Kuna baadhi ya watu bado hawajamuelewa Rais Magufuli!

Kuna baadhi ya watu bado hawajamuelewa Rais Magufuli!

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Wale baadhi ya watu ambao bado wanaojaribu kumtingisha Rais Magufuli wakidhani atabadilisha njia anayotumia katika utendaji kazi wake wananishangaza sana!

Wanaojaribu kumtingisha inawezekana hawamfahamu vizuri au wanamfahamu vizuri lakini wamejivika upumbavu!

Kwa wale wanamfahamu vizuri, siku alipotoa hii hotuba walijua vizuri nini kitafuata na nini cha kufanya!

Ukitaka kuisikia na kuisoma hotuba, GONGA HII LINK>>Magufuli: Tupo imara, atakayejaribu kutuyumbisha tutambomoa.

Baada ya Freeman Mbowe kutangaza oparesheni UKUTA mwezi Julai 2016, watu kama Edward Lowassa wanaomfahamu vizuri Rais Magufuli waliwashauri CHADEMA waachane na uamuzi huo.

Kuna baadhi ya watu kama Nape Nnauye walijaribu kumtingisha wakidhani atabadilika lakini baadaye wakashauriwa/wakajua habadilishi misimamo yake na wakaamua kufanya kile ambacho Waingereza kwenye methali hukisema, ‘’if you can’t beat them, join them’’.

Baadhi ya wale wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ambao hawakubaliani na kile anachokifanya wameamua kujiunga naye au kukaa kimya kwa sababu wanajua hata wakipiga kelele hawawezi kumbadilisha katika misimamo yake.

Mwandishi mmoja wa Gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo aliwahi kuandika wakati wa Utawala wa Rais Kikwete, ‘’John Pombe Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache katika Serikali ya Kikwete wanaochapa kazi. Yeye sheria ikishapitishwa husimama kidete kuitekeleza hadi nukta ya mwisho hata kama athari zake ni kubwa! Tena ataisimamia kwa ukali na vitisho’’.

Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.

Nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi pia kugusia kuhusu msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake wakati akichangia kwenye bajeti kuu mwezi Juni 2019 ambapo alisema;
"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la KUTOKUWA NA MSIMAMO kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali''.

Zitto aliendelea kusema, "Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita".
LINK>>Zitto Kabwe aipongeza Serikali kwa hili

Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu, Kiranga na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
 
Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!
Duh!. Huu sasa unataka kutuletea ukabila. Kama tumeelezwa rais Magufuli ni Msukuma, kitendo cha kusema kuwa Rais Magufuli ni kweli sio Msukuma, ni uchochezi. Ili huu usiwe uchochezi unaweza kuuweka wazi huo ukweli wako?

P
 
Mkuu;
Mlivyoelezwa kuwa ni Msukuma, waliowaeleza waliweka wazi huo ukweli? Kama hawakuweka wazi, kwa nini unataka mimi niweke wazi?
 
Atadhibitiwa tu!! Tunza hii comment kwenye faili la ubongo wako Tanzania ni zaidi ya uijuavyo Tanzania ni zaidi ya Magufuli.

Tulimpeleka Magufuli Ikulu ili apambane na ufisadi sio kukimbizana na wakina Mbowe matokeo yake anasamehe wezi na pesa wanazolipa hatujui zinaenda wapi amekuwa mpora nchi na mtu asiyefata haki za binadamu yeye ataondoka tu na Tanzania itabaki.
 
Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

[/QUOTE]
umeongea kwa uhakika kabisa kwamba si msukuma mimi nilidhani alieanzisha hizi habari hizi alikuwa analenga kupunguza uungaji mkono wa wasukuma kwa magufuli kuwa si mwenzao sababu ya kufikiri hivi ni kuwa magufuli hakujiita msukuma kwa vile alikuwa maeteuliwa kugombea urais najua ni msukuma miaka yote tangu tangu akiwa mkemia wa chama cha ushirika cha Nyanza wala hakuwa anajua kuwa sikumoja atakuwa Rais ,unaweza nisahihisha kwa hilo
 
Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu, [B]Kiranga[/B] na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
unajua kwenye kuongelea issue ambayo tuna-assume unaielewa alafu sisi tusiolewa tukaona unakosea pale tunapoelewa basi the all argument is null and void...
 
Atadhibitiwa tu!! Tunza hii comment kwenye faili la ubongo wako Tanzania ni zaidi ya uijuavyo Tanzania ni zaidi ya Magufuli.
Mkuu;
Nadhani saver za Jamiiforums zitaitunza comment yako!

Ni kweli Tanzania ni zaidi ya niijuavyo lakini nikiangalia kalenda inasomeka ni miaka minne tangu aingie Ikulu kama Rais wa Tanzania!
 
