Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Yaani hapa kuwaelimisha herufi tu miaka 100
Je kutengeneza vitu na kubuni itakuwa 200 mingine
Bado tuko nyuma sana kwa kweli
Kuna think tank wetu wao wanaumiza vichwa ili watoto wawe wapumbavu mpaka wanakuwa
Na hao ndio wameshika nchi
Roho zao mbaya wanahakikisha nchi na watu wake wabaki masikini daima
Think Tanks ndio hawa wanaoruka sarakasi bungeni?
 
Anza na hapa hapa jf. Kiswahili chetu kinazidi kuwa kibovu. Yaani sisi ni shida kwa mfano vijana ukiwasikiliza utagundua wanachanganya kueleza na kuelekeza. Kuahirisha wenyewe wanaandika kuhairisha iko siku wataandika kuharisha. Tunahitaji kuwekeza kwenye kukuza na kufundisha Kiswahili.
Jamani jamani hali ni mbaya sana elimu elimu, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, charts na etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno,

Mungu aingilie kati hili anguko naogopa sana tuko twendako.

Ni hayo tu

Wadiz
 
Nimeshangaa walimu nao wanaandika
  1. Alima wakimaanisha Halima
  2. Muagama wakimaanisha Mhagama
  3. Asumani wakimaanisha Athuman
  4. Mwanaamis wakimaanisha Mwanahamisi
  5. Alamisi wakimaanisha Alhamisi
  6. Maali wakimaanisha Mahali
  7. Maharifa wakimaanisha Maarifa
  8. Maangahiko wakimaanisha Mahangaiko
  9. Nisamee wakimaanisha Nisamehe
Asante wakimaanisha Ahsante, tena tangazo lipo kila siku kwenye tv, sijui Bakita wako wapi.
 
Aliyetoa hiyo certificate alishindwa kuedit matokeo yake ametoa kitu Cha ajabu
 
Asante wakimaanisha Ahsante, tena tangazo lipo kila siku kwenye tv, sijui Bakita wako wapi.
Inabidi itungwe sheria ya kukilinda Kiswahili, chombo chochote cha habari kikiharibu lugha tu kipigwe fine
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Na hili tatizo linakolezwa zaidi na watu kuwa jeuri wanapoambiwa ukweli. Ukimsahihisha mkosaji, anachofanya ni kujaribu kutafuta makosa yako ili akusahihishe. Au wengine watakuambia ''kuandika maneno vizuri kutaniletea maisha mazuri?''.
 
Nimeona

Angalia kitenzi ni tuende au twende? Enda, nenda, (tuende/twende) karibu sana ndugu mwalimu
Kwenye nafsi ya kwanza na uwingi ,mofimu zinazotumika ni "ni" kwa nafsi ya kwanza umoja na "tu" kwa nafsi ya kwanza uwingi na sio "tw" kama unavyotaka kumaanisha wewe.

Mfano 1)Mimi ninasoma.Sisi tunasoma.
2)Mimi ninaimba. Sisi tunaimba.

3)Huku niendako. Huku tuendako.✅

Huku twendako❎
 
Matumizi sahihi ya Lugha yanaongeza vipi kipato cha mtu mmoja mmoja
Pengine yanatambulisha uwezo wa mtu mmoja mmoja katika kuongeza kipato chake mwenyewe.

Kuna vipato vinaanzia kwenye maandiko na vingine vinaongezeka kupitia maandiko.

Kujua/kutojua kuandika ni tofauti kabisa na kukosea sarufi na uandishi wenyewe kiujumla!

Muandishi wa habari kwa taaluma, akisema, "Televisheni inaonyesha", na mimi nikasema "Televisheni inaonesha", makosa ni nini hapo?
 
Kuna awamu kila aliyefeli alienda kusomea ualimu hapo matokeo yake ndo haya
 
Back
Top Bottom