Kuna baadhi ya watu bado hawajamuelewa Rais Magufuli!

Kuna baadhi ya watu bado hawajamuelewa Rais Magufuli!

Angalia figisu figisu zinazoendelea kwenye uchaguzi mdogo hapa nchini kila mtendaji amekuwa muoga kumpitisha mgombea wa upinzani.AMKA
Ninakubaliana na angalizo lako kuhusu watendaji!

Mimi sijalala na huhitaji kuniambia NIAMKE!
 
Duh!. Huu sasa unataka kutuletea ukabila. Kama tumeelezwa rais Magufuli ni Msukuma, kitendo cha kusema kuwa Rais Magufuli ni kweli sio Msukuma, ni uchochezi. Ili huu usiwe uchochezi unaweza kuuweka wazi huo ukweli wako?

P

..natofautiana na mchango wako ktk kumuelezea Jpm.

..binafsi siamini kama ni mtu mwenye msimamo sasa hivi akiwa ni mkuu wa nchi, na hata kabla ya hapo.

..ili useme mtu au kiongozi fulani ana msimamo, ni lazima uangalie msimamo huo ni dhidi ya nani na nini, na risk anayochukua.

..binafsi mtu mwenye msimamo ni yule anayeweza "kumdidindia" mtu mwingine aliyemzidi nguvu au waliyelingana kiuwezo / kimabavu.

..kwa mfano, Je, kuna jambo lolote ambalo Jpm alilitetea akiwa waziri ambalo lilikuwa against wakubwa wake au chama chake? did he ever put his job /position / life on the line for something that he believed in?

..wako Mawaziri kama Mzee Edwin Mtei ambao walisimamia walichokiamini mpaka kufikia kujiuzulu nafasi zao. Kwangu mimi hicho ni kipimo cha msimamo. Kwanza Mtei alisimama kidete dhidi ya bosi wake. Na alipoona hasikilizwi aliamua kujiuzulu.

..Mwingine ninayeweza kumkumbuka hapa ni Hamad Rashid Mohamed. Huyu alipinga uonevu dhidi ya reformers ndani ya CCM. Ilifika wakati akaitwa na wakubwa wake wakimsihi achague nafasi yoyote anayoitaka ili aachane na msimamo wake. Hamad Rashid alikataa na matokeo yake akafukuzwa ktk chama na kupoteza nafasi zote za uongozi.

..Yuko waziri mwingine sitamtaja jina kwa leo. Lakini ilikuwa ni wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi. Waziri huyo aliweka msimamo kwamba kama mapendekezo yake hayatakubaliwa basi alikuwa radhi kujiuzulu. Mzee Mwinyi alikubaliana na mapendekezo ya waziri huyo na akaendelea na majukumu yake.

..Kwa upande wangu sina kumbukumbu ya Jpm kutetea suala lolote lile akiwa waziri, sanasana namkumbuka kama Waziri aliyekuwa kinara wa kumpa sifa za kupitiliza bosi wake Raisi Kikwete.

..Tukija kwa Jpm tangu awe Raisi, sidhani kama anastahili sifa ya kuwa kiongozi mwenye msimamo. Wapinzani anaokinzana nao kimawazo au kimtizamo hawana madhara yoyote kwake. Bunge ambalo lina mamlaka ya kumsimamia na kumdhibiti limesheni ushabiki wa chama tawala na Jpm ndiye mwenyekiti wa chama hicho. Kwa msingi hakuna wa kumtisha Jpm ktk maamuzi yake.

..Jpm alikuwa na nafasi ya kujipambanua kama Raisi mwenye msimamo wakati alipochukua uamuzi wa kutosomesha watoto wanaopata ujauzito. WB walipomtishia kumnyima fedha Jpm na serikali yake wakaachana na msimamo huo. Mwalimu Nyerere amewahi kukataa misaada akitetea yale aliyoyaamini.

..Pia kuna suala la mgogoro dhidi ya kampuni ya Accacia / Barrick. Jpm aliutangazia ulimwengu kuwa tunaibiwa na tunaidai Accacia usd 191 billion. Baada ya mabosi wa Accacia / Barrick kuja nchini Jpm akaachana na madai hayo na kuishia kukubali usd 300 million. Kwangu mimi huyo ni kiongozi kigeugeu asiyekuwa na msimamo.

