafukia mahali mlipo au ndio mchezo uleule wa kuzifuata kwenye makampuni husika?

Na je kwenye ujazaji wa anuani hizo kwa baadhi ya document kwenye makampuni ya biashara mtandao hakuna usumbufu?

Karibu kwa ufafanuzi!

Kwahiyo wewe huwezi kuwa na busara za kupanda Miti ili kizazi chako kije kufaidi kimvuli?

Ukiona umekaa kimvulini, elewa kuna watu wenye busara walipanda hiyo Miti.

Labda faida ya anwani za makazi tutaziona baadaye

Tuna viongozi vichaaa
Vichaaaa
Vichaaaa
Vichaaaa sana.
Wakienda ulaya wakikuta kitu wanakuja kuaply huku.
Mabilioni yale ya post code yangetumika kuboresha afya na elimu.
Mtu anakaa Nyumba ya nyasi post code itamsaidia nini?
SHUHUDA: Mimi mwenyewe natumia post code, nime integrate kwenye ecommerce yangu. Numetumia kwa namna hizi

1. Website ina panel ya logistic agence (kama Posta) hapa inatoa direction ya kwenda kuchukua bidhaa kwa muuzaji

2. Pia delivery agence anapata direction ya ku delivery parcel

3. HII NI Muhimu sana, ninetumia postcode ku calculate shipping/delivery cost, kwa hivyo mtu akinunua bidhaa akiwa point A na mwingine point B shipping cost ni tofauti kabisa

Ukininunua kitu hapa unaletwe hadi mlangoni

Kwenye digital economy postcode ni za muhimu sana ni kwamba sio wengi wanaweza kuzitumi ndio màa zinaonekana hazina tija
 
Niambieni kitu gani kimefanikiwa bongo zaidi ya wizi na ajali
Eti postcodes hivi uki Google map anuani kwa namba na mtaa itakuleta

Wanajua kutafuta hela za kuiba na ndio maana hakuna kitu kinachoendelea eti wazalendo
 
Kipi usichelewa uelekezwe?
Nimeongelea waliojisajiri lakini taarifa zao hazipatikani, mitaa kujirudia majina na mingine kutopatikana kulinganga na majina yaliyopo, nimeuliza wajasilia mali wanao agiza bidhaa nje ya nchi kama mfumo huu umewasaidia kuwafikishia bidhaa zao katika anuani husika,( na hawa ndio wanajua vizuri faida ya postcode)
Najua kata zote ukiangalia kwenye website yao zipo.
Sasa kama kila mmoja ana anuani binafsi za mbona mashirika mengi yanashindwa kuzitumia na wakati wana taarifa zako zote?
TCRA wenyewe ukiwauliza wanakupa namba za maofisa wa kata husika uongee nao. Ukiuliza wanakuambia zoezi hili ni endelevu watafika katika huo mtaa husika na wataalam wa TEHAMA. Ukipewa jibu hilo ndio nitolee
Boss kuhsu kuagiza tunaagiza sana ila hizo post code hazijasaidia kuleta huduma mpaka home.
Mara kadhaa niliagiza kupitia Speedaf mwanzo nilijaza anwani ya wazee pale maduka mawili Chang'ombe ila mtu wa deliver alipiga simu nimfuate mwembe yanga na nilipoagiza kwa kuweka address ya nyumba Mtaa wa mwendokasi manzese mzigo kufika napigiwa simu nimfuate jamaa tiptop so huduma mpaka mlangoni Tz bado sana
 
Sema viongozi wakubwa wa TCRA na wakubwa wa mikoa ndio wamezifaidi sana.
 
Back
Top Bottom