Kuna binadamu wanakula jamani, nani aliwahi kukushangaza kwenye sekta ya misosi?

Kuna binadamu wanakula jamani, nani aliwahi kukushangaza kwenye sekta ya misosi?

Mimi ni wanangu wa kiume wana miaka kati ya 17 na 19, hua wanaamka asubuhi na kuweka wali kwenye rice cooker kwa sababu wakila vitafunio kama mikate hawashibi.

Wanaanza na chai na kitafunio kama starter, halafu wanakula wali wao na mboga watakayokua wamejipikia, Kwa wiki tunamaliza kilo 40 za mchele. Wakiwa wanakula ni kama vita wakimaliza wamelowa jasho na cha kushangaza hawanenepi, ukiwaona huwezi kuamini kiasi cha msosi wanachokula.

Uzuri wote wanapenda kupika na wanajifunza mapishi mapya for fun ili wajifaidie. Kama wazazi tunawasapoti tu hela tu za matumizi wanaenda kuhemea vitu vyao wenyewe.

Niliacha kuwapikia walioifikisha miaka 12 nikahakikisha nimewafundisha basics na kuwanunulia vifaa vya kuwarahisishia mapishi ili wajipikie wenyewe maana sikuweza kukeep up na spidi yao.

Wewe ni nani ambaye unamvulia kofia kwenye hiyo sekta?

View attachment 3239244
Vyakula vimegawanyika katika makundi makuu matatu fuatilia hapa 1.Vyakula vya kujenga miwili (PROTINI) mfano Mayai, samaki, kuku, Maharage
2.Vyakula vya kulinda mwili (Vitamini) mfano Matunda Yote na mboga mboga za Jani
3. Vyakula vya kuupa mwili nguvu (KABOHAIDRET) mfano Wanga na sukari vyakula vyenye Wanga ni kama Wali, Ugali, Mihogo, Viazi, Sukari mfano Miwa, na vinywaji vyenye sukari ama Matunda yaliyoiva au sio + mafuta such as Parachichi, Karanga, Korosho Hitimisho ukitaka machillii wanenepeane wape vyakula vya kujenga miwili sana (PROTINI)
 
Umeelezea poa sana, nafikiri hawanenepi pia kwa sababu ni wachezaji, wanaenda mazoezi kila siku na wanaburn sana energy.

Nimemention tu mchele ila kiasi cha maharage, mayai na nyama wanachokula siwezi kusema hapa, wataniua 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom