Kuna baadhi ya watu bado hawajamuelewa Rais Magufuli!

Wale baadhi ya watu ambao bado wanaojaribu kumtingisha Rais Magufuli wakidhani atabadilisha njia anayotumia katika utendaji kazi wake wananishangaza sana!

Wanaojaribu kumtingisha inawezekana hawamfahamu vizuri au wanamfahamu vizuri lakini wamejivika upumbavu!

Kwa wale wanamfahamu vizuri, siku alipotoa hii hotuba walijua vizuri nini kitafuata na nini cha kufanya!

Ukitaka kuisikia na kuisoma hotuba, GONGA HII LINK>>Magufuli: Tupo imara, atakayejaribu kutuyumbisha tutambomoa.

Baada ya Freeman Mbowe kutangaza oparesheni UKUTA mwezi Julai 2016, watu kama Edward Lowassa wanaomfahamu vizuri Rais Magufuli waliwashauri CHADEMA waachane na uamuzi huo.

Kuna baadhi ya watu kama Nape Nnauye walijaribu kumtingisha wakidhani atabadilika lakini baadaye wakashauriwa/wakajua habadilishi misimamo yake na wakaamua kufanya kile ambacho Waingereza kwenye methali hukisema, ‘’if you can’t beat them, join them’’.

Baadhi ya wale wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ambao hawakubaliani na kile anachokifanya wameamua kujiunga naye au kukaa kimya kwa sababu wanajua hata wakipiga kelele hawawezi kumbadilisha katika misimamo yake.

Mwandishi mmoja wa Gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo aliwahi kuandika wakati wa Utawala wa Rais Kikwete, ‘’John Pombe Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache katika Serikali ya Kikwete wanaochapa kazi. Yeye sheria ikishapitishwa husimama kidete kuitekeleza hadi nukta ya mwisho hata kama athari zake ni kubwa! Tena ataisimamia kwa ukali na vitisho’’.

Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.

Nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi pia kugusia kuhusu msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake wakati akichangia kwenye bajeti kuu mwezi Juni 2019 ambapo alisema;
"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la KUTOKUWA NA MSIMAMO kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali''.

Zitto aliendelea kusema, "Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita".
LINK>>Zitto Kabwe aipongeza Serikali kwa hili

Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu,, Kiranga na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
Kutokana na misimamo yake ya kibabe na kishamba ndio maana maiti zinaokotwa fukweni kwenye viroba, wapinzani wanapotezwa, wanaoshambuliwa kwa risasi huku kodi zetu zikitumika kama pesa yake binafsi. Nchi haijawahi kuwa na rais wa hovyo kama huyu
 
Umefanya research kabla ya kuleta huu uzi ? kumbuka mimi sijui hayo usemayo kama ni kweli au uongo ila kuna kitu/vitu ulivyoweka vina makosa.., sasa kama umeweza kukosea hapo kwanini usikosee pengine..., hence umuhimu wa kuandika unachokielewa / una uhakika nacho no matter how minor.... Kiranga
Mkuu;
Ndio maana nikakuomba uonyeshe vitu ambavyo nimeleta vina makosa!
 
Mkuu;
Unajaribu kuniondoa kwenye msingi wa mada yangu tuanze kujadili suala ambalo linahitimishwa na hisia zako.

Samahani siwezi kujadili hisia zako kwa sababu hisia unazijua mwenyewe!

Kwani hii mada yako ulipoileta hapa jukwaani inabeba hisia za watu wote humu ndani au ni hisia zako tu?
 
Inatawaliwa na ccm, je ni kwa ridhaa ya wananchi wote?
Mkuu;
Hakuna kiongozi wa kisiasa anayekuwa kwenye madaraka kwa ridhaa ya wananchi wote. Unatakiwa kwanza uelewe hii kanuni ambayo hata mwenye akili ya kawaida anaweza kuielewa!
 
Mbona kawatumbua na wakristu..acha lawama za kidini

Waislam wengine ni WAJINGA KILA SITU MNAHISI MNAONEWA

ASSAD KAMTUMBUA SIO KWASABABU NI MUISLAM

Waliotumbuliwa sio waadilifu, lakini huyu ni muadilifu, na kikatiba alistahili kuendelea, ila misimamo yake ya kiuadilifu na dini yake ndio vilivyogharimu ajira yake.
 
Mbona kawatumbua na wakristu..acha lawama za kidini

Waislam wengine ni WAJINGA KILA SITU MNAHISI MNAONEWA

ASSAD KAMTUMBUA SIO KWASABABU NI MUISLAM
Mkuu;
Mimi sikutaka hata kuingia kwenye hoja ya huyo unayemjibu kwa sababu nadhani lengo lake ni kutaka tuanze kujadili hoja ambazo anazijenga kwa hisia zake.
 
Mkuu;
Ndio maana nikakuomba uonyeshe vitu ambavyo nimeleta vina makosa!
Moja ingawa ni arguably kwamba anasimamia sheria pindi inapopitishwa..., ila mpaka sasa tuona anasimamia kila anachotaka hata kama ni kupindisha sheria...