..Kwa maoni yangu Jpm ni kiongozi anayetegemea mabavu ya vyombo vya dola. Wapinzani wangekuwa na wabunge wa kutosha sidhani kama Jpm angekuwa na kiburi cha kuwadhalilisha kama anavyofanya sasa hivi.

..Hiki tunachodhani ni msimamo au ukali infact kinaweza kuwa ni uoga au "inferiority complex" iliyojificha. Kwasababu hana uwezo wa kujenga hoja basi anachofanya ni kutumia vyombo kuwatisha na kuwadhalilisha wale ambao hawezi kushindana nao kwa hoja.

cc tindo, Pascal Mayalla
 
Siku zinavyozidi kusonga mbele ubongo wako unazidi kusinyaa. Jiangalie usijeokota makopo. Sasa udini unautoa wapi? Na unakusaidia Nini?

Ni hivi, habari ndio hiyo.
 
Boss Kalamu1 Boss wewe ndio mnafiki mwenyewe ninaowazungumzia, kichwani ni kusifia na kupamba tu bila HOJA.
Nionyeshe wapi nimekutaja mwanzo kabla ya hii msg??? !!! Mimi hata ukinidharau, unanilisha??? Unanijua??? Dua la Mwewe hilo ... Unajiita Kalamu hata Uandishi wenyewe ... haujui.

Nakushauri jikite kwenye Mada na lete HOJA zenye maana, unalishushia na mnalishushia hadhi Jukwaa.
Naona ujumbe umefika na kueleweka.
Basi tulia. usiwe unaparamia tu kujibishana na watu bila ya kujua misimamo yao ni ipi. Ungetumia muda kidogo tu kuangalia ninayoyaamini mimi na kuyaandika humu JF usingethubutu kuandika uliyoandika kunijibu hapa.
Boss @Kalamu1 Tatizo lenu ndio hilo, mshanyweshwa maji ya Bendera, Jambo gani nimepindisha hapo??? Mimi sina Dhiki na Shida hiyo, Njano naiita Njano, Nyekundu naiita Nyekundu.
Nakudharau kwa maandishi yako ya kipuuzi humu. Maandishi yako yote niliyoyasoma kwenye mada hii yanaonyesha wazi kuwa hustahiri heshima unayodhani unayo.
 
Wale baadhi ya watu ambao bado wanaojaribu kumtingisha Rais Magufuli wakidhani atabadilisha njia anayotumia katika utendaji kazi wake wananishangaza sana!

Wanaojaribu kumtingisha inawezekana hawamfahamu vizuri au wanamfahamu vizuri lakini wamejivika upumbavu!

Kwa wale wanamfahamu vizuri, siku alipotoa hii hotuba walijua vizuri nini kitafuata na nini cha kufanya!

Ukitaka kuisikia na kuisoma hotuba, GONGA HII LINK>>Magufuli: Tupo imara, atakayejaribu kutuyumbisha tutambomoa.

Baada ya Freeman Mbowe kutangaza oparesheni UKUTA mwezi Julai 2016, watu kama Edward Lowassa wanaomfahamu vizuri Rais Magufuli waliwashauri CHADEMA waachane na uamuzi huo.

Kuna baadhi ya watu kama Nape Nnauye walijaribu kumtingisha wakidhani atabadilika lakini baadaye wakashauriwa/wakajua habadilishi misimamo yake na wakaamua kufanya kile ambacho Waingereza kwenye methali hukisema, ‘’if you can’t beat them, join them’’.

Baadhi ya wale wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ambao hawakubaliani na kile anachokifanya wameamua kujiunga naye au kukaa kimya kwa sababu wanajua hata wakipiga kelele hawawezi kumbadilisha katika misimamo yake.

Mwandishi mmoja wa Gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo aliwahi kuandika wakati wa Utawala wa Rais Kikwete, ‘’John Pombe Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache katika Serikali ya Kikwete wanaochapa kazi. Yeye sheria ikishapitishwa husimama kidete kuitekeleza hadi nukta ya mwisho hata kama athari zake ni kubwa! Tena ataisimamia kwa ukali na vitisho’’.

Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.

Nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi pia kugusia kuhusu msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake wakati akichangia kwenye bajeti kuu mwezi Juni 2019 ambapo alisema;
"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la KUTOKUWA NA MSIMAMO kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali''.

Zitto aliendelea kusema, "Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita".
LINK>>Zitto Kabwe aipongeza Serikali kwa hili

Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu, Kiranga na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
Magu anabadilika na muoga, angalia kikokotoo au maagizo aliowapa watendaji kukata wapinzani katika uchaguzi huu.

Swala CAG alijificha kwa Supika, Sheria zake alizobadilisha mwanzo kwa ushamba ameshabadili, wakina Mruma walimdanganya Kiko wapi leo hii.

Wamewapiga risasi na kuua raia kwa woga na kukataa kushindana mikwara yake watu wameshazoea na bado kumvamia tu.

Sifa mnazompa ndio zinamtia ukiziwi lakini wabongo huyu baba akitoka ni sherehe.
 
Atadhibitiwa tu!! Tunza hii comment kwenye faili la ubongo wako Tanzania ni zaidi ya uijuavyo Tanzania ni zaidi ya Magufuli.

Tulimpeleka Magufuli Ikulu ili apambane na ufisadi sio kukimbizana na wakina Mbowe matokeo yake anasamehe wezi na pesa wanazolipa hatujui zinaenda wapi amekuwa mpora nchi na mtu asiyefata haki za binadamu yeye ataondoka tu na Tanzania itabaki.
Ahahahaha!
 
Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!
umeongea kwa uhakika kabisa kwamba si msukuma mimi nilidhani alieanzisha hizi habari hizi alikuwa analenga kupunguza uungaji mkono wa wasukuma kwa magufuli kuwa si mwenzao sababu ya kufikiri hivi ni kuwa magufuli hakujiita msukuma kwa vile alikuwa maeteuliwa kugombea urais najua ni msukuma miaka yote tangu tangu akiwa mkemia wa chama cha ushirika cha Nyanza wala hakuwa anajua kuwa sikumoja atakuwa Rais ,unaweza nisahihisha kwa hilo
[/QUOTE]
Hatuna wasukuma wenye roho mbaya namna hiyo.
 
Hatuna wasukuma wenye roho mbaya namna hiyo.
[/QUOTE]
Hakuna ukweli katika hilo wapo wengi tena wengine zaidi yake tusitake kuaminisha watu kuwa kuna watu au kabila halina mawaa hulka au tabia za mtu hutegemea makuzi na malezi yake leo hii wamerikani waseme trump si mmoja wao kwa kuwa tu kuna maamuzi yake yako tofauti na wanachoamini huo ni unakuwa unafiki
 
Boss Kalamu1 Pole zako sana, Naona unajaribu kunitoa kwenye mada, Tumetumia muda mwingi kujibizana kuliko kushauri na kutoa maoni ya kujenga Taifa. Nishakuambia na narudia tena, Unafiki wako na U Bendera fuata upepo wako ni kwa sababu ya kujali Tumbo lako tu, hauna lingine, hii ni Post yangu ya mwiko, kukupa KIKI usiyostahili. Unajiita Kalamu na sijaona Kalamu yoyote. Hoja hujibiwa kwa HOJA.

Kuhusu kunidharau, nishakuambia, haunilishi, haunivishi, dharau zako hazizuii ridhiki yangu, haunijui, sikujui, yaani ni wewe tu ndio unayeumia. Eti, misimamo??? !!! Tunataka Watu au Kiongozi au Viongozi wenye Misimamo yenye Tija kwa Taifa, Misimamo inayojenga Umoja wa Taifa, Misimamo inayoimarisha Msingi mizuri ya Sheria na Katiba yetu, Misimamo inayojali Utu wa Mtu, Misimamo isiyokuwa na Unafiki ndani yake.

Mimi sijawahi, na sitawahi kukaa na kuparamia na kujibishana na mtu wa watu, ni wewe tu, kwanza sijui kwanini nakupa KIKI na Hadhi ya kujibiwa na mimi, Mshukuru sana MUNGU aka ALLAH kwa hilo.

