Kuna binadamu wanakula jamani, nani aliwahi kukushangaza kwenye sekta ya misosi?

Kuna binadamu wanakula jamani, nani aliwahi kukushangaza kwenye sekta ya misosi?

Mimi huwa nashangaa inakuaje watu wanaweza kula jioni wakati wanaenda kulala binafsi nafungua kinywa asubuhi kidogo na kula mchana, ila nashangaa wanaweza vipi kula milo zaidi ya miwili?
Na miti unapiga kama kawa???
 
Mimi ni wanangu wa kiume wana miaka kati ya 17 na 19, hua wanaamka asubuhi na kuweka wali kwenye rice cooker kwa sababu wakila vitafunio kama mikate hawashibi.

Wanaanza na chai na kitafunio kama starter, halafu wanakula wali wao na mboga watakayokua wamejipikia, Kwa wiki tunamaliza kilo 40 za mchele. Wakiwa wanakula ni kama vita wakimaliza wamelowa jasho na cha kushangaza hawanenepi, ukiwaona huwezi kuamini kiasi cha msosi wanachokula.

Uzuri wote wanapenda kupika na wanajifunza mapishi mapya for fun ili wajifaidie. Kama wazazi tunawasapoti tu hela tu za matumizi wanaenda kuhemea vitu vyao wenyewe.

Niliacha kuwapikia walioifikisha miaka 12 nikahakikisha nimewafundisha basics na kuwanunulia vifaa vya kuwarahisishia mapishi ili wajipikie wenyewe maana sikuweza kukeep up na spidi yao.

Wewe ni nani ambaye unamvulia kofia kwenye hiyo sekta?

View attachment 3239244

View attachment 3239243
Kuna dawa za asili upewe hasa kwa watoto wenye umri wa miaka kuanzia 15-20 katika hali ya kubalance mambo hayo ili wasipitilize
 
Mimi huwa nashangaa inakuaje watu wanaweza kula jioni wakati wanaenda kulala binafsi nafungua kinywa asubuhi kidogo na kula mchana, ila nashangaa wanaweza vipi kula milo zaidi ya miwili?
Miwili tu kama mimi, safi!
ila mimi nakula mchana na jioni, mlo wangu wa kwanza saa sita na nusu mchana.
 
Duuh! Hao wanao ni hatari. Lol

Japo nikiwa kama mzazi pia nakushauri hao wanao walee kwa kuwajengea kwamba kuna leo na kesho nikimaanisha si kila wanachofanya sasa basi uwaache tu sababu unao uwezo wa kuwatimizia.

Kilo 40 za mchele nyingi eti kwa wiki.
Wamerithi kwa wazazi wao sio bure
 
Back
Top Bottom