Kuna baadhi ya Vijana wa Chuo ni wajinga sana

Ingawa vijana wa vyuo wana ujinga wao lakini nadhani kwa ulimwengu tulionao ulitumia mbinu zinazofanana na matapeli.......

Imagine mtu anakujia na kibegi mgongoni anataka maongezi na wewe hali ya kuwa humjui na upo kwenye ratiba zako.......
Msikilize mtu. That is the first rule.
 
Mimi hapa ninauhitaji wa laptop☝️😲 nipo Mtwara. ukiguswa kwa hiari.
 
Mhh vitu vya bure tena kuwapa wanaume 😂😂😂lazima aogope, wadada wengi si tamaa mbele hawez kunyali wala.
 
Kuna rafiki yangu mmoja ambaye si Mtanzania anaishi Marekani, Boston state!

Huyu jamaa kiasili ni Msweden ambaye anaishi huko Kwa Joe Biden, mimi na yeye urafiki wetu ulianza miaka mingi kidogo baada ya kukutana mkoani Arusha kwenye ishu moja hivi, kuanzia hapo tukawa kama ndugu!.

Sikutaka kabisa kushea hii ishu lakini kuna mdau mmoja nimekutana naye akanieleza habari za vijana ambao wako vyuoni na kile alichotaka kufanya ni kama amekatishwa tamaa na muitikio, mind u, hiyo ishu ingewanufaisha wanafunzi wenyewe lakini ni kama alikuwa anapigia mbuzi gitaa!

Ok kinaona nami niandike huu uzi uenda Vijana mlioko vyuoni mtabadilika kwasababu mnakosa fursa na bahati na mkimaliza vyuo mnaanza kupigia watu kelele!

Mwaka jana mwezi wa 4 huyo rafiki yangu Msweden aishie Marekani tuliwasiliana nae na akanitaka na kuniomba ya kwamba kuna lap top aina ya Mac book ziko 20 mpya kabisa ambazo anatarajia kunitumia,na atakapozituma nitafute wanafunzi wa vyuo ambao wako na changamoto za lap top niwagawie ili niwasaidie katika masomo yao!.

Hii ishu tulikuwaga tukiongea ananiambia kwasababu wakati yuko Arusha alipokuwa akitembelea vyuoni anaona namna wanafunzi wanavyopata taabu,hivyo akanitaka zitakapofika nihakikishe zinawafikia walengwa na kila nitakayekuwa nampatia nihakikishe nampigia Via WhatsApp wanawasiliana ili kumu-encourage,siyo hivyo tu bali alituma na kiasi cha fedha ambacho alitaka kila mwanafunzi kwenye hao wanafunzi 20 niwagawie $500 kila mtu!.

Ok,baada ya mzigo kufika na kuupokea nikaona ni vyema nianze na vyuo vya jiji la Dar es salaam kwakuwa ndipo nilipo ili baadae kwakuwa project ni endelevu nitaelekea mikoani huko pia!.

Chuo cha kwanza kwenda ilikuwa ni UDSM,Niliondoka na gari yangu nikaenda kuipaki pale mawasiliano,sikutaka kwenda na gari pale Udsm kwasababu nilizozijua mimi,hivyo nikachukua Laptop 4 nikaziweka kwenye Begi la mgongoni kisha nikaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea huko!

Ilikuwa mida ya saa 6 mchana,wakati naingia pale Udsm kuna wanafunzi kadhaa nilikutana nao lakini kila nikijaribu kuwasimamisha walinikaushia huku wengine wakisogeza Earphone zao vizuri ili waendelee kula ngoma za Kiba na Mondi fresh!.

Nikaona siyo kesi,nikaendelea kupandisha juu ili ikiwezekana nizigawe na kuondoka,na sikutaka kuzigawa kama pipi, nilitaka kwanza tupige stori mbili tatu ili nifahamu kabisa niliyeongea naye anaouhitaji huo!

Kuna mademu ambao nilikuwa nikiwaangalia naona kabisa hata chai yawezekana hawajanywa lakini ukiwasimamisha wanajifanya kunataka huku hata kukuangalia hawakuangalii!.

Nilifika hadi uelekeo wa ile Maktaba mpya nikakutana na sister mmoja ambaye umri wake ulikuwa umeenda kidogo,nikamsimamisha nikamuomba aniazime muda na akakubali,hivyo nikaanza kumuhoji na kiukweli alikuwa na uhitaji huo,ikabidi nichomoe laptop nikampatia na nikamkabidhi na ile $500, aisee yule sister alidhani natania maana aliruka kwa furaha mnoo!, baada ya hapo wakazingumza na mshikaji akamshukuru sana!

