Kuna brand za nguo zilitikisa sana aisee!

Kuna zile tracksuits zilikuwa zimeandikwa OPEL ni za Adidas kama sikosei ila zilibamba sana enzi zile
Mwenzangu tracksuits zile zilikuwa bomba sanaaaa.
Nakumbuka miaka hiyo nilipanda Mohamed trans toka dar kwenda shy basi sasa!!!!! Kwenye bus alikuwepo noorah msanii wa hip hop kama sikosei.. yule kaka alinitafuta mpaka akanipata kupitia hiyo tracksuits ya adidas ilikuwa full white na huku pembeni vi mstari vyekundu.
 
Kuna Jeans zilikua zinatumia jina la Michael Jackson kama Brand name,kitambo sana.
 
LEGS,SAVCO,TOMY HILFIGER,FUBU,PUMA,NIKE NK
 
Yaani zilikuwa nzuri mno zile track suit ukivaa unaonekana mwenyewe.
 
Hapa ndo mnaponichanganya wahenga wa JF.

Hiyo minguo na miviatu ya kale mlivaa lakini likija suala la umri mnajipandisha kwa Gen Z mnajifanya watoto 😹😹😹

Hebu acheni ubabaifu anzeni kupunguza matumizi ya chumvi ni hatari kwa umri wenu..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…