Mkuu;
Mlivyoelezwa kuwa ni Msukuma, waliowaeleza waliweka wazi huo ukweli? Kama hawakuweka wazi, kwa nini unataka mimi niweke wazi?

Ni kweli ana msimamo na chuki ya wazi dhidi ya wapinzani na waislamu. Baadhi ya misimamo yake ni kuhakikisha anaua vyama vya upinzani kwa kutumia madaraka yake. Pia kwenye utawala wake waisilamu wana nafasi finyu. Angalia msimamo wake dhidi Assad muisilamu muadilifu mwenye msimamo katika usimamizi wa fedha za umma. Ameamua kumtoa mbali ya uadilifu wake, ameona bora ampe mkristo mzembe kwani kwake uislamu ni nongwa hasa ukiwa na msimamo, na weledi katika kazi. Misimamo hii iko wazi dhidi ya wapinzani na waisilamu, je katika mazingira hayo tutegemee Tanzania salama? Muda utaamua.
 
umeongea kwa uhakika kabisa kwamba si msukuma mimi nilidhani alieanzisha hizi habari hizi alikuwa analenga kupunguza uungaji mkono wa wasukuma kwa magufuli kuwa si mwenzao sababu ya kufikiri hivi ni kuwa magufuli hakujiita msukuma kwa vile alikuwa maeteuliwa kugombea urais najua ni msukuma miaka yote tangu tangu akiwa mkemia wa chama cha ushirika cha Nyanza wala hakuwa anajua kuwa sikumoja atakuwa Rais ,unaweza nisahihisha kwa hilo
Mkuu;
Hoja yako inakosa nguvu za hoja kwa sababu hatuchagui viongozi kwa misingi ya kabila!

Huo uungwaji wa mkono kwa msingi wa kabila uliuona wapi na kwa utafiti gani unaokidhi viwango vya kimataifa? Naomba unielimishe!
 
unajua kwenye kuongelea issue ambayo tuna-assume unaielewa alafu sisi tusiolewa tukaona unakosea pale tunapoelewa basi the all argument is null and void...
Kieleze kile ambacho kinafanya argument yangu iwe null and void!
 
Kieleze kile ambacho kinafanya argument yangu iwe null and void!
Umefanya research kabla ya kuleta huu uzi ? kumbuka mimi sijui hayo usemayo kama ni kweli au uongo ila kuna kitu/vitu ulivyoweka vina makosa.., sasa kama umeweza kukosea hapo kwanini usikosee pengine..., hence umuhimu wa kuandika unachokielewa / una uhakika nacho no matter how minor.... Kiranga
 
Ni kweli ana msimamo na chuki ya wazi dhidi ya wapinzani na waislamu. Baadhi ya misimamo yake ni kuhakikisha anaua vyama vya upinzani kwa kutumia madaraka yake. Pia kwenye utawala wake waisilamu wana nafasi finyu. Angalia msimamo wake dhidi Assad muisilamu muadilifu mwenye msimamo katika usimamizi wa fedha za umma. Ameamua kumtoa mbali ya uadilifu wake, ameona bora ampe mkristo mzembe kwani kwake uislamu ni nongwa hasa ukiwa na msimamo, na weledi katika kazi. Misimamo hii iko wazi dhidi ya wapinzani na waisilamu, je katika mazingira hayo tutegemee Tanzania salama? Muda utaamua.
Mkuu;
Unajaribu kuniondoa kwenye msingi wa mada yangu tuanze kujadili suala ambalo linahitimishwa na hisia zako.

Samahani siwezi kujadili hisia zako kwa sababu hisia unazijua mwenyewe!
 
Ni kweli ana msimamo na chuki ya wazi dhidi ya wapinzani na waislamu. Baadhi ya misimamo yake ni kuhakikisha anaua vyama vya upinzani kwa kutumia madaraka yake. Pia kwenye utawala wake waisilamu wana nafasi finyu. Angalia msimamo wake dhidi Assad muisilamu muadilifu mwenye msimamo katika usimamizi wa fedha za umma. Ameamua kumtoa mbali ya uadilifu wake, ameona bora ampe mkristo mzembe kwani kwake uislamu ni nongwa hasa ukiwa na msimamo, na weledi katika kazi. Misimamo hii iko wazi dhidi ya wapinzani na waisilamu, je katika mazingira hayo tutegemee Tanzania salama? Muda utaamua.
Mbona kawatumbua na wakristu..acha lawama za kidini

Waislam wengine ni WAJINGA KILA SITU MNAHISI MNAONEWA

ASSAD KAMTUMBUA SIO KWASABABU NI MUISLAM
 
Back
Top Bottom