Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Kwanza una tin number? Kwa sababu nyie mnaolialia hapa utakuta ndio wanyonyaji wakubwa
TIN mi nilimiliki kabla hata wewe hujazaliwa kwenye biashara yangu! Nakatwa Kodi ya 67k Kila mwezi as PAYE.
 
Habari JF,

Mimi kama mtanzania wa hali ya chini nimekuwa nikifuatilia namna wananchi tunavyolipa kodi na Tozo mbali mbali lakini kuna mikopo mikubwa sana tumechukua ndani ya kipindi kifupi.

Kila nikijaribu kufuatilia pesa hizi zinatumika wapi sipati majibu sahihi, wengine wanasema JPM aliacha Nchi haina pesa kabisa hivyo zinapelekwa kwenye miradi, ukiwauliza mbona mpaka anaondoka miradi ilikuwa inaendelea vizuri? Wanakosa majibu.

Baadhi wanasema zinakwenda kwenye mirafi mipya, ukiwauliza ni miradi ipi hiyo mikubwa ya trilions of money wanakosa Jibu.

Nikajiuliza je zinakwenda kulipa mishahara ,posho na mafuta magari ya serikali nimeona bado tumekusanya pesa Nyingi.

Swali kwa wale wanaojua pesa hizi zinakwenda wapi atoe jibu tafadhari ,ili nikatwe kodi/tozo nikiwa na Amani.
Zawadi kwa Kila goli mashindano ya caf, kulipana posho kwenye seminars nk ( refer Kuna Uzi wa TANAPA) nk
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Back
Top Bottom