Kuna baadhi ya Vijana wa Chuo ni wajinga sana

Kuna baadhi ya Vijana wa Chuo ni wajinga sana

Kumbe ni miradi😆😆 bas sawa ndugu
Ni msaada maalumu kwa ajili ya wanafunzi,wewe pambana na umasikini wako mkuu!

Au endelea kubeti ipo siku utatoboa kwa kujifariji!
 
Kuna rafiki yangu mmoja ambaye si Mtanzania anaishi Marekani, Boston state!

Huyu jamaa kiasili ni Msweden ambaye anaishi huko Kwa Joe Biden, mimi na yeye urafiki wetu ulianza miaka mingi kidogo baada ya kukutana mkoani Arusha kwenye ishu moja hivi, kuanzia hapo tukawa kama ndugu!.

Sikutaka kabisa kushea hii ishu lakini kuna mdau mmoja nimekutana naye akanieleza habari za vijana ambao wako vyuoni na kile alichotaka kufanya ni kama amekatishwa tamaa na muitikio, mind u, hiyo ishu ingewanufaisha wanafunzi wenyewe lakini ni kama alikuwa anapigia mbuzi gitaa!

Ok kinaona nami niandike huu uzi uenda Vijana mlioko vyuoni mtabadilika kwasababu mnakosa fursa na bahati na mkimaliza vyuo mnaanza kupigia watu kelele!

Mwaka jana mwezi wa 4 huyo rafiki yangu Msweden aishie Marekani tuliwasiliana nae na akanitaka na kuniomba ya kwamba kuna lap top aina ya Mac book ziko 20 mpya kabisa ambazo anatarajia kunitumia,na atakapozituma nitafute wanafunzi wa vyuo ambao wako na changamoto za lap top niwagawie ili niwasaidie katika masomo yao!.

Hii ishu tulikuwaga tukiongea ananiambia kwasababu wakati yuko Arusha alipokuwa akitembelea vyuoni anaona namna wanafunzi wanavyopata taabu,hivyo akanitaka zitakapofika nihakikishe zinawafikia walengwa na kila nitakayekuwa nampatia nihakikishe nampigia Via WhatsApp wanawasiliana ili kumu-encourage,siyo hivyo tu bali alituma na kiasi cha fedha ambacho alitaka kila mwanafunzi kwenye hao wanafunzi 20 niwagawie $500 kila mtu!.

Ok,baada ya mzigo kufika na kuupokea nikaona ni vyema nianze na vyuo vya jiji la Dar es salaam kwakuwa ndipo nilipo ili baadae kwakuwa project ni endelevu nitaelekea mikoani huko pia!.

Chuo cha kwanza kwenda ilikuwa ni UDSM,Niliondoka na gari yangu nikaenda kuipaki pale mawasiliano,sikutaka kwenda na gari pale Udsm kwasababu nilizozijua mimi,hivyo nikachukua Laptop 4 nikaziweka kwenye Begi la mgongoni kisha nikaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea huko!

Ilikuwa mida ya saa 6 mchana,wakati naingia pale Udsm kuna wanafunzi kadhaa nilikutana nao lakini kila nikijaribu kuwasimamisha walinikaushia huku wengine wakisogeza Earphone zao vizuri ili waendelee kula ngoma za Kiba na Mondi fresh!.

Nikaona siyo kesi,nikaendelea kupandisha juu ili ikiwezekana nizigawe na kuondoka,na sikutaka kuzigawa kama pipi, nilitaka kwanza tupige stori mbili tatu ili nifahamu kabisa niliyeongea naye anaouhitaji huo!

Kuna mademu ambao nilikuwa nikiwaangalia naona kabisa hata chai yawezekana hawajanywa lakini ukiwasimamisha wanajifanya kunataka huku hata kukuangalia hawakuangalii!.

Nilifika hadi uelekeo wa ile Maktaba mpya nikakutana na sister mmoja ambaye umri wake ulikuwa umeenda kidogo,nikamsimamisha nikamuomba aniazime muda na akakubali,hivyo nikaanza kumuhoji na kiukweli alikuwa na uhitaji huo,ikabidi nichomoe laptop nikampatia na nikamkabidhi na ile $500, aisee yule sister alidhani natania maana aliruka kwa furaha mnoo!, baada ya hapo wakazingumza na mshikaji akamshukuru sana!

