Kuna baadhi ya watu ukiwasalimia hawaitikii salamu

Mim salamu ya shikamoo nilishaacha kitambo sana ,wazazi nyumbani nawasalimu kwa lugha ya kikoloni Good morning, afternoon au evening inatosha hao wengine kitaa salamu ya shkamoo unawapa wanakutazama tu machoni ,so salamu yangu ni habari za saa hizi au za asubui etc imetosha
 
Kumbe bado wapo wanaosalimia siku hizi?🤔

Hawa nilionao naona huwa wanakatiza tu kama vishandu wale wa boda

Akikusalimia tu basi jiandae kisaikolojia kuna sehemu kakwama anataka umsaidie
 
Fresh,hivi ndivyo inatakiwa tusalimiane kaka mtu🤣
Jumapili Leo vipi nawe ni muumini au upande wa pili?
Inatakiwa kuwa hivi Dadamtu, mambo ya kunizeesha sitaki🤣
Leo zamu yako nadhani, jana ilikuwa zamu yangu😝
 
Kuna mzee mmoja hivi anajifanyaga Bado kijana coz Kila kukicha unakuta kapaka piko kichwani

Kila ukimsalimia shikamoo!! Mzee!

Anakujibu Asante!

Me nakomaa nae tu.. Kuna siku nikamkuta Yuko na wazee wenzake ilipofika zamu yake kumsalimu nikaongeza sauti!

Mzeee Shikamooooo!!! Mbona aliipokea but alinikata jicho hilo[emoji3166]
 
Mkuu umenikosha hapo kwenye lishabiki la uto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…