Kuna Basi la Mwendokasi lilikuwa linapita njia ambayo sio yake, limegonga mtu kwenye Zebra, amefariki Kimara

Kuna Basi la Mwendokasi lilikuwa linapita njia ambayo sio yake, limegonga mtu kwenye Zebra, amefariki Kimara

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Habari, huku Mtaani kwetu kuna jamaa amefariki baada ya kupata ajali ya kugonjwa na basi la Mwendokasi jioni mida ya saa moja, Machi 8, 2025 wakati anavuka kwenye Zebra.

Mashuhuda wanasema kuwa kuna Basi la Mwendokasi ambalo lilikuwa linapita njia ambayo siyo ya kwake, ilikuwa ikitokea Ubungo kwenda Kimara lakini ikapita katika njia ya kutokea Kimara kwenda Ubungo.

Hivyo, jamaa wakati anavuka alikuwa ameelekeza macho upande mwingine, bahati mbaya ni kuwa basi hilo likamgonga kwa kuwa lilikuwa katika nia iliyokuwa yake na halikusimama baada ya hapo.

Daniel.jpg
Marehemu alikuwa ni Dalali, zamani alikuwa muuza chipi mitaa ya Korogwe anafahamika kwa jina la Daniel Anderson Apolo, alibebwa na wenzake akapelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambapo mwili wake upo huko mpaka sasa.

Wenyeji wa Kimara wanamjua na vizuri na wengi tupo hapa kwenye majonzi mpaka muda huu naandika andiko hili.

Huyu mtu ni mwenyeji wa Singida lakini aliondoka kwao miaka mingi, hivyo ndugu zake wengi hawajulikani kiivyo, lakini taarifa za msiba wake zipo zaidi hapa Kimara Korogwe, kinachoendelea ni michango ili kukamilisha mchakato wa kufanikisha kumzika.

Ukifika Korogwe Baa au kwa Pati napo ndipo ambapo kuna taarifa kwa ukaribu, kwa anayehitaji kufika karibuni.

Kinachosikitisha ni kuwa Mwendokasi hawajatoa tamko lolote na wanaweza kukaa kwa kuwa basi lenyewe halikusimama.

Tunaomba Uongozi wa Mabasi ya Mwendokasi mje mtoe hata rambirambi, kama nikivyoeleza msiba upo hapa Korogwe Baa au mnaweza kuulizia Kwa Pati.

==============================

DART WASEMA SIO KWELI
JamiiForums imewasiliana na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kupitia kwa Ofisa wa Kitengo cha Habari DART, Elias Malima, awali alisema anafuatilia baada ya kupewa taarifa hiyo.

Baadaye akarejea na kusema “Nimefuatilia taatifa hizo sio za kweli, hakuna popote ambapo imeripotiwa juu ya tukio hilo na wakati huu ambapo kuna watu wengi wnaweza kuripoti ingekuwa imeshajulikana tu.

“Huku kwetu hatuna ripoti ya aina hiyo, pia suala la kusema basi lilikuwa linapita njia ambayo siyo yake sijawahi kusikia.”

 
Kifo sijawahi kukielewa kabisa ,jamaa apumzike kwa amani.

Shangazi yangu alikuja kumuuguza uncle hapo Dar , uncle alikuwa hajitambui kabisa alifanyiwa operation kama mara mbili maana wanasema alifumuka mshono hapo Muhimbili alibaki kungojes kifo tu.

Shangazi siku moja anavuka pale keko maduka matatu anaelekea upande wa pili ,alikuwa anatokea hapa Toroli ..Basi akapigwa mziga alikuwa na chupa za uji wa ugonjwa ambaye ni uncle, alikuwa awahisha Muhimbili.

Shangazi akafa hapo hapo na mgonjwa akafa baada ya mwezi . Shangazi alitoka Tanga kaacha wanawe kaenda kumuhudumia mgonjwa mara moja .​
 
Kila anayegongwa na mwendokasi ni lazima afariki yule jamaa wa Kisutu tu ndio alipona, na siku hizi watu wanagongwa sana na Mwendokasi, juzi tu ilikuwa Magomeni bodaboda kachimbwa.. Mwaka jana kuna ndugu yangu kagongwa na mwendokasi kapewa ulemavu wa muda police wakawa wanamlazimisha aandike kagongwa na Noah
 
Mwendokasi sijui wanashida gani
Hiyo tarehe nane niko kwenye bajaji, hapo korogwe, ghafla tunashtuka mwendokasi inaelekea kimara ipo upande wa kuelekea Ubungo, tena ipo kasi
Pengine ndo hiyo iligonga hapo kwenye Zebra🙌😓.
Wanajifanyia tu wanavyotaka, madai yao madereva ni wanajeshi.
 
Back
Top Bottom