Tamati na Mwisho, basi tufanye UMESHINDA Boss, ili ukachukue Buku 7 zako pale Lumumba.


Naona ujumbe umefika na kueleweka.
Basi tulia. usiwe unaparamia tu kujibishana na watu bila ya kujua misimamo yao ni ipi. Ungetumia muda kidogo tu kuangalia ninayoyaamini mimi na kuyaandika humu JF usingethubutu kuandika uliyoandika kunijibu hapa.

Nakudharau kwa maandishi yako ya kipuuzi humu. Maandishi yako yote niliyoyasoma kwenye mada hii yanaonyesha wazi kuwa hustahiri heshima unayodhani unayo.
 
Wale baadhi ya watu ambao bado wanaojaribu kumtingisha Rais Magufuli wakidhani atabadilisha njia anayotumia katika utendaji kazi wake wananishangaza sana!

Wanaojaribu kumtingisha inawezekana hawamfahamu vizuri au wanamfahamu vizuri lakini wamejivika upumbavu!

Kwa wale wanamfahamu vizuri, siku alipotoa hii hotuba walijua vizuri nini kitafuata na nini cha kufanya!

Ukitaka kuisikia na kuisoma hotuba, GONGA HII LINK>>Magufuli: Tupo imara, atakayejaribu kutuyumbisha tutambomoa.

Baada ya Freeman Mbowe kutangaza oparesheni UKUTA mwezi Julai 2016, watu kama Edward Lowassa wanaomfahamu vizuri Rais Magufuli waliwashauri CHADEMA waachane na uamuzi huo.

Kuna baadhi ya watu kama Nape Nnauye walijaribu kumtingisha wakidhani atabadilika lakini baadaye wakashauriwa/wakajua habadilishi misimamo yake na wakaamua kufanya kile ambacho Waingereza kwenye methali hukisema, ‘’if you can’t beat them, join them’’.

Baadhi ya wale wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ambao hawakubaliani na kile anachokifanya wameamua kujiunga naye au kukaa kimya kwa sababu wanajua hata wakipiga kelele hawawezi kumbadilisha katika misimamo yake.

Mwandishi mmoja wa Gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo aliwahi kuandika wakati wa Utawala wa Rais Kikwete, ‘’John Pombe Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache katika Serikali ya Kikwete wanaochapa kazi. Yeye sheria ikishapitishwa husimama kidete kuitekeleza hadi nukta ya mwisho hata kama athari zake ni kubwa! Tena ataisimamia kwa ukali na vitisho’’.

Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.

Nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi pia kugusia kuhusu msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake wakati akichangia kwenye bajeti kuu mwezi Juni 2019 ambapo alisema;
"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la KUTOKUWA NA MSIMAMO kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali''.

Zitto aliendelea kusema, "Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita".
LINK>>Zitto Kabwe aipongeza Serikali kwa hili

Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu, Kiranga na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
Hujagusia yaliyompata Tundu Lissu
 
Boss @Kalamu1 Pole zako sana, Naona unajaribu kunitoa kwenye mada, Tumetumia muda mwingi kujibizana kuliko kushauri na kutoa maoni ya kujenga Taifa. Nishakuambia na narudia tena, Unafiki wako na U Bendera fuata upepo wako ni kwa sababu ya kujali Tumbo lako tu, hauna lingine, hii ni Post yangu ya mwiko, kukupa KIKI usiyostahili. Unajiita Kalamu na sijaona Kalamu yoyote. Hoja hujibiwa kwa HOJA.
Katika mistari minne tu unajichanganya, hivi kweli wewe unazo kichwani?
 
Nampeni more 5 years ili azidi leta maemdeleo tuki quote maneno ya hayati mwl. Julius kambarage nyerere anasema. "Kuna watu katiba suala la maemdeleo wanadhani ni jambo la kubabaisha babaisha, hakuna hili jambo ni very serious"
 
Raisi usipuuze wanao kusema vibaya wanakupenda pia Kwa njia tofauti na njia uliyoizoea
 
Back
Top Bottom