Kuna baadhi ya watu ukiwasalimia hawaitikii salamu

Mimi mtu nikimsalimia asipoitika na nikithibitisha kafanya makusudi ndio imetoka hiyo hatopata tena salam yangu.

Na sio kuitika tu uitike sawa na nilivyokusalimia, sio nakusalimia kwa bashasha halafu we unaitika kama shabiki wa simba aliyekumbuka kipigo cha 5 kwa 1. Ukileta madeko kwenye kuitika nayo sikusalimii tena.
 
Binafsi salam ya shkamoo na marahaba sitoi wala sipendi kuzipokea. Mtu akiniamkia shkamoo nitapokea tu ili asijisikie vibaya ila huwa simwambii mtu shkamoo. Salam ya kishenzi sana...
 
Hapa kuna mwanajesh kahamia ana miez miwili sasa ajabu mkewe hanisalimii kbs mpk mi nimsalimie hata tukikutana wawili hanisalimii nikimkuta amekaa na mwanamke wng ile akiniona kwa mbali anaondoka faster huwa najiuliza spati pcha ana matatzo gn.
 
Unamuamkia mtu kwa nia nzuri lakini anakutazama kama hajasikia, unapotezea, kesho tena unamsalimia lakini bado haitikii salamu, hujawahi kosana nae wala kupishana kauli, hawa watu wapo ila wanakera sana, hasa hasa wadada.

sijui ni stress za maisha au wanaona huna hadhi ya kusalimiana nae,

Najua hata wewe ushakutana na chanagamoto kama hiyo.
Mkuu! Hawa wapo wengi sana. Kuna kijana alikuwa anakuja kwangu mara kwa mara na ikazoeleka nami nikamfanya kama mdogo wangu wa mwisho.
Mwisho wa siku akawa anasimulia habari mbalimbali za mapambano ya maisha. Nami kwa kuwa alikuwa kama ndugu sasa nikamshauri afungue biashara ya duka.
Kwa jinsi alivyokuwa na hofu niliamua kutoa usaidizi wangu ili biashara ikae vizuri. Baada ya biashara kuimalika nikamshauri amuweke mkewe dukani, nae aendelee na mapambano mengine.
Ukweli Mungu kawasaidia wamepata kausafiri wana tumifugo nk. Basi mkewe kiburi kimeingia hataki hata kusalimia, anajifanya hakuoni hata ukimsalimia.
Binadamu wana kazi mzee!
 
Tenda wema nenda zako, hayo ndo malipo ya wema uliowatendea.
 
Sasaivi silamii mtu shikamoo ata awe anaweza nizaa salamu ni habari yako uhali gani, habari za muda n.k pia ninavyomsalimu nahakikisha amenitizama,
pia sina kawaida ya kumsalimia mtu ambae kanikuta mpka nimkute ndo nitaanza kumsalimia, usitegemee umekuja ukanikuta nimekaa nikuanze kukusalimia never labda mzazi wangu tu, nami nikifika sehemu nikakuta watu lazima niwasalimie
 
Unamuamkia mtu kwa nia nzuri lakini anakutazama kama hajasikia, unapotezea, kesho tena unamsalimia lakini bado haitikii salamu, hujawahi kosana nae wala kupishana kauli, hawa watu wapo ila wanakera sana, hasa hasa wadada.

sijui ni stress za maisha au wanaona huna hadhi ya kusalimiana nae,

Najua hata wewe ushakutana na chanagamoto kama hiyo.
Nikupe shule kidogo.
1.Tunamsalimu mtu hatumsalimii

2. Tunamuamkia SHIKAMOO mzazi,Boss wako kazini,na yeyote alokuzidi umri. Shikamoo ni maamkizi na si salamu.
Hivyo amkia watatu tu.
 
Mkuu! Hawa wapo wengi sana. Kuna kijana alikuwa anakuja kwangu mara kwa mara na ikazoeleka nami nikamfanya kama mdogo wangu wa mwisho.
Mwisho wa siku akawa anasimulia habari mbalimbali za mapambano ya maisha. Nami kwa kuwa alikuwa kama ndugu sasa nikamshauri afungue biashara ya duka.
Kwa jinsi alivyokuwa na hofu niliamua kutoa usaidizi wangu ili biashara ikae vizuri. Baada ya biashara kuimalika nikamshauri amuweke mkewe dukani, nae aendelee na mapambano mengine.
Ukweli Mungu kawasaidia wamepata kausafiri wana tumifugo nk. Basi mkewe kiburi kimeingia hataki hata kusalimia, anajifanya hakuoni hata ukimsalimia.
Binadamu wana kazi mzee!
Pole sana mkuu. Wanawake wana tabia za ajabu sana, si unaona hata kwenye huduma customer care ya wengi wao ni mbaya kwa wateja. Endela na maisha yako tu, muda ni kila kitu kwenye maisha.
 
Back
Top Bottom