Mbili ambayo ni minor.., kwamba wasikuma wana msimamo hence example mojawapo Kiranga...

Sasa kama umepotoka hapo kwanini usipotoke pengine ?
 
Kutokana na misimamo yake ya kibabe na kishamba ndio maana maiti zinaokotwa fukweni kwenye viroba, wapinzani wanapotezwa, wanaoshambuliwa kwa risasi huku kodi zetu zikitumika kama pesa yake binafsi. Nchi haijawahi kuwa na rais wa hovyo kama huyu
Umeandika, ''Nchi haijawahi kuwa na Rais wa hovyo kama huyu''

Nadhani tatizo lako huijui historia ya Tanzania!
 
Mkuu;
Hakuna kiongozi wa kisiasa anayekuwa kwenye madaraka kwa ridhaa ya wananchi wote. Unatakiwa kwanza uelewe hii kanuni ambayo hata mwenye akili ya kawaida anaweza kuielewa!

Kama ni hivyo kwanini asiheshimu mfumo unaotambua kuwa sio wote wanamkubali? Mfumo huo wakutambua walio na mtazamo tofauti na wake ni upinzani nao upo kisheria. Kwanini haheshimu mfumo huu, je hiyo misimamo lengo lake ni kuvuruga mifumo iliyopo kisheria?
 
Moja ingawa ni arguably kwamba anasimamia sheria pindi inapopitishwa..., ila mpaka sasa tuona anasimamia kila anachotaka hata kama ni kupindisha sheria...

Mbili ambayo ni minor.., kwamba wasikuma wana msimamo hence example mojawapo Kiranga...

Sasa kama umepotoka hapo kwanini usipotoke pengine ?
Mkuu;
Kama hoja yako ni kabila la Kiranga
Ninavyofahamu kiranga ni Msukuma ambaye amekulia Dar na Ughaibuni!
 
Ni hii misifa ya kijinga kijinga ndio imetufikisha hapa. Tumeamua kurudi kwenye ujima and barbarism.Tunauwa hata zile strong institutions chache zilizobakia in favour of idiocy na tunaona ni sawa,siku moja historia itatuhukumu vibaya sana. Watoto na wajukuu wetu watatuuliza, tulikuwa wapi?
 
Mkuu;
Mimi sikutaka hata kuingia kwenye hoja ya huyo unayemjibu kwa sababu nadhani lengo lake ni kutaka tuanze kujadili hoja ambazo anazijenga kwa hisia zake.

Kwani huyu uliyemquote huu mjadala wako ni sehemu ya hisia zake? Au ww unawaza kwa niaba yake kiasi kwamba hisia zako ni lazima ziwiane na zake?
 
Atadhibitiwa tu!! Tunza hii comment kwenye faili la ubongo wako Tanzania ni zaidi ya uijuavyo Tanzania ni zaidi ya Magufuli.

Tulimpeleka Magufuli Ikulu ili apambane na ufisadi sio kukimbizana na wakina Mbowe matokeo yake anasamehe wezi na pesa wanazolipa hatujui zinaenda wapi amekuwa mpora nchi na mtu asiyefata haki za binadamu yeye ataondoka tu na Tanzania itabaki.
Hii inchi ina miongozo yake watu hawaelewi kuwa kuna siku atathibitiwa mpaka hawataamini.inchi ina misingi yake ambayo haiwezi kukiukwa.
 
Mkuu;
Nadhani saver za Jamiiforums zitaitunza comment yako!

Ni kweli Tanzania ni zaidi ya niijuavyo lakini nikiangalia kalenda inasomeka ni miaka minne tangu aingie Ikulu kama Rais wa Tanzania!
Muda ni mwl .mzuri atadhitiwa mpaka msiamini
 
Boss Ng'wamapalala Mh. Rais nae ni Binadamu kama wewe na mimi, Mh. Rais nae ana mapungufu kama wewe na mimi. Kuna maeneo Mh. Rais anaudhubutu sana, na kuna maeneo Mh. Rais kachemka.

Tatizo letu Watanzania na Wananchi ni Unafiki, Sasa hivi Mh. Rais kazungukwa na watu Wanafiki sana, kazi yao ni kupamba na kusifia tu. Ukishaona Mtu muda wote anakusifia tu, jua kuna jambo si bure.

Pamba na Sifia kwa kujenga HOJA, hata mtu akisoma anakubali.

Wale baadhi ya watu ambao bado wanaojaribu kumtingisha Rais Magufuli wakidhani atabadilisha njia anayotumia katika utendaji kazi wake wananishangaza sana!

Wanaojaribu kumtingisha inawezekana hawamfahamu vizuri au wanamfahamu vizuri lakini wamejivika upumbavu!

Kwa wale wanamfahamu vizuri, siku alipotoa hii hotuba walijua vizuri nini kitafuata na nini cha kufanya!

Ukitaka kuisikia na kuisoma hotuba, GONGA HII LINK>>Magufuli: Tupo imara, atakayejaribu kutuyumbisha tutambomoa.

