Kuna Basi la Mwendokasi lilikuwa linapita njia ambayo sio yake, limegonga mtu kwenye Zebra, amefariki Kimara

Ubaya magari ya mwendokasi hayana makelele yanakua kama yanakunyemelea vile. Na hizi stress na jua la bongo ikatokea liko nyuma yako huwezi sikia. Kama unajifanya umevaa ear pods na limepita njia siyo yake ndiyo kabisa

Lilinikosa Posta na hapo Urafiki. Yalikua kwenye njia zake ila mimi katika kuvuka barabara ndiyo moto ukataka kuwaka
 
Hivi lakini tuweni serious hivi mtu unavaa earpods kwenye msongamano ili iwe nini? Kwa kelele jua na joto hili, foleni na wavuta bangi kupewa leseni tujiandae kufa sana
 
Angalau wewe umejisemea Ukweli, wengi hapa JF uongo mtupu. Uangalifu wakati wa kuvuka Barabara ni shida hapa mjini. Imagine mtu anaamini Zebra siku hizi! Wakati wa JPM sawa ila sasa wakati wa mama, kuamini zebra ni kukitafuta kifo
 
Mabasi ya mwendakasi,gari za serikali,gari za ccm ujiona kama wapo kwenye F1 wakati miundo mbinu yenyewe iwezi kuwa rafiki kwa usalama
Juzi jzi pale magomeni mataa mapipa,ilimgawanyisha boda kiwiliwili,mwili wa boda ukawekwa kwenye Kiribati kupelekwa mwananyamala

Ova
 
Na ile likikugonga kwenye njiaa yake hakuna kesi 😄

Ova
 
Angalau wewe umejisemea Ukweli, wengi hapa JF uongo mtupu. Uangalifu wakati wa kuvuka Barabara ni shida hapa mjini. Imagine mtu anaamini Zebra siku hizi! Wakati wa JPM sawa ila sasa wakati wa mama, kuamini zebra ni kukitafuta kifo
😄

Ova
 
Sasa mbona msemaji wa DART amekanusha, tumuamini nani?
Huyo aliekanusha hana utu hata kidogo,na siku izi mwendokasi wanavunja sheria za barabarani, na mamlaka ziko kimya, watu wanakufa kila kukicha.

Iyo ajali hata mimi nimeishuhudia kwa macho yangu, Mwendokasi kamgonga mtu aliyekuwa kwenye upande wake sahihi.

Mwendokasi lilikuwa lane ambayo sio ya upande wake.

Jamaa mpaka wanampandisha kwenye gari alikuwa bado anapumua kwa mbaali, lakini kwa muonekano wa majeraha ilikuwa ngumu kupona,
 
Hiyo ndiyo ishamalizwa
 
Mwendokasi zamani walikua wanaheshimu hizo zebra, siku hizi wanapita kishada.

Na watembea kwa miguu ni vizuri kuangalia pande zote, juzikati boda ilinikosa kwa hilo la kuamini gari zinatokea uapnde huu tu, kumbe kuna mwehu anapiaha na wenzie.
Mkuu boda wamezidi hiyo kwao kawaida niliwahi isema humu nikaonekana mjinga , jamaa wanaacha nji.a sahihi hivyo ni vyema kucheck pande zote mimi nilisikia tu shati inagongwa KUCHEKI hivi kumbe boda kicha kapita kwa Kasi niloshukuru Mungu tu
 
Hivi viongozi wa taasisi kama hawa, pumzi za kukanusha kipumbafpumbaf huwa wanazitoa wapi na ni kwa faida ya nani?

Angelikuwa ni mtoto wake wa kuzaa angelikanusha ki layman namna hiyo?

Enhe kakurupuka kukanusha, baadaye ukweli ukijulikana ataomba radhi au nd'okupiga kimya?
 
Huyo dereva wa mwendokasi aliyekimbia ajue Kuna kitu kinaitwa KARMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…