Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
 
sasa si ungeandika vizuri kwanza bandiko lako
 
Nimeshangaa walimu nao wanaandika
  1. Alima wakimaanisha Halima
  2. Muagama wakimaanisha Mhagama
  3. Asumani wakimaanisha Athuman
  4. Mwanaamis wakimaanisha Mwanahamisi
  5. Alamisi wakimaanisha Alhamisi
  6. Maali wakimaanisha Mahali
  7. Maharifa wakimaanisha Maarifa
  8. Maangahiko wakimaanisha Mahangaiko
  9. Nisamee wakimaanisha Nisamehe
 
Mungu atusaidie mimi naogopa sana, tutakuja kuletewa program ya universal writing skills education (UWSE)
 
Yaani hapa kuwaelimisha herufi tu miaka 100
Je kutengeneza vitu na kubuni itakuwa 200 mingine
Bado tuko nyuma sana kwa kweli
Kuna think tank wetu wao wanaumiza vichwa ili watoto wawe wapumbavu mpaka wanakuwa
Na hao ndio wameshika nchi
Roho zao mbaya wanahakikisha nchi na watu wake wabaki masikini daima
 
Kwani ni Charts au Chats?, Tuanzie hapo🙄
 
CC
chawa wa chama chetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…