Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Mimi mwenyewe naona limekuwa tatizo kubwa sana..

Ntaanza kukurekebisha wewe kwanza

Utapia ujinga -Ninaamini kabisa lengo lako lilikuwa kuandika watu waliozidi ujinga yaani utapia akili..
utapia maana yake ni ukosefu wa ubora wa kitu kwa mfano utapia mlo ni ukosefu wa mlo bora ..
Hivyo basi ukisema utapia ujinga maana yake ni ukosefu wa ujinga maana mtu huyo atakuwa na akili sana

Nyakati za sasa tumia tu neno wakati wa sasa nyakati huweza kumaanisha miaka mingi sana kama generation au enzi kwa english tungesema (era) na kwa maelezo yako umesema shida imeanza siku za hivi karibuni kwa hiyo neno zuri ni wakati wa sasa

Naogopa sana tuko-
Nina hakika ulitaka kusema huko...

Hoja yako!


Swala la kwanza
hoja yako ina mashiko na Pana sana ila ilipaswa kuangalia Swala moja kubwa ambalo ni swala la lahaja..

Tanganyika na nchi ya East Africa (Kipindi cha ukoloni) kwa pamoja ilipata azimio na Kwa pamoja Walikubaliana kutumia Lahaja ya Kiunguja kama lahaja ya kiswahili Sanifu...

Lakini hii haikuwa kifo cha lahaja zingine kama kihadimu(Kimakunduchi) , kimrina (Inayopatikana pangani), kimgao,kipate ,kingozi kibajuni,kipemba,kivumba (Tanga) ,kimtangang'ata (Tanga) ,Kingazija na etc..

Ambazo nazo kwa ongezeko la watu hao zinakua kwa kasi hivyo kudhibiti matumizi ya lahaja zingine inabidi liwekwe azimio jingine la chaguzi ya lahaja kimaandishi na kimisemo...

Swala la pili

kiufupi ni kwamba kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake na wote wakawa sawa ni Vyema aongozwe na wale Wanaoweza kuona...

Miongoni mwa lahja mbovu kimaumbo na kimatamshi zinatoka Tanzania Bara..

Huku lahaja bora zikitoka pwani na Visiwani kwa mujibu huo ni wazi sasa Sifa mojawapo ya walimu kufundisha kiswahili isiwe ufaulu wa kukariri ila iwe ni Mmoja atokaye katika moja ya lahaja bora ikiwemo Kiunguja na kimakunduchi ili kuokoa taifa hili...
Maana yake Wale wote wenye lahaja hizi wahimizwe kufundisha kiswahili kuliko Kumkuta mwalimu wa kiswahili ni Msukuma au Mkurwa lazma kiswahili cha wanafunzi kiharibike ...

Asanteni
O Level mwlimu wangu wa kiswahili alikua Mhaya... actual wacha nizienderee zanna..!!
 
Soma hapa tena na tena.

" mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc."
 
Watoto wengi siku hizi kuandika kwa usahihi ni janga kubwa, inafika muda unajiuliza huko shuleni wanasoma nini?

Ukipita Facebook watu hawawezi kutofautisha hakuna na akuna, hela na ela na vingine vingi. Kuna muda huwa naona labda mimi nazeeka ndiyo maana nacomplicate mambo!
 
Nimeshangaa walimu nao wanaandika
  1. Alima wakimaanisha Halima
  2. Muagama wakimaanisha Mhagama
  3. Asumani wakimaanisha Athuman
  4. Mwanaamis wakimaanisha Mwanahamisi
  5. Alamisi wakimaanisha Alhamisi
  6. Maali wakimaanisha Mahali
  7. Maharifa wakimaanisha Maarifa
  8. Maangahiko wakimaanisha Mahangaiko
  9. Nisamee wakimaanisha Nisamehe
IMG_20231021_183704.JPG
 
Darasa la saba ukimaliza unajua kuandika vizuri lugha ya kiswahili, tatizo ni watu kujiendekeza
 
Watoto wengi siku hizi kuandika kwa usahihi ni janga kubwa, inafika muda unajiuliza huko shuleni wanasoma nini?

Ukipita Facebook watu hawawezi kutofautisha hakuna na akuna, hela na ela na vingine vingi. Kuna muda huwa naona labda mimi nazeeka ndiyo maana nacomplicate mambo!
Tatizo kuna maneno mengi sana ambayo watanzania hawajawahi kuyaona kwa ufasaha wake yakiandikwa.

INakuwa ni ngumu sana kujua usahihi wa neno ambalo haujawahi kuliona likiandikwa na hiyo inapelekea shida hata kwenye kulitamka.

Njia bora ya kuwa fasaha katika uandishi ni kusoma sana makala na maandiko mbalimbali,hiyo itamfanya mtu kujua maneno namna yanavyoandikwa kwa usahihi.

Watanzania sisi sio wapenzi wa kusoma bali ni wapenzi wa kuangalia na kusikiliza,na katika kusikiliza hauwezi kupata usahihi wa maneno kwa sababu haujui yanatamkwa vipi.
 
Unasikia ati:
"Analia machozi" badala ya "Analia" au "Amalia na kutoa machozi"
"Amefariki dunia" badala ya "Amefariki" au "Ameaga dunia"
Kuchanganya au kutumia vibaya maneno.
"Sio" panapostahili kutumia"Siyo"
"Ndio" panapostahili kutumia"Ndiyo".
Hawa "Mbashara" wengine " Mubashara".
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Kuna akina xaxa naenda xokoni na jomoni xitaki.
Yaani utopolo tu.
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Kama mtu anaandika xaxa badala ya sasa cna badala ya sina halafu ukimuangalia ni mtu mzima na ni kiongozi wa taasisi kwa kweli hali ni mbaya mkuu mabadiliko ya haraka yanahitajika
 
Ni kweli hali ni tete.Majina ya watu,miji nk siku hizi yanaanza kwa herufi ndogo.Huo muandiko ndo usiseme,"S" inakatwa na mstari katikati ndo inakuwa nane,"f" inachorwa kama mswaki.Nafikiri wale walimu waliotufundisha kuumba herufi huku wakitushika mkono walipostaafu kilikuja kizazi cha .com ikawa ndo mwisho wa kuumba herufi.Na vile vidaftari vyenye mistari mikubwa na midogo vya kujifunzia miandiko sijui kama bado vipo.
 
Back
Top Bottom