Baada ya Freeman Mbowe kutangaza oparesheni UKUTA mwezi Julai 2016, watu kama Edward Lowassa wanaomfahamu vizuri Rais Magufuli waliwashauri CHADEMA waachane na uamuzi huo.

Kuna baadhi ya watu kama Nape Nnauye walijaribu kumtingisha wakidhani atabadilika lakini baadaye wakashauriwa/wakajua habadilishi misimamo yake na wakaamua kufanya kile ambacho Waingereza kwenye methali hukisema, ‘’if you can’t beat them, join them’’.

Baadhi ya wale wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ambao hawakubaliani na kile anachokifanya wameamua kujiunga naye au kukaa kimya kwa sababu wanajua hata wakipiga kelele hawawezi kumbadilisha katika misimamo yake.

Mwandishi mmoja wa Gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo aliwahi kuandika wakati wa Utawala wa Rais Kikwete, ‘’John Pombe Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache katika Serikali ya Kikwete wanaochapa kazi. Yeye sheria ikishapitishwa husimama kidete kuitekeleza hadi nukta ya mwisho hata kama athari zake ni kubwa! Tena ataisimamia kwa ukali na vitisho’’.

Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.

Nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi pia kugusia kuhusu msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake wakati akichangia kwenye bajeti kuu mwezi Juni 2019 ambapo alisema;
"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la KUTOKUWA NA MSIMAMO kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali''.

Zitto aliendelea kusema, "Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita".
LINK>>Zitto Kabwe aipongeza Serikali kwa hili

Misimamo ya Rais Magufuli(ubishi na kusimamia anachokiamini) haiwezi kuwashangaza wale ambao wanajua tabia za Wasukuma. Ni kweli Rais Magufuli siyo Msukuma lakini kwa sababu amekulia katika mazingira ya Wasukuma ndio maana amechukua moja ya tabia ya Wasukuma!

Kama ukitaka kujua tabia halisi za Wasukuma (ubishi na kusimamia wanachokiamini) basi jaribu kufanya majadiliano na Nyani Ngabu, Kiranga na Pascal Mayalla ambao ni wana Jamiiforums! 😀😀😀
 
Huwa nawashangaa sana baadhi ya watu waonapiga kelele za kisiasa wakidhani Rais Magufuli ataweza kubadilika! HAWEZI.
Sijafika huko chini, lakini mstari huu umenishawishi nikatae yote uliyoandika.

Wananchi wakikataa hatabadilika?

Alipokuwa waziri, hakubadilishwa? Ghorofa la Tanesco mbona lilikaa pale, na yapo mengi aliyoonywa na akabadilika!

Huyo mtu asiyebadilika ni kiongozi wa namna gani yeye? Akikosea bado ang'ang'anie kuwa yeye habadiliki; hiyo ndio sifa tunayotafuta kiongozi wetu ajulikane nayo?

Bado muda ni mbichi sana kutoa hitimisho kama hili.

Hivi wale wasichana wenye mimba vipi?
 
Ni kweli ana msimamo na chuki ya wazi dhidi ya wapinzani na waislamu. Baadhi ya misimamo yake ni kuhakikisha anaua vyama vya upinzani kwa kutumia madaraka yake. Pia kwenye utawala wake waisilamu wana nafasi finyu. Angalia msimamo wake dhidi Assad muisilamu muadilifu mwenye msimamo katika usimamizi wa fedha za umma. Ameamua kumtoa mbali ya uadilifu wake, ameona bora ampe mkristo mzembe kwani kwake uislamu ni nongwa hasa ukiwa na msimamo, na weledi katika kazi. Misimamo hii iko wazi dhidi ya wapinzani na waisilamu, je katika mazingira hayo tutegemee Tanzania salama? Muda utaamua.
Wewe ni mpumbavu Makamu wake ni dini gani labda na Waziri Mkuu ni dini emu tuambie!! Usitake kuhusisha mambo ya Rais na udini kaa pembeni na fikiria kwanza.
 
Boss Ng'wamapalala Mh. Rais nae ni Binadamu kama wewe na mimi, Mh. Rais nae ana mapungufu kama wewe na mimi. Kuna maeneo Mh. Rais anaudhubutu sana, na kuna maeneo Mh. Rais kachemka.

Tatizo letu Watanzania na Wananchi ni Unafiki, Sasa hivi Mh. Rais kazungukwa na watu Wanafiki sana, kazi yao ni kupamba na kusifia tu. Ukishaona Mtu muda wote anakusifia tu, jua kuna jambo si bure.

Pamba na Sifia kwa kujenga HOJA, hata mtu akisoma anakubali.
Dhana potofu kabisa.
Tukuweke wewe usiyekuwa mnafiki ukamshauri? Hivi kwa nini watu huwa mnapenda sana kupindisha mambo ambayo yapo wazi?

Wewe kama mshauri ungebadilisha nini kwa mtu mwenye tabia yake!
 
Back
Top Bottom