Nikaelekea kwenye vile vizimba vya kujisomea,nikakuta wanafunzi 4,jamaa 2 na mademu 2 ila baada ya kuwasalimia na kuomba niongee na mmoja nikaona wenzie wanaondoka wakamwambia atawakuta stendi wanamsubiri ili waondoke,jamaa naye nikaona mawazo yako kwa yule demu mwingine akaniambia Bro nina haraka utanisamehe!,Ok nikaona isiwe kesi,nikaondoka zangu kutafuta wengine!.

Zile lap top pale mlimani zote nilizigawa kwa wanafunzi wa kike kwasababu wanaume wote kila nikitaka kuzungumza nao wanajifanya wanaweka Earphone masikioni!.

Baada ya hapo nilielekea vyuo vingine pia!.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba,Wanafunzi wa vyuo wengi ni wajinga na malimbukeni for nothing!.

Wengi wanajiona wajanja kumbe ni wajinga tu,hata sisi vyuo tumesoma na hatukuwahi kuwa na ulimbukeni huo wa kijinga!.Badilikeni

Baada ya hilo tukio nasikia wameanza kufunguka masikio na wananisubiri sana,kuna wengine wananipigia simu sana nadhani namba walipewa na hao waliopata hiyo bahati,naishia tu kuwaambia labda siku nyingine maana ni zamu ya wanafunzi wa mikoani!.

Wanafunzi wa vyuo badilikeni,unaposoma huwa ni kuondoa ujinga kichwani na kuwa na maarifa mapya,lakini baadhi yenu mnakuwa wajinga kwa kunata kiasi kwamba utadhani ni wewe tu ndiyo mwenye degree hapa duaniani!.
Marekani yote HAKUNA State inayoitwa Boston
 
1. Vile haviitwi vizimba, vinaitwa vimbweta.

2. Wanafunzi wa UDSM hawajapauka, hata mtu awe na shida kuna mazingira mazuri ya kuishi nazo.

3. Kwa matukio ya utapeli yaliyowahi kutokea, wewe ni mtu ambaye hukutakiwa kuaminiwa kwa namna yoyote ile. Tena watu kama nyinyi huwa mnatolewa mfano kabisa wakati wa orientation.
 
1. Vile haviitwi vizimba, vinaitwa vimbweta.

2. Wanafunzi wa UDSM hawajapauka, hata mtu awe na shida kuna mazingira mazuri ya kuishi nazo.

3. Kwa matukio ya utapeli yaliyowahi kutokea, wewe ni mtu ambaye hukutakiwa kuaminiwa kwa namna yoyote ile. Tena watu kama nyinyi huwa mnatolewa mfano kabisa wakati wa orientation.
Kama ulitapeliwa na elimu yako,basi wewe ni ZEZETA LA KIMATAIFA
 
Mkuu mimi ninaona njia uliyotumia haikua sahihi sana hasa ulimwengu wa sasa ambao uaminifu umekua jambo gumu kidogo

Ungetafuta uongozi wa chuo mfano dean of students au serikali ya wanafunzi wao wanawafahamu baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji mkubwa wa fedha na hizo laptop labda hawana mikopo na wenda wametoka familia ambazo kikawaida zinashindwa kuwatimizia mahitaji kama hayo

Ungeomba uongozi ukukutanishe na hao wanafunzi kisha uzungumze nao, binafsi naona kazi yako ingekua nyepesi na ungefikia kundi husika la wahitaji ambayo ndio target kubwa ya huyo mtoa msaada

Kwa njia uliyotumia ni wazi kwamba kuna watu walinufaika na huo msaada wakati kimsingi sio walengwa wakuu

Kingine hizo dola 500 ungemshauri mtoa msaada azielekeze kuwalipia ada baadhi ya wanafunzi ambao wanakwama kabisa kulipa ada na wenda kusitisha masomo kwaiyo hapo kungekua na wanufaika wa hizo laptop na wanufaika wa ada (baada ya kujihakikishia kwamba ni wahitaji ungewaomba control namba zao kisha ungewalipia na kuwakabidhi pay in slip)

Maoni yangu ni hayo mkuu kama nimeongea kinyume na mapenzi yako basi unisamehe.
 
Japo kuna risk ya kusimamishwa na tapeli ila ni kua tu makini
😅😅😅Mkuu tapeli utamjua kwenye maneno yake..

All in all,

Tujifunze kua genuine and humble hivi vitu viwili vina lipa Sanaa..
 
Back
Top Bottom