Nikaelekea kwenye vile vizimba vya kujisomea,nikakuta wanafunzi 4,jamaa 2 na mademu 2 ila baada ya kuwasalimia na kuomba niongee na mmoja nikaona wenzie wanaondoka wakamwambia atawakuta stendi wanamsubiri ili waondoke,jamaa naye nikaona mawazo yako kwa yule demu mwingine akaniambia Bro nina haraka utanisamehe!,Ok nikaona isiwe kesi,nikaondoka zangu kutafuta wengine!.

Zile lap top pale mlimani zote nilizigawa kwa wanafunzi wa kike kwasababu wanaume wote kila nikitaka kuzungumza nao wanajifanya wanaweka Earphone masikioni!.

Baada ya hapo nilielekea vyuo vingine pia!.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba,Wanafunzi wa vyuo wengi ni wajinga na malimbukeni for nothing!.

Wengi wanajiona wajanja kumbe ni wajinga tu,hata sisi vyuo tumesoma na hatukuwahi kuwa na ulimbukeni huo wa kijinga!.Badilikeni

Baada ya hilo tukio nasikia wameanza kufunguka masikio na wananisubiri sana,kuna wengine wananipigia simu sana nadhani namba walipewa na hao waliopata hiyo bahati,naishia tu kuwaambia labda siku nyingine maana ni zamu ya wanafunzi wa mikoani!.

Wanafunzi wa vyuo badilikeni,unaposoma huwa ni kuondoa ujinga kichwani na kuwa na maarifa mapya,lakini baadhi yenu mnakuwa wajinga kwa kunata kiasi kwamba utadhani ni wewe tu ndiyo mwenye degree hapa duaniani!.
Niliwahi kuandika uzi wenye kuonesha ni kwa namna gani vijana skuizi tuna ujuaji wa kijinga.

Nashukuru sana scenario imeprove andiko langu.
Nashukuru pia kwakua nimejifunza kitu pia[emoji120]
 
Wazo langu:

Wameathiriwa na pranksters (hiddenen cameras) wasamehe sana .

(Kwa lugha rahisi.)
Kwasasa ukiwaaproach kwa njia hiyo wanaogopa kuonekana wakitrend youtube.
 
Kuna shida sana kwenye communication skills ya jamii yetu sio tu kwa wanachuo, hata wadada tu mtaani ukitaka mazungumzo nae njian mostly wanaanzaga na nyodo.

Kuna siku nilikua nimepita chuo cha kcmc, nilikua nataka kujua location ya ATM ya NMB kwa maeneo yalo, Haloo nikisimamisha wadada wa3 walio kua wakipita pale wote hawakua positive kutaka kuongea na mm, mpaka nika ghairi hilo zoezi.

Ni kama tunawaza ngono ngono tu, kwamba ukisimamishwa tu mtongozo unafuata, na hata kama ni hivyo huwezi kusema una mume/boyfriend?

Ni vyema watu tukabadili mtizamo, we need to socialize ety
 
Well said mkuu, tabia hii wanayo haswa wanawake. Unaweza kumsimamisha mwanamke mtaani kutaka kumuuliza kitu, cha kwanza anaanza kukutajia shida zake, hapo bado hujaanza kumwambia kile unachotaka kumuuliza. Yaani wanaboa kishenzi. Ndiyo maana kama nataka uliża mtu directions natafuta mwanamme mwenzangu.
 
Ungetengeneza shindano Moja zuri Kisha mshindi akapata hiyo laptop kigezo Cha kwanza ni asiwe na laptop na awe anatokea mazingira magumu kidogo nadhani hata huyo mfadhiri angeona umefanya vema we ukaleta mambo ya tik tok haya bhna
 
Ungeenda kwa Dean ,yy angekupa maelekezo na list ya wanachuo wahitaji
 
Asilimia kubwa ya wahitimu wa vyuo hapa Tanzania bado wapumbavu na wana mambo ya kijinga sana. Usishangae muhitimu wa chuo kikuu hapa Tanzania kuwa na brain capacity ya mwanafunzi wa darasa la 5.
 
Uwongo mwingine wa ajabu sana.
Kwanza hakuna Mswede akupe laptop Apple 20 bure na dola juu ukagawe hamna.
Na kama ungepewa we ungekua mtu wa kwanza kuiba.
We sema umetaka kuwapa makavu wanachuo kwa njia hiyo.
 
Back
Top Bottom