Kuna baadhi ya watu ukiwasalimia hawaitikii salamu

Kuna baadhi ya watu ukiwasalimia hawaitikii salamu

Mim salamu ya shikamoo nilishaacha kitambo sana ,wazazi nyumbani nawasalimu kwa lugha ya kikoloni Good morning, afternoon au evening inatosha hao wengine kitaa salamu ya shkamoo unawapa wanakutazama tu machoni ,so salamu yangu ni habari za saa hizi au za asubui etc imetosha
 
Unamuamkia mtu kwa nia nzuri lakini anakutazama kama hajasikia, unapotezea, kesho tena unamsalimia lakini bado haitikii salamu, hujawahi kosana nae wala kupishana kauli, hawa watu wapo ila wanakera sana, hasa hasa wadada.

sijui ni stress za maisha au wanaona huna hadhi ya kusalimiana nae,

Najua hata wewe ushakutana na chanagamoto kama hiyo.
Kumbe bado wapo wanaosalimia siku hizi?🤔

Hawa nilionao naona huwa wanakatiza tu kama vishandu wale wa boda

Akikusalimia tu basi jiandae kisaikolojia kuna sehemu kakwama anataka umsaidie
 
Kuna mzee mmoja hivi anajifanyaga Bado kijana coz Kila kukicha unakuta kapaka piko kichwani

Kila ukimsalimia shikamoo!! Mzee!

Anakujibu Asante!

Me nakomaa nae tu.. Kuna siku nikamkuta Yuko na wazee wenzake ilipofika zamu yake kumsalimu nikaongeza sauti!

Mzeee Shikamooooo!!! Mbona aliipokea but alinikata jicho hilo[emoji3166]
 
kuna mama mmoja hivi nilimpa salam akanikata jicho la chuki, akanicheki juu mpaka chini aisee halafu akayeya...

nusu saa baadae akarudi akanikuta namhesabia jirani yake laki moja na nusu.

Yule mama ikabidi ashindwe aende au arudi, asalimie au akauke..

nilivyoondoka tu jirani yake akampa data zangu...

kesho yake mchana napigiwa simu na namba ngeni, sauti ya mwanamke, inahitaji kuniona, kuna emergence eti... hahaha..

kwenda, namkuta yule mama sura limemshuka kama lishabiki la Yanga lililofungwa goli 3 na waarabu.. eti na yeye anataka KUKOPA LAKI...

TAFUTENI HELA, SALAM ACHIENI WATOTO WADOGO..
Mkuu umenikosha hapo kwenye lishabiki la uto
 
Back
Top Bottom