Habari, huku Mtaani kwetu kuna jamaa amefariki baada ya kupata ajali ya kugonjwa na basi la Mwendokasi jioni mida ya saa moja, Machi 8, 2025.
Mashuhuda wanasema kuwa kuna Basi la Mwendokasi ambalo lilikuwa linapita njia ambayo siyo ya kwake, ilikuwa ikitokea Ubungo kwenda Kimara lakini ikapita katika njia ya kutokea Kimara kwenda Ubungo.
Hivyo, jamaa wakati anavuka alikuwa ameelekeza macho upande mwingine, bahati mbaya ni kuwa basi hilo likamgonga kwa kuwa lilikuwa katika nia iliyokuwa yake na halikusimama baada ya hapo.
Marehemu alikuwa ni Dalali, zamani alikuwa muuza chipi mitaa ya Korogwe anafahamika kwa jina moja la Daniel, alibebwa na wenzake akapelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambapo mwili wake upo huko mpaka sasa.
Wenyeji wa Kimara wanamjua na vizuri na wengi tupo hapa kwenye msiba mpaka muda huu naandika andiko hili.
Huyu mtu ni mwenyeji wa Singida lakini aliondoka kwao miaka mingi, hivyo ndugu zake wengi hawajulikani kiivyo, lakini msiba kwa sasa upo hapa Kimara Korogwe, kinachoendelea ni michango ili kukamilisha mchakato wa kufanikisha kumzika.
Ukifika Korogwe Baa au kwa Pati napo ndipo msiba ulipo, kwa anayehitaji kufika karibuni.
Kinachosikitisha ni kuwa Mwendokasi hawajatoa tamko lolote na wanaweza kukaa kwa kuwa basi lenyewe halikusimama.
Tunaomba Uongozi wa Mabasi ya Mwendokasi mje mtoe hata rambirambi, kama nikivyoeleza msiba upo hapa Korogwe Baa au mnaweza kuulizia Kwa Pati.
DART WASEMA SIO KWELI
JamiiForums imewasiliana na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kupitia kwa Ofisa wa Kitengo cha Habari DART, Elias Malima, awali alisema anafuatilia baada ya kupewa taarifa hiyo.
Baadaye akarejea na kusema “Nimefuatilia taatifa hizo sio za kweli, hakuna popote ambapo imeripotiwa juu ya tukio hilo na wakati huu ambapo kuna watu wengi wnaweza kuripoti ingekuwa imeshajulikana tu.
“Huku kwetu hatuna ripoti ya aina hiyo, pia suala la kusema basi lilikuwa linapita njia ambayo siyo yake sijawahi kusikia.”