Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Kwa hiyo tafsiri yako unataka ili uitwe mlipa kodi lazima uwe na TIN uwe unailipia directly whether una biashara au huna ila ukienda kudai risit ya malipo kwa muuzaji we siyo mlipa kodi?
Kama huna biashara au kazi inayokuwezesha kulipa Kodi hiyo Hela ya kununua bidhaa unaipata wapi? Isijekua tupo na majambazi humu
 
Uache upumbavu Kati ya watu M60 ni M2 tu ndio walipakodi ?
Weka wewe ukweli hapa sasa mbona unapinga bila takwimu? Yeye kakuonyesha mpaka takwimu bado umekaza fuvu tu[emoji23] haya pitia bajeti kuu, pitia bajeti ya kila wizara halafu angalia mapato ya ndani ndio uje kubishana Kwa takwimu badala ya kubwabwaja tu hapa
 
Hizo link wametoa wenye tin number siyo idadi ya walipa kodi. Kulipa kodi ni wajibu wa kila raia ndo maana tunasisitizwa kudai risit halali ya malipo tuliyofanya ili kodi zetu zifike kiuhalisia.
Jitahidi uwe na tin number ACHA kuishi kiujanjaujanja unanyonya wenzako
 
Ya simu unamaanisha Tozo?

Kodi inayoongelewa hapo ni ya kile unachozalisha wewe, Kama ni Mfanyakazi Kuna PAYE, Kama Ni Mfanyabiashara ama unamiliki Mali nyengine Kuna Tin no etc.


Haiwezekani unamiliki Mijumba kibao unaingizia mamilioni ya Hela kwa mwezi hulipi kodi eti unasema nilipojaza mafuta Gari nimelipa kodi?

Kodi ni Ile unachozalisha na sio alichozalisha mwenzako.
Haelewi huyu Kodi inatokana na mapato ya ulichozalisha vinginevyo wewe ni jambazi/tapeli
 
Hicho ndo wasichokijua. Mi ninunue umeme umeweka VAT eti unasema silipi kodi ila mlipaji ni tanesco. Nibet nile mil.5 nakatwa tax napewa mil.4 unasema silipi kodi. Rubbish kabisa, bora wewe umemfafanulia vzr.
Tueleze hiyo Hela unayoyafanyia yote hayo umeilipia Kodi ya mapato? Vinginevyo hiyo Hela hujaipata kihalali
 
Mkuu ukishinda million 100, serikali inakukata MSHINDI at least 12-18M.

Kingine Kodi nyingi ni shiftable, mfano gari linapotoka kiwandani Bei yake ni million 5 lakini mpaka lifike downstream market Bei ishafika 8m hapo ukinunua wewe na kuagiza kwa CFI unakuta limefika 15M hivi unadhani hiyo 10m iliyoongezeka hakuna ushuru uliohamishwa kutoka Kwa TOYOTA kuja kwa mlaji wa mwisho??

Bei za bidhaa zote zimechajiwa kwa wazalishaji ila wao wanapouza Wana include Ile Kodi waliyokatwa so mwisho wa siku WEWE unailipa sio WAZALISHAJI tena.
So mzalishaji hua halipi Kodi?
 
Hujanielewa concept yangu, kinachotakiwa ni VALUE sio QUANTITY ya walipaji!! Kodi ya FDIs kubwa 100 zina offset Kodi za wamachinga wote!!

Kingine unielewe, Kodi nyingi in VALUE zinatokana na indirect tax, haya matozo, Kodi za miamala, VAT kwenye bidhaa zinaingiza pesa nyingi kuliko PAYE au Corporate Tax!! Sababu Kila mtu ananunua bidhaa whether ana kazi au Hana, ila hao wanaolipa DIRECT TAX ni fraction tu ya tax base.

So ni makosa kudhani waTanzania million 30 hawalipi Kodi ilihali wananunua bidhaa ambazo kama nilivyoeleza hapo juu Zina SHIFTABLE TAX yaani mzigo wa Kodi wa mzalishaji anaishia kulipa mteja wa mwisho.
Hizo fedha za kununua bidhaa wanazipata wapi ilhali umesema hawana kazi/shughuli yoyote?
 
Hii nchi inajenga madarasa miaka yote.... Yaani toka Nyerere. Ina maana population yetu inakuwa kwa speed kubwa kuliko nchi nyingine au ni mipango yetu mibovu?
Wakati tunapata uhuru 1961 tulikuwa milioni 8 au 10 Leo tupo watu milioni 60 au 65 kama sikosei
 
Hizo fedha za kununua bidhaa wanazipata wapi ilhali umesema hawana kazi/shughuli yoyote?
Wanazipata kupitia multiplier effect, Kumbuka pia nusu ya waTanzania ni watoto yaani below 18 so wengi ni dependents, pia Kuna remittances hizi ni pesa wanazotuma watu kutoka nje au hata ndani mfano mzazi yupo kijijinu n.k

So mpaka watoto tegemezi wanalipa Kodi kupitia indirect tax kwenye pipi, biskuti, vocha n.k.
 
Hao wanaotia mafuta hela zao wanapata wapi? Sababu anaelipa kodi hapo ni mwenye kituo cha mafuta. Imeingia kodi ya Mtu mmoja,

Huyo anaejaza mafuta Sasa sehemu anayoingizia Kipato amelipa Kodi?
sasa wewe kuna vitu huvielewi
 
Hela zooote hizo zikikusanywa Hazitoshi hata budget yetu kujitegemea wenyewe, tuna tegemea wafadhili watuongezee

Nchi ina watu zaidi ya milioni 60, milioni 2 tu ndo walipakodi, hizo hela unazoona ni nyingi Hazitoshi hata kidogo.

Tra wanakusanya Around Trilioni 1, kwa mwaka ni kama Trilioni 18, Hapo Kuna Trilioni 6 mishahara na Trilioni 7 deni la Taifa, hapo Tayari umekaribia kumaliza hela yote

Bado Kuna Miradi ya Matrilioni ya Hela karibia 20 na matumizi mengine yasiyo Mishahara ya Serikali Takriban Trilioni 4.

Kasome budget yako mambo yote yameelezewa

walipa kodi mil 2!mil 58 je?
 
Weka wewe ukweli hapa sasa mbona unapinga bila takwimu? Yeye kakuonyesha mpaka takwimu bado umekaza fuvu tu[emoji23] haya pitia bajeti kuu, pitia bajeti ya kila wizara halafu angalia mapato ya ndani ndio uje kubishana Kwa takwimu badala ya kubwabwaja tu hapa
Kila mtumia bidhaa ni mlipa Kodi!
 
Back
Top Bottom